Tuesday, May 29, 2012

Msanii wa filamu Elizabeth Michael (Lulu) akiwa amezungukwa na walinzi kwenye Mahakama Kuu Dar es Salaam jana

Msanii wa filamu Elizabeth Michael (Lulu) akiwa amezungukwa na walinzi kwenye Mahakama Kuu Dar es Salaam jana kutokana na tuhuma zinazomkabili za kuhusishwa na kifo cha msanii mwenzake Steven Kanumba. (Na Mpigapicha Wetu).
 
 
 

MKOA WA RUVUMA WAPOKEA MWENGE WA UHURU JANA

Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Severin Tossi(kushoto) akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Njombe John Mahali .Mwenge wa Uhuru umepokelewa jana mkoani Ruvuma katika kijiji cha Ngelenge wilaya ya Ludewa kabla haujaanza mbio zake mkoani Ruvuma.(Picha na Muhidin Amri Nyasa= Songea)

St.Agustin​e Bingwa wa Mashindano ya Safari Higher Learning Pool

 Meya wa Manispaa ya Iringa, Aman Mamwingi akimkabidhi Kombe nahodha wa timu ya St.Agustine, Jimmy Nicas baada ya kutwaa ubingwa wa mashindano ya Safari Higher Learning Pool Competition yaliyomalizika Mkoani Iringa mwishono mwa wiki.Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Pool(TAPA) Fred Mushi.
Wachezaji wa timu ya St.Agustine wakiwa wamembeba nahodha wa timu yao, Jimmy Nicas mara baada ya kuibuka mabingwa kwenye mashindano ya Safari Lager Higher Learning Pool Competition yaliyomalizika Mkoani Iringa mwishoni mwa wiki. 
 
CHUO cha St.Augustine cha mkoa wa Mwanza juzi kilitawazwa kuwa mabingwa wapya wa mashindano ya mchezo wa pool kwa wanafunzi wa vyuo vikuu yanayojulikana kama 'Safari Higher Learning Pool Competition 2012 baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 13-9 dhidi ya waliokuwa mabingwa watetezi chuo cha IFM kutoka mkoa wa Dar es salaam katika mchezo wa fainali wa mashindano hayo.

Fainali za mashindano hayo ambazo zilishirikisha vyuo vinane ambavyo vilikuwa mabingwa katika mikoa yao ngazi ya mikoa ya mashindano hayo na kudhaminiwa na wadhamini wakuu wa mchezo wa pool nchini,Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager,zilifanyikia kwenye ukumbi wa Iringa All Fear mkoa hapa.

St.Augustine kwa kuwa mabingwa wapya wa mashindano hayo walijinyakulia fedha taslim Sh. Mil.2.5 pamoja na kikombe kikubwa cha ubingwa huo.

IFM ambao licha ya kucheza vizuri katika fainali hizo na kujikuta wakipoteza ubingwa huo walizawadiwa fedha taslim Sh.Mil.1.5 kwa kushika nafasi ya pili, chuo cha RUCO kutoka Iringa chenyewe kiliondoka na Sh.Mil.1.3 kwa kushika nafasi ya tatu na St.John's kutoka mkoa wa Dodoma kilishika nafasi ya nne na kupewa Sh. Mil.1.

Vyuo vya MUCCOBS (Kilimanjaro), IAA (Arusha),Mzumbe (Morogoro) na TIA (Mbeya) vyenyewe vilizawadia Sh.500,000 kila chuo ikiwa ni kifuta jasho cha kushiriki fainali hizo.

Kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja (wanaume) mchezaji wa chuo cha St. John's cha Dodoma, Obiara David alitwaa ubingwa huo baada ya kumgaragaza vibaya Jackson Raphael wa  chuo cha MUCCOBS (Kilimanjaro) magoli 4-0 katika mchezo wa fainali.

Obiara kwa kutwaa ubingwa huo alijinyakulia fedha taslim Sh.300,000 na ngao wakati ambapo Jackson kwa kushika nafasi ya pili alizawadia fedha taslim Sh.200,00, Said Mohamed (RUCO) alishika nafasi ya tatu na kupewa Sh.150,000 na Patrick Peter (IFM) aliambulia Sh.100,000 kwa kushika nafasi ya nne.

Kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja (wanawake), Modesta David (IFM) alitwaa ubingwa huo na kuzawadiwa Sh. 200,000, Remmy Jackson (St.John's) alishika nafasi ya pili na kupewa Sh.150,000, Suchi Anatasia (KCMC) alishika nafasi ya tatu na kupewa Sh.100,000 na Violeth Silas (IAA) aliambulia Sh.50,000 kwa kushika nafasi ya nne.

Aliyekuwa mgeni rasmi katika fainali hizo ni Meya wa Manispaa ya Iringa, Amani Mwamwindi.
 
 

No comments:

Post a Comment