Kiongozi wa Jumuiya ya UAMSHO Shekh
Farid Hadi Ahmed akishuka kwenye gari la Polisi kuelekea Mahakama ya
Mwanakwerekwe kwenda kusomewa mashtaka yao yanayomkabili ikiwemo
kusababisha fujo na uchochezi.
Mmoja kati ya Viongozi wa UAMSHO
Shekh Azan Khalid Hamdan (43) akishuka kwenye gari la Polisi kuelekea
Mahakamani Mwanakwerekwe kwenda kusomewa mashtaka yao.
Gari la Polisi la pili ambalo
liliwachukuwa Viongozi wa Jumuiya ya UAMSHO ambao walishitakiwa kwa
makosa ya kufanya fujo na uchochezi likiwa linasindikizwa na magari ya
Polisi kuja Mahakama ya Wilaya ya Mwanakwerekwe.
Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia
wakiwa wanaimarisha usalama katika eneo la Mahakama ya Wilaya
Mwanakwerekwe ambapo Viongozi wa Jumuiya ya UAMSHO walipelekwa kwenda
kusomewa mashitaka yao.
Gari la Polisi ambalo liliwachukuwa
Viongozi wa Jumuiya ya UAMSHO ambao walishitakiwa kwa makosa ya kufanya
fujo na uchochezi likiwa linawasili Mahakama ya Wilaya ya Mwanakwerekwe.
Baadhi ya Wananchi walioenda
Mahakamani hapo kwenda kushuhudia kesi inayowakabili Viongozi wa Jumuiya
ya UAMSHO ambao walikosa dhamana na kurudishwa Rumande.Picha na Makame
Mshenga-Maelezo Zanzibar.Wanafunzi Buguruni Viziwi na Balozi wa Airtel AY-waomba Watanzania kuchangia vifaa vya kufundishia.
Balozi wa Airtel nchini Ambwene Yessaya (AY) (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa chekechea ya shule ya msingi Buguruni Viziwi walipotembelea shule hiyo mwishoni mwa wiki hii.Airtel kwa kushirikiana na BAMVITA wanaendesha mradi maalum utakaowezesha wanafunzi hao wenye uhitaji maalum kupata vifaa vya kujifunzia.
Meneja huduma za jamii wa Airtel Hawa Bayumi akiangalia ujuzi wa wanafunzi wa shule ya Buguruni viziwa alipotembelea shule hiyo mwishoni mwa wiki hii. wakati AIRTEL na Balozi wao msanii AY walipofanya ziara maalum ya kuhamasisha jamii kuchangia wanafunzi hao wa shule ya msingi Buguruni viziwi kupata vifaa vya kujifunzia kwa kushirikiana na BAMVITA.
Mwalimu wa shule ya msingi Buguruni Viziwi akiwapa ujumbe wanafunzi wa shule hiyo baada ya kutembelewa na wafanyakazi wa Airtel, kutoka kushoto ni mwamlimu mkuu wa shule hiyo bi Winfrid Jeromia, akifuatiwa na Meneja huduma za jamii wa Airtel Hawa Bayumi na Airtel Ambassador Ambwene Yessaya (AY). Airtel kwa kushirikiana na BAMVITA wanaendesha mradi maalum utakaowezesha wanafunzi hao wenye uhitaji maalum kupata vifaa vya kujifunzia
Meneja huduma za jamii wa Airtel Hawa Bayumi akiongea na wanafunzi wa shule ya Buguruni Viziwi mwishoni mwa wiki hii wakati ambapo airtel walitembelea shule ya msingi viziwi kuhamasisha upatikanaji wa vifaa vya kufundishia pamoja na nyenzo mbalimbali kupitia mradi maalumu wa kuchangia vitabu unaoendeshwa na Airtel kwa kushirikiana na BAMVITA, kushoto ni Mwalimu wa shule hiyo bi Judith Kaneno akifuatiwa na Airtel Ambassador ajulikanae kwa jina la AY( Ambwene Yessaya) kulia ni Mwalimu mkuu bi. Winfrid Jeromia.
========== ========= ==========
Wanafunzi Buguruni Viziwi na Balozi wa Airtel AY-waomba Watanzania kuchangia vifaa vya kufundishia.
Ni moja kati ya shule zitakazofaidika na mradi wa Airtel na BAMVITA
Wanafunzi wa shule ya Buruguni viziwi wameomba watanzania na wadau mbalimbali kuchangia ili kufanikisha upatikanaji wa vifaa vya kufundishia pamoja na nyenzo mbalimbali kupitia mradi maalumu wa kuchangia vitabu unaoendeshwa na Airtel kwa kushirikiana na BAMVITA. Wanafunzi hao waliosema hayo wakati Airtel pamoja na balozi wake AY walipotembelea shuleni hapo mwisho mwa wiki hii.
