Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Makamu wa Rais wa Iran, Mhe. Mohammad Reza Rahimi, wakati alipowasili Ofisini
kwake Ikulu Dar es Salaam kwa mazungumzo leo Mei 30, 2012. Makamu wa
Rais wa Iran amewasili nchini kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku
tatu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea
zawadi kutoka kwa Makamu wa Rais wa Iran, Mhe. Mohammad Reza Rahimi,
baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu
Dar es Salaam, leo Mei 30, 2012, (kulia) ni Waziri wa Kazi wa Iran,
Sheykhales Lam (kushoto) ni Mkarimaniwa Makamu wa Rais wa Iran.Makamu
wa Rais wa Iran amewasili nchini kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku
tatu.
Makamu wa Rais wa Iran, Mhe. Mohammad Reza Rahimi, akiweka saini katika kitabu cha Ofisi
ya Makamu wa Rais wa Jmahuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed
Gharib Bilal, (katikati) wakati alipofika Ofisini kwake kwa ajili ya
mazungumzo leo Me 30, 2012. Kulia ni Waziri wa Kazi wa Iran, Sheykhales Lam. Makamu wa Rais wa Iran amewasili nchini kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akiongozana na Makamu wa Rais wa Iran, Mhe. Mohammad Reza Rahimi,
wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam leo, Mei 30, 2012
kwa ajili ya mazungumzo. Makamu wa Rais wa Iran amewasili nchini kwa
ajili ya ziara ya kikazi ya siku
tatu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akiagana na Makamu wa Rais wa Iran, Mhe. Mohammad Reza Rahimi,
baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu
Dar es Salaam, leo Mei 30, 2012. Makamu wa Rais wa Iran amewasili
nchini kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal na Makamu wa Rais wa Iran, Mhe. Mohammad Reza Rahimi, wakiwa
katika mazungumzo maalum, katika ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro
Dar es Salaam leo Mei 30, 2012. Makamu wa Rais wa Iran amewasili nchini
kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu.Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Airtel yaongeza zawadi ya Tsh 143 m/-katika promosheni ya Nani Mkali
Kampuni ya simu za mkononi ya
Airtel imeongeza muda kwa wateja wake kuendelea kucheza promosheni yake
kabambe ya Nani mkali ambayo ilianza miezi mitatu iliyopita na
kuwafaidisha zaidi ya wateja 90 wa Airtel waliojishindia jumla ya
miliono 217 kwa mgawanyo wa kuanzia milioni 1 kila siku, milioni 3 kila
wiki na milioni 30 kwa washindi wa mwezi
Akiongea na waandishi wa habari leo Meneja
uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando alisema promosheni hii
imekuwa na faida kwetu Airtel wateja wetu waliokuwa wakishiriki
wameifurahia na ndio maana leo tumeamua kuongeza zawadi na muda wa
promosheni ya Nani Mkali
Hivyo promosheni yetu inaongezwa muda wa
miezi miwili huku zawadi zitakazo toka ni pesa taslim Jumla ya ya
shilingi milioni 143 katika mgawanyo wa kuanzia shilingi milioni 1 kila
siku-washindi 52, milioni 3 kila wiki –washindi 7,na milioni 30 kwa
kila mwezi itatoka kwa washindi 2.
Mkataba wa ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilometa 22.1 kutoka Wete hadi Chakechake kisiwani Pemba wasainiwa
Waziri wa Fedha Dkt William Mgimwa (kushoto)
akibadilishana hati ya mkataba wa mkopo nafuu na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Waarabu
inayojishughulisha na Maendeleo ya Uchumi ya Afrika (BADEA) Bw. Abdelaziz
Khelef (kulia)leo mjini Arusha wa mradi wa ujenzi wa barabara yenye urefu wa
kilometa 22.1 kutoka Wete hadi Chakechake kisiwani Pemba. Mradi huo utagharimu
shilingi bilioni 15.
Waziri wa Fedha Dkt William Mgimwa (kushoto) akitoa
ufafanuzi kwa waandishi wa habari jana mjini Arusha mara baada ya kubadilishana
hati ya mkataba wa mkopo nafuu na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Waarabu inayojishughulisha
na Maendeleo ya Uchumi ya Afrika (BADEA) Bw. Abdelaziz Khelef (kulia) wa mradi
wa ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilometa 22.1 kutoka Wete hadi Chakechake
kisiwani Pemba. Mradi huo utagharimu shilingi bilioni 15.
Waziri wa Fedha na Mipango Ofisi ya Rais Yusuf Omar
Mzee (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari jana mjini Arusha juu
ya umuhimu wa barabara mpya inayotarajiwa kujengwa kutoka ChakeChake hadi Wete
kisiwani Pemba mara baada ya Tanzania na Benki ya Waarabu inayojishughulisha na
Maendeleo ya Uchumi ya Afrika (BADEA) kusaini mkataba wa mkopo wa masharti
nafuu wa mradi wa ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilometa 22.1. Kulia ni
Waziri wa Miundombinu ,Mawasiliano na Uchukuzi wa Serikali ya Zanzibar Hamad Masoud
Naibu Waziri wa Fedha Saada Salum (katikakati) akibadilishana mawazo na Msemaji
wa Wizara ya Fedha Bi. Ingiahedi Mduma(kushoto) wakati wa mapumziko baada ya
mikutano mbalimabli inayoendelea mjini Arusha ya Benki ya Maendeleo ya
Afrika(AfDB). Kulia ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango ya Zanzibar Amina
Khamis Shaaban.
