Mary Chizi aibuka kidedea kwenye Mashindano ya Michezo kwa Warembo wa Redd's Miss Tanzania 2012 jijini Dar
Mshiriki wa Redd's Miss Tanzania 2012,Mary Chizi ndie alieibuka kidedea leo katika mashindano ya Michezo mbali mbali iliyowashirikisha warembo wote wa Redd's Miss Tanzania 2012,ambapo yeye ameweza kuwa kinara katika michezo mitatu mfululizo ukiwemo wa kuogelea na kuwaacha wenzake wakijikongoja.Mary Chizi anaungana na wenzake wawili walioshinda mataji ya Miss Photogenic (Lucy Stephan) na Top Model (Magdalena Roy) ambao kwa pamoja wataingia moja kwa moja katika hatua ya nusu fainali ya Redd's Miss Tanzania 2012 mwaka huu.
Warembo walioingia hatua ya Tano Bora katika mashindano ya Michezo Mbali mbali wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Warembo wa tatu waliojihakikishia kuingia hatua ya nusu fainali ya Mashindano ya Redd's Miss Tanzania 2012.Kutoka kulia ni Lucy Stephan (Redd's Miss Photogenic),Mary Chizi (Redd's Miss Tanzania Sports Lady) pamoja na Magdalena Roy (Redd's Miss Tanzania Top Model).
Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino Agency ambao ndio waandaaji Mashindani ya Miss Tanzania,Hashim Lundenga akitangaza mshindi wa jumla kwenye Michezo mbali mbali.
Bw. Yasson Mashaka akitangaza washindi wa Michezo yote kabla ya kutangaza warembo walioingia hatua ya tano bora.
Warembo wa Redd's Miss Tanzania wakitoana
jasho kwenye michezo mbalimbali hii leo
Warembo wa Redds Miss Tz wakishiriki kwenye mchezo wa wavu hii leo
kwenye fukwe ya bahari ya hindi kwenye mwendelezo wa maandalizi ya
fainali ya Redds Miss Tz hapo mwezi ujao. mbio za Magunia.
Mchezo wa Soka.
Mkuu wa Itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania,Albert Makoye akitoa maelekezo wa warembo wa Redd's Miss Tanzania wakati wa kushindana kuruka umbali mrefu.
Mchezo wa kuruka.
Mpira wa Wavu.
Kuvuta kamba.
RAIS KIKWETE AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA KENYA LEO IKULU DAR ES SALAAM
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametaka wananchi wa
Kenya wapewe nafasi ya kuamua ni viongozi gani wanawataka katika Uchaguzi Mkuu
uliopangwa kufanyika Machi mwakani.
Aidha,
Rais Kikwete amesema kuwa wananchi wa Kenya wanayo haki ya msingi kabisa kuamua
hatma ya taifa lao katika Uchaguzi Mkuu huo.
Mheshimiwa
Rais aliyasema hayo leo Oktoba 21, 2012 alipokutana na kufanya mazungumzo na
ujumbe wa wabunge wa vyama mbalimbali vya siasa vya nchini Kenya uliomtembelea
Ikulu jijini Dar es salaam.
Ujumbe
huo uliongozwa na Naibu Waziri Mkuu wa Kenya na Waziri wa Fedha Mhe. Uhuru
Kenyatta ambaye pia ni Mwenyekiti wa
chama cha TNA na Waziri wa Sheria wa Kenya Mhe Eugene Wamalwa wa chama
cha New Ford Kenya. Wote wawili ni wagombea wa nafasi ya Urais katika uchaguzi
ujao.
Wengine
katika msafara huo walikuwa ni Naibu Waziri wa Afya na mbunge wa Mombasa Mhe.
Kambi Kazungu, Mbunge wa kuteuliwa wa chama cha TNA Bi Rachel Shebesh, na Mbunge wa Kajiado kwa
tiketi ya TNA Moses ole Sakuda na mbunge wa zamani Mhe Abdullahi Alli.
Rais
Kikwete aliwapongeza kwa kuamua kufanya kazi kwa pamoja licha ya kuwa
watakuwa washindani katika
kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu huo.
Mheshimiwa
Rais ameitakia heri nchi ya Kenya katika uchaguzi huo ujao, na kusisitiza
kwamba nchi hiyo ya jirani ina umuhimu katika mustakabali wa kiuchumi kwa
nchi za Afrika Mashariki.
Rais
Kikwete wakati huo akiwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) alikuwa miongoni
mwa viongozi walioshughulika sana kutafuta ufumbuzi wa ghasia na vurugu
zilizozuka kufuatia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2007 nchini Kenya.
Rais
Kikwete alikaa siku tatu nchini Kenya akitafuta usuluhishi wa vurugu hiyo ya
kisiasa nchini humo, ambayo katika mazungumzo yake leo ameyataja kama ajali
iliyolipata Taifa la Kenya, na ambayo majirani wake hawaitarajii kutokea katika
uchaguzi ujao.