Wanafunzi wa shule ya buruguni viziwi
ambao mbali na masomo ya darasani pia wanafundishwa kazi za stadi,
walionekana kufanya kazi za stadi za mikono ikiwemo kutengeneza shanga
pamoja na mazulia madogo ya miguu, wametia hamasa na kuthibithisha
kwamba wakiwezeshwa na kupatiwa nyenzo wanauwezo mkubwa sana wa kufanya
shughuli za stadi na ubunifu.
Akiongea katika ziara hiyo Meneja
huduma za jamii wa Airtel Hawa Bayumi alisema “leo tumetembelea shuleni
hapa ikiwa ni mwendelezo wa utaratibu wetu katika kubainisha mahitaji ya
ziada ambazo shule hizi zenye mahitaji maalumu zinahitaji. Shule ya
Buruguni viziwi ni moja kati ya shule zitakazofaidika Mradi huu
unaoshirikisha Airtel na BAMVITA una lengo la kusaidia kuendeleza
kiwango cha Elimu hapa nchini na kutoa nafasi kwa jamii yetu kuweza
kushiriki na kuchangi elimu ya msingi kwa watoto wenye mahitaji maalum. ‘
Naye Balozi wa Airtel AY Ambwene
Yesaya alisema “ Tunawashukuru watanzania kwa kuitikia wito na kuanza
kuchanga na tunaendelea kutoa wito kwa watanzania kuendelea kuchangia
kwa kutuma neno “Vitabu” kwenda namba 15626 na kwakufanya hivyo kila SMS
utakayotuma utakuwa umechangia shilingi 200 au kuchangi kiwango
chochote kupitia Airtel money 0788 041361 ambapo jina la fumbo ni
VITABU.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi
Buguruni Viziwi bi. Winfrid Jeromia alikuwa na haya ya
kusema”tunaishukuru sana Airtel kwa kuweza kuja na mradi kama huu wa
kuweza kuinua Elimu hapa nchini na kurahisha mazingira yetu ya
ufundishaji hapa shuleni. Tunawaomba watanzania wengine na makampuni
mengine makubwa yajitokeze kwa wingi kuweza kuchangia katika mradi huu
ili kuinua wigo wa Elimu hapa nchini.
Kampeni hii ya kuchangia vifaa kwa
shule zenye mahitaji maalumu inayoendeshwa na Airtel kwa kushirikiana
ilizinduliwa Agosti 23 2012 na itaendelea kwa muda kwa mienzi mitatu.
Kwa kuanzia shule tatu za jijini Dar es Salaam ambazo ni Uhuru
Mchanganyiko, Sinza Maalum, na Buguruni Viziwi zitafaidiaka na mradi
huu.
Kivuko cha Mto Kilombero
Kivuko cha Mv Kilombero Na. 1 kikivusha wananchi na mali zao juzi Mto
Kilombero, mkoani Morogoro kufuatia kivuko cha awali cha Mv Kilombero
Na. 2 kuleta hitilafu katika mfumo wa usukani. Picha na Juma Mtanda
Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad:'CUF itaendelea kuwaunganisha Watanzania.'
Wafuasi
na wapenzi wa CUF wakimsikiliza Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar na Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif
Sharif Hamad wakati akiwahutubia katika viwanja vya Buguruni jijini Dar
es Salaam.
Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar na Katibu
Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad akiwahutubia wafuasi ya wapenzi wa
chama hicho katika viwanja vya Buguruni jijini Dar es Salaam.
Aliyekuwa
Mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa ADC Bw. Al-Badawi akizungumza katika
mkutano wa hadhara wa CUF baada ya kuamua kurejea CUF akitokea ADC.
Kabla ya kwenda ADC na baadae kurejea CUF Al-Badawi alikuwa mwenyekiti
wa CUF Wilaya ya Temeke
Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar na Katibu
Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad akimkabidhi shati la chama hicho
kijana Joseph Christian ambaye alikuwa katibu mwenezi wa CHADEMA tawi la
Chuo Kikuu Dodoma. Joseph amekihama CHADEMA na kujiunga na CUF kwenye
mkutano wa hadhara huko Buguruni jijini Dar es Salaam.Picha na Salmin
Said-Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar
---
Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar na Katibu
Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad amesema chama
chake kitaendelea kutetea na kutekeleza sera yake ya kuwaunganisha
watanzania popote walipo bila ya ubaguzi wa aina yoyote.
Amesema
operesheni mchakamchaka hadi mwaka 2015 iliyozinduliwa na chama hicho
hivi karibuni imekuwa ni sehemu ya utekelezaji wa sera hiyo,na kwamba
tayari imeanza kuleta mafanikio katika mikoa iliyoanza kutekelezwa
ukiwemo mkoa wa Arusha.
