Sunday, December 16, 2012

WANA UDOM TUMEONDOKEWA NA RAFIKI YETU KIPENZI OTTO



     Ni masikitiko makubwa sana kwa wana UDOM kuondokewa na mwanafunzi mwenzetu aliyekua akisoma mwaka wa pili katika college ya Earth science anayejulikana kwa jina la Otto, wengi tukimfahamu kama sir Otto aliyefariki juzi jijini Dar es salaam katika hospitali ya taifa ya muhimbili alipopelekwa kupata matibabu zaidi.Taarifa juu ya chanzo cha kifo chake tutawajulisha zaidi baada ya kupata taarifa toka kwa madaktari. Taarifa zilizotufikia ni kwamba mwili wa marehemu unatarajiwa kufika leo usiku majira ya saa sita mjini Dodoma ukitokea jijini Dar es salaam, mazishi yanatarajia kufanyika kesho eneo la area C jijini dodoma. Wana dodoma wote tunaombwa kushirikiana kwa pamoja katika kumsindikiza ndugu yetu huyu katika safari yake ya mwisho hapa duniani. Sisi tulimpenda lakini mungu kampenda zaidi. bwana alitoa na bwana ametwaa

                                
                                                                          R.I.P sir Otto      

No comments:

Post a Comment