Mwisho
Imetolewa na:
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS
DAR ES SALAAM,
21 Oktoba, 2012
Tigo, American Garden wa-surprise watoto katika ‘Happy Birthday’ ya Andrew Chale
Andrew Chale akiwa katika Picha ya Pamoja na Watoto ambapo walipewa zawadi mbalimbali na Kampuni ya Simu Za Mikononi ya TIGO
Hii ndio Keki Iliyokatwa na Mdau
Andrew Chale aliyesherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwake na watoto
waishio kwenye mazingira magumu
Mdau Andrew Chale akikata keki tayari kwa kugawa kwa watoto waliohudhuria katika hafla fupi hiyo
Mtoto Mashaka Juma wa kituo cha Mitindo
House, akimlisha keki kwa niaba ya watoto wenzake zaidi ya 50
waliojitokeza wakati wa sherehe ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mwandishi
wa gazeti hili Andrew Chale, jana iliyofanyika ndani ya viunga vya Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni jijini Dar es Salaam na kudhaminiwa na kampuni ya Tigo Tanzania na American Garden.
Watoto wakishangilia na kufurahia pamoja na Mdau Andrew Chale
Wenceslaus Kisarika ambae ni Marketing Manager wa K&K pamoja Cons Ltd, akifungua shampeni
KAMPUNI
ya Tigo Tanzania leo Oktoba 21, imeweza kufanya ‘surprise’ mbalimbali
kwa watoto waliojitokeza katika siku maalum ya kuzaliwa kwa mdau na
mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima na blog, Andrew Chale,
iliyofanyika ndani ya viunga vya Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni
jijini Dar es Salaam.
Katika party
hiyo maalum, Andrew Chale amesema ni ya kwanza kabisa kwa Mtanzania
kufanya hivyo kwani ilianza tokea Oktoba Mosi kwa kutembelea
vituo vya watoto waishio kwenye mazingira magumu na hatarishi na kutoa
misaada na pia kutembelea watoto mahospitalinio na kuwafariji.
Akielezea
mtandao huu, Andrew Chale anasema alimwamini Mungu muda wote ndio maana
ameweza kufika hapo na pia kutumia nafasi hiyo kwa pamoja kufurahi na
watoto hao wakiwemo wale waishio kwenye mazingira magumu.
“Leo, ni siku
muhimu sana kwangu, najiona nipo na mamilioni ya marafiki kwa kufika
kwenu kumenitia sana faraja Mungu awabariki nyote” alisema
Andrew wakati akiwashukuru watoto mbalimbali waliojitokeza kufanya nao
sherehe hiyo.
Watoto hao
wakiwemo waliotoka kwenye vituo vya kulelea watoto vikiwemo
vya Tanzania Mitindo House kilicho chini ya Mbunifu,Khadija Mwanamboka,
New Life Orphanage center cha Kigogo, watoto waishio mitahani na wale
wa majumbani walijumuika kwa pamoja na kufurahia na ‘Uncle’ wao Andrew
Chale ikiwemo kutembelea sehemu kadhaa za ndani ya jumba hilo la
kumbukumbu na kujionea mambo mbalimbali.
Furaha hiyo ya
siku maalum ya kuzaliwa kwa Andrew Chale imeweza kuongezwa utamu na
kampuni ya Mawasiliano ya mtandao wa simu nchin, Tigo Tanzania, ambayo
iliwezesha kumpatia keki na shampeni maalum pamoja na zawadi zingine
nyingi kwa watoto.
Kwa upande wake
Ofisa wa masoko wa tigo, Benny Lutaba, alipongeza kwa sherehe hiyo na
kuomba jamii kuendelea kuwaunga mkono kwa bidhaa zao hapa nchini
sambamba na kusaidia jamii kwa rika zote.
Nae Wenceslaus
Kisarika ambae ni Marketing Manager wa K&K pamoja Cons Ltd alipongeza kwa hatua ya watu kukumbuka watoto hasa
waishio kwenye mazingira hatarishi na magumu hapa nchini.
“Tumefarijika
sana kuunga kwenye siku hii muhimu, hakika jamii iiige mfano huu wa
kuwakumbuka watoto hasa wanaohitaji msaada si utoe fedha hata kuwaleta
mahala kama hapa ni moja ya kuwatimizia mahitaji yao” alisema Wence.
Aidham mbali na
tigo, American Garden kwa upande wao waliweza kuwa ‘surprise’
watoto kwa kuwapatia zawadi za bidhaa zao zinazopatikana nchini kote.
Akizungumza
na mtandao huu kwenye sherehe hiyo, Ofisa masoko wa Kingsway
International (T) ltd, American Garden, Miraji Chambuso alipongeza kwa
hatua hiyo ya kuwakumbuka watoto hao na ni moja ya kuhamasisha utalii
wa ndani.