Rais Jakaya Kikwete Afanya Mazungunzo na Rais Allasane Ouattara wa Ivory Coast Jijini Arusha
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Allasane Ouattara wa
Ivory Coast wakitembea kwa miguu kuelekea kwenye sehemu waliyotengewa
kufanyia mazungumzo rasmi katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha leo
May 30, 2012 ambako Rais huyo wa Ivory Coast amefika kuhudhuria mkutano
wa afDB ambao unbafunguliwa rasmi kesho na Rais Kikwete katika ukumbi
wa AICC. Katika maongezi yao Rais Kikwete amesema Tanzania inaunga
mkono juhudi za Ivory Coast za kutaka kurejesha nchini humo makao makuu
ya afDB ambayo yamehamia Tunisia kutokana na vurugu zilizotokea
Abidjan baada ya uchaguzi mkuu mwaka jana.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Allasane Ouattara wa
Ivory Coast wakiangalia shamba la kahawa wakati wakielekea kwenye
sehemu waliyotengewa kufanyia mazungumzo rasmi katika hoteli ya Ngurdoto
jijini Arusha leo May 30, 2012 ambako Rais huyo wa Ivory Coast amefika
kuhudhuria mkutano wa afDB ambao unbafunguliwa rasmi kesho na Rais
Kikwete katika ukumbi wa AICC. Katika maongezi yao Rais Kikwete amesema
Tanzania inaunga mkono juhudi za Ivory Coast za kutaka kurejesha nchini
humo makao makuu ya afDB ambayo yamehamia Tunisia kutokana na vurugu
zilizotokea Abidjan baada ya uchaguzi mkuu mwaka jana.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Allasane Ouattara wa
Ivory Coast wakiwa katika mazungumzo rasmi katika hoteli ya Ngurdoto
jijini Arusha leo May 30, 2012 ambako Rais huyo wa Ivory Coast amefika
kuhudhuria mkutano wa afDB ambao unbafunguliwa rasmi kesho na Rais
Kikwete katika ukumbi wa AICC. Katika maongezi yao Rais Kikwete amesema
Tanzania inaunga mkono juhudi za Ivory Coast za kutaka kurejesha nchini
humo makao makuu ya afDB ambayo yamehamia Tunisia kutokana na vurugu
zilizotokea Abidjan baada ya uchaguzi mkuu mwaka jana.Picha na IKULU
Mbunge wa Bumbuli(CCM)January Makamba Apeleka Umeme Kata ya Mgwashi Kwa Mara ya Kwanza
Mbunge wa bumbuli(CCM)na Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia Mh
January Makamba akihutubia wananchi wake(wapiga kura)kata ya Mgwashi
Jimboni kwake Bumbuli,Kwa mara ya kwanza
Mbunge
wa bumbuli(CCM)na Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia Mh January
Makamba akilakiwa na wapiga kura wake muda mfupi baada ya kumaliza
mkutano wake kata ya mgwashi Bumbuli Mei 28,2012,
WAREMBO MISS DAR INTERCOLLEGE WAJIFUA VILIVYO LAMADA HOTEL
Washiriki wa shindano la kumtafuta Malkia wa Miss Dar Intercollege
wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mazoezi yao yanayofanyika kwenye
hoteli ya Lamada iliyoko Ilala jijini Dar es salaam jana jioni, warembo
hao kila mmoja kwa wakati wame wamejitapa kufanya vizuri katika
shindano hilo na kuibuka na ushindi.
Mwalimu wa warembo mwanaoshiriki katika shindano la Miss Dar Inter College Mrarylydia Bonoface akiwaelekeza jambo wakati wa mazoezi yao jana yanayofanyika kwenye hoteli ya Lamada Ilala jijini Dar es salaam.
Mratibu wa shindano hilo Dina Ismail na mmiliki wa blogu ya www.mamapipiro.blogspot.com akieleza jambo wakati wa mazoezi hayo, na kuwaasa warembo hao kuwa na nidhamu katika mazoezi jambo ambalo litawafanya kuzingatia mambo muhimu watakayoelekezwa na mwalimu wao.
Mwalimu wa warembo mwanaoshiriki katika shindano la Miss Dar Inter College Mrarylydia Bonoface akiwaelekeza jambo wakati wa mazoezi yao jana yanayofanyika kwenye hoteli ya Lamada Ilala jijini Dar es salaam.
Mratibu wa shindano hilo Dina Ismail na mmiliki wa blogu ya www.mamapipiro.blogspot.com akieleza jambo wakati wa mazoezi hayo, na kuwaasa warembo hao kuwa na nidhamu katika mazoezi jambo ambalo litawafanya kuzingatia mambo muhimu watakayoelekezwa na mwalimu wao.
No comments:
Post a Comment