Maalim
Seif ametoa kauli hiyo katika viwanja vya Buguruni jijini Dar es
Salaam alipokuwa akiwahutubia wafuasi na wapenzi wa chama hicho kwenye
mkutano maalum wa hadhara uliolenga kuwakaribisha wanachama wapya na
kuwapokea wanachama walioamua kurejea CUF baada ya kukihama na kuhamia
vyama vyengine.Katika
mkutano huo Maalim Seif aliwapokea na kuwapa kadi za chama hicho
wanachama kadhaa walioamua kurejea chama hicho wakitokea chama cha ADC
wakiongozwa na aliyekuwa Mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa ADC Bw.Al-Badawi.
Kabla
ya kujiunga na ADC, Bw. Al-Badawi alikuwa mwenyekiti wa CUF Wilaya ya
Temeke, na sasa ameamua kurejea CUF kwa kile alichokieleza kuwa ni
ubabaishaji ndani ya chama hicho kipya kinachohusishwa na mbunge wa
jimbo la Wawi Mhe. Hamad Rashid Mohd.
Maalim
Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar amesema
Tanzania imekuwa ikipita katika kipindi kigumu cha migogoro na uvunjifu
wa amani, mambo ambayo yanapaswa kupigwa vita ili kurejesha hali ya
amani na kuvumiliana.
Amedai
kuwa chanzo kikuu cha migogoro ya kijamii ikiwemo ya ardhi na mizozo ya
kidini inatokana na kutokuwepo kwa mikakati imara ya kuendesha nchi, na
kwamba viongozi wanapaswa kujifunza kutokana na migogoro hiyo, ili
kuweka mikakati imara ya kuendesha nchi kwa uhakika.
“Nchi haiendeshwi kwa kuigiza, bali kwa kuwa na viongozi wenye dira ya
mabadiliko kwa maendeleo ya wananchi”, alisisitiza Maalim Seif.
Amesema
kutokana na viongozi kutokuwa na dira na mikakati imara ya kuendesha
nchi, Watanzania wameshindwa kunufaika na rasilimali za nchi yao ambazo
ni nyingi na zinaweza kuwabadilisha kiuchumi.
Amefafanua
kuwa iwapo wananchi watanufaika moja kwa moja na rasilimali zao,
wataweza kuzitunza na kuzilinda ili ziwe endelevu, na kwamba kinyume
chake ni kuzihujumu rasilimali ambazo watahisi haziwanufaishi.
“Popote
pasipo na haki hakuna amani, tunataka kila Mtanzania ajihisi kuwa ana
haki sawa katika nchi hii, sio kuwa na raia wa madaraja, yaani daraja la
kwanza, la pili na latatu”,alifahamisha huku akishangaliwa na umati wa
watu waliojitokeza kwenye mkutano huo.
Katika
hatua nyengine, aliyekuwa katibu mwenezi wa Chama Cha Demokrasia na
Maendeleo CHADEMA katika tawi la Chuo Kikuu Dodoma bw. Joseph Christian
amejiengua katika chama hicho na kujiunga na CUF.
Akizungumza katika mkutano
huo bw. Joseph amesema ameamua kujiengua CHADEMA na kujiunga na CUF kwa
madai kuwa chama hicho kimekuwa kikiendeshwa kwa misingi ya undugu na
ukabila, na kuwatelekeza vijana wenye lengo la kuleta mabadiliko ya
kisiasa nchini.
Amewatahadhamisha vijana kuwa makini na sera za chama hicho na kuacha kukurupuka kuvamia sera za vyama wasivyovifahamu.Nae
Mwenyekiti wa ADC Wilaya ya Kinondoni Bw. Saburi Mtoro, ambaye pia
ameamua kukihama chama hicho na kujiunga na CUF amemuahidi Katibu Mkuu
wa CUF kuwa wanachama wote wa ADC katika Wilaya hiyo watajiunga na CUF.
