Wanafunzi wa shule za sekondari za Makongo, St Mary na Mama Salma Kikwete washuhudia sarakasi za Tigo Mama Africa
Mtaalamu
wa Biashara na Masoko wa Tigo, Gaudence Mushi (kulia) akizungumza na
baadhi ya wanafunzi waliohudhuria onyesho la sarakasi la Tigo Mama
Afrika lililodhaminiwa na Tigo katika Viwanja vya New World Cinema,
Mwenge, jijini Dar es Salaam . Kushoto ni mwalimu wa Shule ya Sekondari
Makongo, John Ngowi. Wanafunzi zaidi ya 1000 kutoka shule za sekondari
za Makongo, St Mary na Mama Salma Kikwete walihudhuria.
Ofisa
Uhusiano wa Tigo, Alice Maro (kushoto) akishakana mikono na Mwalimu wa
Shule ya Sekondari Makongo, Kapteni Mstaafu, Hamisi Mfaume kabla ya
onyesho la sarakasi la Tigo Mama Afrika kuanza. Katikati ni Mtaalamu wa
Biashara na Masoko wa Tigo, Gaudence Mushi.
Baadhi ya wanafunzi wa sekondari wakipewa viburudisho kabla ya onyesho la sarakasi la Tigo Mama Africa kuanza
Wasanii wa kikundi cha sarakasi cha Mama Afrika, wakitoa burudani katika onyesho la sarakasi la Tigo Mama Afrika
Wasanii wa kikundi cha sarakasi cha Mama Afrika, wakitoa burudani katika onyesho la sarakasi la Tigo Mama Afrika
Baadhi
ya wanafunzi waliohudhuria onyesho la sarakasi la Tigo Mama Afrika
wakishangilia wakati wasanii wa kikundi hicho wakionyesha umahiri wao
katika onyesho lililodhaminiwa na Tigo katika Viwanja vya New World
Cinema, Mwenge, Dar es Salaam jana. Zaidi ya wanafunzi 1000 kutoka shule
za sekondari za Makongo, St Mary na Mama Salma Kikwete walihudhuria.(PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE)
No comments:
Post a Comment