Mwanamuziki mahiri ndani ya kundi
la Quartie Latin aitwae Cindy, linaloongozwa na nyota wa muziki wa
dansi kutoka nchini DRC-Congo,Koffi Olomide akiimba jukwaani usiku huu
mbele ya umati mkubwa uliojitokeza kwa wingi (hawapo pichani),kwenye
tamasha la usiku wa Tusker Carnival ndani ya viwanja vya lidaz
Club,Kinondoni jijini Dar
Mwanamuziki Koffi Olomide
akijimwaya mwaya kwa madaha kabisa jukwaani usiku huu kwenye tamasha la
Tusker Carnival,huku akishangiliwa na umati mkubwa watu uliohudhuria
tamasha hilo.
Pichani juu na chini ni Mwanamuziki wa Kimataifa Koffi Olomide sambamba na skwadi lake la Quartie Latin
Koffi Olomide akimtambulisha
rafiki yake mkubwa jukwaani,Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Joseph
Kusaga,ambaye ndiye aliyemleta hapa nchini kwa udhamini mkubwa wa
kampuni ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake cha Tusker,ambapo
pia mwanamuziki huyo alimshukuru sana Joseph kusaga kwa ukarimu wake
Mkurugenzi wa Clouds Media
Group,akizungumza machache na kuwashukuru sana wadhamini wa onesho hilo
sambamba na wadau mbalimbali waliojitokeza kwa wingi kwenye onesho hilo
ambalo limefana kwa kiasi kikubwa.Picha zaidi BOFYA HAPA.
No comments:
Post a Comment