MAKAMU WA RAIS DK GHARIB BILAL AKIHUTUBIA WAKATI WA UFUNGUZI WA MKUTANO WA AKINA MAMA WAJASIRIALIAMALI KUTOKA NCHI ZA UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa akina Mama Wajasiliamali kutoka Nchi za Ukanda wa Afrika, uliofanyika leo Oktoba 22, kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam, ukiwa ni mkutano wa kwanza kufanyika nchini Tanzania.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungao wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano wa akina Mama Wajasiliamali kutoka Nchi za Ukanda wa Afrika, uliofanyika leo Oktoba 22, kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam, ukiwa ni mkutano wa kwanza kufanyika nchini Tanzania. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
Ukumbi Walipuka kwa Shangwe Baada ya Rais Jakaya Kikwete Kuwasili na Kuhutubia Kwenye Kilele cha mkutano mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)Mjini Dodoma
Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika
ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma kufunga mkutano mkuu wa Umoja wa
Wanawake Tanzania (UWT)
Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiiimba na kucheza nyimbo mbalimbali katika
ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma alipowasili leo kufunga mkutano mkuu wa Umoja wa
Wanawake Tanzania (UWT)
Mwenyekiti wa UWT Sophia Simba akiongea katika
ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma baada ya kufunga mkutano mkuu wa
Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)
Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akihutubia katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma kufunga
mkutano mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)
Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na
Mwenyekiti wa UWT Sophia Simba na Katibu Mkuu Amina Makilagi katika
ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma baada ya kufunga mkutano mkuu wa
Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)
Sehemu ya wajumbe wa mkutano mkuu wa UWT wakicheza segere
Sehemu ya wajumbe wa mkutano mkuu wa UWT
Wanachama wakongwe wa UWT na CCM wakishangilia
Sehemu ya wajumbe wa mkutano mkuu wa UWT wakirushwa na Sizya Mazongela wa kundi la Segere
Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akisalimiana na wakongwe wa UWT katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini
Dodoma baada ya kufunga mkutano mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania
(UWT)
Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akisalimiana na wake wa viongozi katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini
Dodoma baada kufunga mkutano mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)
Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipozi na
wanachama wakongwe wa UWT Ikulu ndogo Dodoma katika mchaplo
aliowaandalia wajumbe wa Umoja huo baada ya kutoka katika ukumbi wa
Chuo cha Mipango mjini Dodoma kufunga mkutano mkuu wa Umoja wa Wanawake
Tanzania (UWT).Picha na IKULU
TCRA: TV ZENYE MIGONGO NA MATUMBO MAKUBWA PIA ZITAPOKEA MATANGAZO YA DIGITALI
Imeelezwa kuwa TV zote zikiwemo
zile zenye migongo, matumbo na viuno virefu zote zina uwezo sawa wa
kupokea matangazo ya digitali na Watanzania waepuke uvumi wa watu
wachache wanaodai kuwa TV za zamani hazitapokea zitafutwa mara Tanzania
itakapoingia kwenye mfumo wa Digitali.
\
Wito huo umetolewa na Naibu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano hapa nchini TCRA ambaye pia na
Mratibu wa Ofisi za Kanda Bw. Victor Nkya, wakati wa mkutano wa
Wataalamu wa Mawasiliano ya Habadi kwa njia ya digitali kutoka nchi za
SADC unaojadili umuhimu wa mfumo wa Digitali.
Bw. Nkya amesema kuwa wananchi
hawana haja ya kuwa na hofu juu ya TV walizonazo zikiwemo zenye matumdo
na migongo mikubwa kuwa hazitaweza kupokea matangazo ya televishen
katika mfumo mpya wa digitali.
Amesema kutokana na watu wengi
kutumia televishen za Analojia, ni lazima kila mmoja wetu awe na
kingamuzi na kazi ya Mamlaka ya mawasiliano ni kuwajengea wananchi
matumaini na kuepuka kudanganywa.
Kwa siku za hivi karibuni baada
ya Tanzania kuridhia mabadiliko ya mfumo wa Digitali, wananchi wamekubwa
na wasiwasi wakidhani kuwa huo ndio mwisho wa tv za zamani.
Awali akifungua Mkutano huo wa
siku tatu hapa mjini Zanzibar, Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano
Zanzibar Mh. Rashid Suleiman, amewataka wananchi kukabiliana na
changamoto mbalimbali zitakazojitokeza wakati wa mabadiliko ya kutoka
katika mfumo wa analojia na kuingia katika digitali.
Amesema ni vema wananchi wakahama
mapema kutoka katika mfumo huo wa zamani ili kuepuka usumbufu wakati
yatakapotokea mabadiliko hayo kwani hakutakuwa na muda wa nyongeza kama
Watanzania walivyozoea.
Na kuna umuhimu wa wananchi pia
kusikiliza maelekezo ya wataalamu badala ya kusikiliza propaganda za
watu wasio na ujuzi juu ya teknolojia hiyo.
”Watanzania hawana haja ya
kuogopa na badala yake wajiandae kujipatia vingamuzi na kinyume cha
hivyo watashindwa kupata matangazo ya televishen kama wanavyotarajia.”
Alisema Waziri.
Amesema kila mabadiliko yana
hasara na faida zake, lakini kwa mabadiliko ya kutoka katika mfumo wa
analojia kwenda digitali, kuna faida kubwa na moja ya faida hizo ni
kuwawezesha watu wote kupokea matangaza sawa na yenye ubora unaofanana
na kwa wakati muafaka.Mkutano huo wa siku tatu unazishirikisha nchi zote
za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC ikiwemo Angola,
Afrika ya Kusini, Malawi, Namibia, Botswana, Swazlland, Lesotho,
Msumbiji na wenyeji Tasnzania.
No comments:
Post a Comment