Monday, March 4, 2013

Diwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kata ya Makulu mkoani Dodoma Ally Biringi:'Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Dodoa kinajichanganya na kujikaanga kwa mafuta yake kwa ubaguzi wa Kiitikadi katika kuwahudumia raia wake.

  Bomoa nyumba Njedengwa Dodoma Oktoba 2011
  KUZIMIA, Mama ambaye jina lake halikufahamika alizimia Bommoabomoa Dodoma.
  Mwananchi aliyekuwa na silaha kwenye eneo la bomoabomoa.
 Majeruhi wa Njedengwa Dodoma Oktoba 2011. 5
waandishi wa habari walivyoonja adha ya Mabomu
--

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

DIWANI  wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kata ya Makulu mkoani Dodoma Ally Biringi, amekirushia Makombora Mazito Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani humo akikituhumu kuwa kinajichanganya na kujikaanga kwa mafuta yake kwa ubaguzi wa Kiitikadi katika kuwahudumia raia wake.

Biringi alisema hayo jana kufuatia Kauli ya CCM dhidi ya wapangaji wa Kaya zaidi ya 100 zenye wakazi takribani 1,044 wa Kata ya Kikuyu inayotawaliwa na CCM, waliopanga kwenye nyumba za Mamlaka ya Ustawishaji Makao Mkuu (CDA), waliotakiwa kuhamishwa kwa nguvu Alhamisi, Februari 28, 2013.

Akizungumzia tuhuma hizo Biringi ambaye wananchi humuita Kiboko cha Yusuf Makamba alisema, CCM kinajichanganya kinafanya Siasa na Usanii kwenye Haki za Wananchi wake, ambapo Katibu Mkuu wake wa Mkoa wa Dodoma Albert  Mgumba alipoongea na Wandishi na kusema CCM inaishauri Serikali na CDA itumie Busara na Hekima suala la kuwahamisha kwa nguvu wapangaji hao.

“Sipingi kauli ya kutumia Hekima, Busara kuwahamisha wapangaji ndicho Serikali na CDA inavyotakiwa ifanye, ila CCM haikutoa kauli ya namna hiyo bomoabomoa ya Njedengwa kwa wananchi wa Kata yangu Oktoba 2011, walipigwa Mabomu, kuharibiwa mali na Damu kumwagwa ili kumfurahisha mwekezaji”.

Biringi alisema, Mioyo ya Wananchi walioko kwenye Maeneo na Kata za CCM ni sawa na Mioyo ya wananchi walioko kwenye maeneo yanayotawaliwa na vyama vyote vya upinzani kikiwemo Chadema,  hivyo wote wana fursa sawa ya kutendewa haki kama unavyokata msumeno.

Aidha alisema, kitendo cha CCM kuinua mdogo na kupaza sauti ya utetezi pale tu ambapo utawala uliopo ni wa Chama chake na kuwa likizo maeneo ambayo yanatawaliwa na upinzani, hali hiyo inatafsirika kama ni ubaguzi wa kiitikadi.

No comments:

Post a Comment