Wednesday, September 26, 2012

NMB YAKABIDHI ZAWADI KWA WASHINDI WA BIBI BOMBA

Washindi wa Bibi Bomba wakiwa kwenye picha ya pamoja na maofisa NMB na Clouds tv baada ya makabidhiano hayo yaliyofanyika kwenye ofisi za Clouds Media.
Mshindi wa tatu wa kipindi kilichokuwa kinaitwa Bibi Bomba Bi. Nasra M. Abdullar (kushoto) akipokea mfano wa hundi kutoka kwa Meneja Mawasiliano wa NMB Bi. Josephine Kulwa  akishuhudia katikati  ni Mratibu wa vipindi vya Clouds tv Bw. Wasiwasi Mwabulambo.
Mshindi wa pili wa kipindi kilichokuwa kinaitwa Bibi Bomba Bi. Anna S. Indina (kushoto) akipokea mfano wa hundi kutoka  kwa Meneja Mawasiliano wa NMB Bi. Josephine Kulwa  akishuhudia, katikati  ni Mratibu wa vipindi Clouds tv Bw. Wasiwasi Mwabulambo.
Mshindi wa kwanza wa Bibi Bomba Bi.Veronika Mpandala Matia akipokea mfano wa hundi baada ya kujishindia zawadi ya fedha taslim shilingi milioni 5. Akikabidhi mfano wa hundi ni Meneja Mawasiliano NMB Bi. Josephine Kulwa (kulia), katikati akishuhudia ni  Bw.Wasiwasi Mwabulambo, Mratibu wa vipindi Clouds tv na Babu wa Kitaa – Mtangazaji wa kipindi cha Bibi Bomba

No comments:

Post a Comment