Saturday, June 2, 2012

WINFRIDA PAULO AIBUKA MSHINDI WA MISS REDDS 2012 MKOANI MBEYA


 HAPA AKIVISHWA  ILE KOFIA YA USHINDI
 AKIWA NA FURAHA MUDA MFUPI BAADA YA KUVISHWA TAJI LA USHINDI
KUTOKA KUSHOTO NI MSHINDI WA PILI ANAITWA SABRINA ABDUL NA KULIA NI MSHINDI WA TATU ANAITWA CAREEN ELIAS .Picha na Mbeya Yetu Blog

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA KATIKA MKUTANO WA SADC LUANDA ANGOLA

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (kulia)  wakizungumza na Rais wa Zambia, Michael Santa katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi  Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC uliofanyika Juni 1, 2012, Luanda Angola. Mheshimiwa Pinda alimwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika Mkutano huo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akifurahia katika mazungumzo kati yake na Waziri Mkuu wa Kwanza wa Namibia, Hage Geigob wakati walipokutana  katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC, Luanda , Angola Juni 1, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 

Rais Dk. Shein akutana na Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais,Mikoa

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na Uongozi wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mikoa ikiwa ni utaratibu wake wa kuzungumza na kila wizara katika utekelezaji wa kazi katika Mikoa.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na Uongozi wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mikoa ikiwa ni utaratibu wake wa kuzungumza na kila wizara katika utekelezaji wa kazi katika Mikoa,(kushoto) Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamadi.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
 

No comments:

Post a Comment