Tuesday, January 8, 2013

Chama cha Mapinduzi (CCM),Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Chama cha Wananchi (CUF)Vyawasilisha Maoni Yao Tume ya Mabadiliko ya Katiba


Mmoja wa Viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Ndg. Andrew Chenge akiwasilisha maoni ya chama chake kuhusu Katiba Mpya katika mkutano na Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo Januari 7, 2013 katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba akifafanua jambo kuhusu mfumo wa uchambuzi wa maoni ya wananchi kwa viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF) waliofika katika ofisi za Tume kuwasilisha maoni ya chama hicho kuhusu Katiba Mpya leo Januari 7, 2013:. Viongozi hao pia walipata fursa ya kutembelea Kitengo cha Taarifa Rasmi (Hansard) na Kitengo cha Utafiti. Kulia kwa Mwenyekiti ni Katibu wa Tume Assaa Rashid na kushoto ni Mwenyekiti wa CUF Prof. Lipumba.
  Mmoja wa Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu akiwasilisha maoni ya chama chake kuhusu Katiba Mpya katika mkutano na Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo (Jumatatu, Jan 7, 2013) katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
 Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba (kulia) wakiongozwa na Dkt. Salim Ahmed Salim wapokea maoni kuhusu Katiba Mpya kutoka kwa uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ulioongozwa na Mwenyekiti wake Ndg. Freeman Mbowe katika Ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam leo Januari 7, 2013
 Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba akiwasilisha maoni ya chama chake kuhusu Katiba Mpya mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo (Jumatatu, Jan 7, 2013) katika Ofisi za Tume jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Tume Jaji Joseph Warioba na kulia kwa Prof. Lipumba ni Katibu wa Tume Assaa Rashid.
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba katika picha ya pamoja na Viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF) wakiongozwa na Mwenyekiti wao Prof. Ibrahim Lipumba mara baada ya chama hicho kuwasilisha maoni yake kuhusu Katiba Mpya kwa Tume jijini Dar es Salaam leo Januari 7, 2013.

No comments:

Post a Comment