Friday, October 5, 2012

Mahabusu ampora SMG askari polisi na kutokomea gizani mkoani Arusha

Mahabusu ampora SMG askari polisi na kutokomea gizani mkoani Arusha

 
Mahmoud Ahmad,Arusha
…………………………
MAHABUSUmmoja ambaye hakufahamika mara moja mkazi wa jijini Arusha, ametoroka chini ya ulinzi mkali wa polisi mahakamani hapo na kutokomea kusikojulikana baada ya kufanikiwa kumnyang’anya silaha aina ya SMG mmoja wa askari polisi aliyekuwa akiwalinda wakati  akitolewa kwenye chumba cha mahabusu na kupandishwa kalandinga la polisi kurudishwa gerezani .
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo,limetokea majira ya saa 7.30 mchana katika mahakama kuu jijini Arusha ambapo tukio hilo lilizua hofu kubwa mahakamani hapo baada ya kuwalazimu baadhi ya watumishi wa mahakama hiyo kujifungia ndani ya vyumba vya mahakama wakihofia mahabusu huyo kuwafyatulia risasi.
Taarifa zimedai kwamba mahabusu huyo alikuwa wa kwanza kutoka kwenye chumba cha mahabusu na alipomkaribia askari huyo ambaye pia hajafahamika ghafla alivaa na kumpora silaha hiyo inayodaiwa kuwa na risasi 30 na kuruka uzio mrefu wa mahakama hiyo.
Mashuhuda walisema kuwa mahabusu huyo wa jinsia ya kiume alitokomea  na silaha hiyo kwenye mto sanawari uliopo pembezoni mwa mahakama hiyo, hata hivyo baadae  aliitelekeza silaha hiyo na polisi walifanikiwa kuipata .
 
‘’unajua tukio hilo limewshtua watu sana hawawatumishi wa mahakama walijifungia ndani wakihofia usalama wao hata hawa watu wanaokaahapa kusikiliza kesi za ndugu zao wote walitawanyika ‘’alisema shuhuda huyo n akuongeza kuwa ‘’si jambo la kawaida kutokea ila kuna uzembe Fulani umefanywa na polisi kwani haiwezekeni askari aporwe silaha tene smg akiwa ameishikilia ,hii ni hatari sana ‘’ Baada ya tukio hilo polisi walianza kuhaha kumsaka mahabusu hiyo na kwamba wakati wakipita eneo alilokimbilia walifanikiwa kuikuta bunduki hiyo ikiwa imetelekeza kwenye mawe ene la mtoni.Hata hivyo haikufahamika mara moja mahabusu huyo alikuwa akikabiliwa na makosa gani mahakamani hapo .
Kamanda wa polisi mkoani Arusha Liberatus Sabas amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kwamba polisi inafanya uchunguzi wa tukio hilo huku wakifanya msako mkali wa mahabusu hiyo.

No comments:

Post a Comment