Saturday, March 30, 2013

RAMBI RAMBI KUTOKA UJERUMANI KUFUATIA KUANGUKA KWA JENGO DAR
Umoja wa Watanzania Ujerumani umepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kuanguka kwa jengo mjini Dar es Salaam.
tunawapa pole nyingi ndugu na jamaa wa waliopoteza maisha, Umoja Wa Watanzania Ujerumani unaungana na watanzania wote pamoja wafiwa katika maombolezi ya msiba huu mkubwa.

Tunawaombea marehemu wote mungu awaweke mahala pema peponi AMIN


MAKAMU WA RAIS DKT. MOHAMMED GHARIB BILAL AFIKA KUJIONEA JENGO LA GHOROFA 16 LILILOPOROMOKA JIJINI DAR LEO

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia Jengo la Ghorofa 16, lililoporomoka lenyewe leo asubuhi katika Mtaa wa Indra Ghand na Zanaki. Makamu amefika kushuhudia Shughuli za uokoaji ambazo zinaendelea, ambapo hadi sasa idadi ya watu waliofariki imeelezwa kuwa imefikia watatu na waliookolewa wakiwa hai ni 17, kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum, Suleiman Kova.
 Uokoaji ukiendelea.....
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiondoka eneo la tukio baada ya kuangalia Jengo la Ghorofa 16, lililoporomoka lenyewe leo asubuhi katika Mtaa wa Indra Ghand na Zanaki. Makamu amefika kushuhudia Shughuli za uokoaji ambazo zinaendelea, ambapo hadi sasa idadi ya watu waliofariki imeelezwa kuwa imefikia watatu na waliookolewa wakiwa hai ni 17, kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum, Suleiman Kova.
Askari Jeshi wakikokota Jenereta kubwa kusogeza eneo la tukio ili kuhakikisha mwanga unapatikana kurahisisha shughuli za uokoaji hadi usiku, baada ya giza kuingia.

Monday, March 4, 2013

Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Hai Freeman Mbowe Azindua Mashina Mapya Rukwa

 Baadhi ya wafuasi wa Chadema wakiwa mbele ya jiwe la msingi mufa mfupi kabla ya mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe kulizindua mkoani rukwa
 Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Hai Mh Freeman Mbowe akizindua mmoja ya mashina mapya ya Chadema Mkoani Rukwa
 Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Hai Mh Freeman Mbowe akihutubia muda mfupi baada ya kuzindua mmoja ya mashina mapya ya Chadema Mkoani Rukwa.Picha Zote na Chadema