“Watoto
wanapopata nafasi ya kufika sehemu kama hizi ni kuhasisha utalii wa
ndani na sisi tupo mstari wa mbele katika kuhakikisha watoto wanatimiza
ndoto na malengo yao” alisema Miraji.
Makamu wa Rais Dkt . Bilal kufungua Mkutano wa saba wa Kimataifa wa Wafanyabaishara wanawake jijini Dar es salaam kesho
Mwenyekiti
wa Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC) Fatma Riyami (kulia)
akiongea na waandishi wa habari (leo) jijini Dar es salam juu ya
Mkutano wa Saba wa Kimataifa wa Wanawake wafanyabiashara wa Nchi ya
Mashariki mwa Afrika unaofanyika Tanzania kwa mara ya kwanza na
unaotarajiwa kufunguliwa na Makamu wa Rais wa Tanzania Dr. Mohamed
Gharib Bilal . Kushoto ni Makamu wa Mwenyekiti wa TWCC Anna Matinde.
Mkutano huo unafunguliwa tarehe 22.10.2012 katika Hotel Kunduchi Beach.
…………………………………………………………….
Na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dar es salaam
Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt.
Mohamed Gharib Bilal anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika ufunguzi wa
Mkutano wa Saba wa Kimataifa wa Wanawake wafanyabiashara wa Nchi ya
Mashariki mwa Afrika unaonza kesho jijini Dar es salaam kwa lengo la
kuimarisha mtandao wao.
Kauli hiyo imetolewa leo na
Mwenyekiti wa Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC) Fatma Riyami
wakati akiongea na waandishi wa habari Ofisi kwake.
Amesema kuwa Mkutano huo ambao ni
wa saba(7) unafanyika nchini Tanzania kwa mara ya kwanza tangu
walipoanzisha ushirikiano huo wa wanawake wafanyabiashara kwa nchi za
Afrika Mashariki.
Mwenyekiti huyo amesema kuwa
wajumbe wa Mkutano huo wanatarajiwa kutoka katika Nchi za Kenya, Uganda,
Rwanda , Burundi, Ethiopia , Sudan Kusini na mwenyeji Tanzania.
Amesema kuwa Mkutano huo utakuwa
fursa nzuri kwa wajumbe kutoka nchi zote saba kubadilishana uzoefu
katika kazi ya kuwainua kiuchumi wakimama na kuimarisha Mtandao wa
Wafanyabiashara wanawake katika Nchi za Afrika Mashariki.
Ameongeza kuwa hatua hiyo
itasaidia kufanya soko la wafanyabiasha wanawake wa Afrika Mashariki
kuwa kubwa na hivyo kuwainua kiuchumi wakimama.
Aidha Bibi Fatma Riyami amesema
kuwa TWCC imeanzisha matawi katika Mikoa ya Kagera, Mwanza, Pwani,
Dodoma, Mbeya, Dar es salaam na Arusha ikiwa na lengo la kutaka kuwa
karibu na wafanfanyabiashara wanawake kwa nia kuimarisha Umoja wao.
Wakati huo Mwenyekiti huyo
amewasisitiza wajumbe wa Mkutano huo kufika katika Hoteli hiyo ifikapo
saa 1.30 Asubuhi , Mgeni rasmi atafungua mkutano huo saa 2.00 kamili
Matukio katika picha ziara ya Rais Kikwete Oman
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza wakti wa mkutano na Watanzania
waishio Oman uliofanyika jijini Muscat hivi karibuni.Kulia ni Waziri wa
Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe na kushoto ni
Balozi wa Tanzania nchini Oman, Bwana Ali Ahmed Saleh
Baadhi
ya Wafanyabiashara kutoka Tanzania na wenzao wa Oman wakiwa katika
picha ya pamoja na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete muda wakati wa mkutano
wa pamoja kati ya wanyabiashara wan chi hizo mbili uliofanyika katika
Hoteli ya Al Bustan Palace jijini Muscat hivi karibuni.
Baadhi
ya Wafanyabiashara kutoka Tanzania na wenzao wa Oman wakiwa katika
picha ya pamoja na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete muda wakati wa mkutano
wa pamoja kati ya wanyabiashara wanchi hizo mbili uliofanyika katika
Hoteli ya Al Bustan Palace jijini Muscat hivi karibuni.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na watanzania mbalimbali waliohudhuria katika mkutano huo
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na baadhi ya Watanzania waishio
Oman katika mkutano uliofanyika jijini Muscat wiki iliyopita
Baadhi
ya Watanzania waishio Oman wakiimsalimia kwa shauku Rais Dkt.Jakaya
Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya kuongea nao jijini Muscat wakati wa
ziara yake iliyomalizika hivi karibuni.Picha na Freddy Maro
No comments:
Post a Comment