Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds
Media Group,Joseph Kusaga 'Joe' pichani kushoto akichanganua jambo kwa
Mkurungezi Mtendaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti,Steve Gannon mara
baada ya kutembezwa studio mpya na ya kisasa kabisa,iliyofungwa mjengoni
humo,ambayo inatarajia kuanza kutumika hivi karibuni,Steve Gannon
amefanya ziara fupi mwishoni mwa wiki na kutembelea vitengo vyote
kampuni hiyo huku akijionea namna shughuli mbalimbali zinavyofanyika
mjengoni humo.
Steve Gannon akitazama picha za
wasanii mbalimbali wa nje waliowahi kufika nchini Tanzania na kufanya
maonesho yao kadhaa ndani ya ofisi za Prime Time Promotions Ltd.
Mkurugenzi wa mambo ya utafiti na
vipindi vya Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akifafanua jambo
kwa Mkurungezi Mtendaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti,Steve Gannon
ambaye nae alikuwa akimsikiliza kwa makini.
Mkurungezi Mtendaji wa Kampuni ya
bia ya Serengeti,Steve Gannon akimuuliza jambo mtangazaji wa kipindi cha
Power Breakfast,Gerald Hando kuhusiana na mambo mbalimbali ya
kikazi,alipotembezwa kwenye studio ya ziada.
Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds
Media Group,Joseph Kusaga 'Joe' pichani kushoto akifafanua jambo kwa
Mkurungezi Mtendaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti,Steve Gannon mara
baada ya kufanya ziara fupi mwishoni mwa wiki na kutembelea vitengo
vyote kampuni hiyo huku akijionea namna shughuli mbalimbali zikifanya
mjengoni humo.
Mkurungezi Mtendaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti,Steve Gannon akizungumza jambo na baadhi ya wafanyakazi wa kitengo muhimu cha kampuni hiyo cha Masoko.
Steve Gannon akisalimiana na
Oparesheni Meneja wa Prime Time Promotions Ltd.Balozi Kindamba,mara
alipotembelea ndani ya kampuni hiyo ambayo imekuwa ikijihusisha na
matamasha mbalimbali likiwemo tamasha kubwa la Fiesta ambalo hufanyika
kila mwaka.
Steve Gannon akisalimiana na Gerald Hando
Mkurungezi Mtendaji wa Kampuni ya
bia ya Serengeti,Steve Gannon akioneshwa matoleo mbalimbali ya jariba la
burudani la KITANGOMA linachapishwa na kampuni ya Prime Time
Promotions.
Mkurungezi Mtendaji wa Kampuni ya
bia ya Serengeti,Steve Gannon akipeana mkono na Mmoja wa wafanyakazi wa
Prime Time Promotions,Godliva Nicholaus mara alipowasili ndani ya ofisi
za kampuni hiyo.
Mkurugenzi wa mambo ya Masoko na
Mauzo,Shebba Kusaga akifafanua jambo kwa Mkurungezi Mtendaji wa Kampuni
ya bia ya Serengeti,Steve Gannon.
Chief Editor wa Clouds
TV,Bwa.Kanyopa akitoa maelezo mafupi kuhusiana na ufanyaji wao kazi
ikiwemo na urushaji wa vipi kupitia Tv yao,Pichani kushoto ni Boss Joe
akisikiliza kwa makini.
Mkurungezi Mtendaji wa Kampuni ya
bia ya Serengeti,Steve Gannon alitembezwa pia ndani ya chumba maalum cha
kuandalia habari,hapa Mtangazaji wa kipindi cha Michezo Shaffih Dauda
akifafanua jambo kwa Steve Gannon.
Baada ya ziara kutembelea vitengo
mbalimbali vya kampuni hiyo,pia Steve Gannon alipata wasaa wa kukaa meza
moja na uongozi wa juu wa kampuni hiyo na kuzungumza machache,ikiwa ni
sehemu ya mchakato wa ufanisi wa kikazi kwa mwaka mpya wa 2013.
BALOZI WA NIGERIA NCHINI MAREKANI AMFANYIA DINNER YA KUMUAGA BALOZI WETU MH. MWANAID MAAJAR
Balozi wa Tanzania nchini Marekani
na Mexico Mhe. Mwanaidi Maajar (wapili toka kulia)akiingia nyumbani kwa
Balozi wa Nigeria (hayupo pichani) Potomac, Maryland, huku wakipokelewa
na afisa ubalozi wa Nigeria (wa kwanza kulia) anayesalimia ni mama Lily
Munanka ambaye ni mkuu wa utawala na fedha Ubalozi wa Tanzania nchini
Marekani akifuatiwa na mume wa Balozi, Bwn. Shariff Maajar siku ya
Jumapili January 6, 2013 siku Balozi wa Nigeria alipomfanyia chakula cha
jioni maalum kwa ajili ya kumuaga Balozi wetu ambaye anamaliza muda
wake.
Mhe. Mwanaidi Maajar akilakiwa na
Balozi wa Nigeria nchini Marekani, Mhe.Adebowale Ibidpo Adefuye siku ya
Jumapili January 6, 2013 alipomkaribisha chakula cha jioni maalum kwa
ajili ya kumuaga Balozi wa Tanzania nchini Marekani ambaye anamaliza
muda wake.
Mke wa Balozi wa Nigeria
akisalimiana na kumkaribisha Mhe. Mwanaidi Maajar huku mumewe Bwn.
Shariff Maajar akiwa amesimama kwenye ngazi akiangalia.
Balozi na mumewe Bwn. Shariff
Maajar wakisalimiana na Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV, Bwn Idd
Sandaly ambaye pia aliongozana na mkewe (wakwanza kushoto) kwenye
chakula cha jioni alichoandaliwa Balozi wetu na Balozi wa Nigeria kwa
ajili ya kumuaga siku ya Jumapili January 6, 2013 nyumbani kwake
Potomac, Maryland.
Kutoka kushoo ni Rais wa Jumuiya
ya Watanzania DMV akiwa pamoja na mkewe, Balozi wa Benin nchini Marekani
Mhe.Cyrille S. Oguin katika picha ya pamoja na Balozi wa Nigeria nchini
Marekani Mhe.Adebowale Ibidpo Adefuye.
Balozi
wa Nigeria nchini Marekani Mhe.Adebowale Ibidpo Adefuye (kulia)
akisalimiana na Mume wa Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico,
Bwn. Shariff Maajar.
Balozi
wa Nigeria nchini Marekani Mhe.Adebowale Ibidpo Adefuye akisalimiana na
kumkaribisha Balozi wa Botswana nchini Marekani Mhe. Tebelelo Seretse nyumbani kwake Potomac, Maryland siku
ya Jumapili January 6, 2013 alipomualika chakula cha jioni maalum kwa
ajili ya kumuaga Balozi wetu ambaye anamaliza muda wake.
Balozi wa Botswana nchini Marekani Mhe. Tebelelo Seretse (kushoto) akiongea jambo na Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Mwanaidi Maajar.
Kutoka kushoto ni Mkuu wa Utawala
na Fedha Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, mama Lily
Munanka, Mke wa Balozi wa Zimbabwe, Balozi wa Zimbabwe nchini Marekani,
Mhe. Dr. Machivenyika Mapuranga na Balozi wa Benin nchini Marekani Mhe.
Cyrille S. Oguin.
Wakati wa chakula.Picha na Vijimambo Blog
No comments:
Post a Comment