Watoto watatu ambao hawajatambuliwa majina yao wakiwa wamelala nyuma ya
Pickup kwa ajili ya kupelekwa Hospitali baada ya kujeruhiwa na nyaya za
umeme.
Majumba
Sita wafunga barabara
Watoto watatu ambao walikuwa wakitembea pembezoni mwa barabara
wameangukiwa na nyaya za umeme baada ya gari dogo aina ya Escudo kugonga
nguzo asubuhi maeneo ya Mbagala Zakheem.
Watoto hawa watatu ambao walikuwa wakitembea pembeni wamejeruhiwa
vibaya na kuunguzwa sehemu mbalimbali kwenye miili yao, ambapo wasamalia
wema waliwasaidia na kuwapakia kwenye gari kukimbizwa Hospitali.
Wakazi wa Eneo la Ukonga Majumba Sita
Wilaya ya Ilala jijini Dar es sal;aam wafunga barabara kuu ya Nyerere
katika eneo hilo la majumba sita kushinikiza kuwekwa kwa matuta katika
eneo hilo kufuatia kukuthiri kwa ajali za wakazi wa eneo hilo kugongwa
wavukapo barabara hiyo.
Tukio hilo lilitokea leo majira ya saa
za asubuhi na kudumu hadi saa nane mchana baada ya kijana mmoja
kungongwa katika eneo hilo akijaribu kuvuka barabara hiyo na kufa papo
hapo.
Wakiwa na mabango, mawe na matofali
wakazi hao waname, wanawake, wazee kwa watoto walifurika katika barabara
hiyo na kushinikiza kuja kwa mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na kuwekwa
kwa matuta.
Wananchi wakiwa wamefurika kwa wingi
barabarani na hata Jeshi la polisi lililopfika na kuwasihi waruhusu
magari kupita waligoma na huko mitaani pia walizuia boda boda (pikipiki)
kupita hadi matuta yawekwe.
Magari yakiwa yamezuiwa eneo hilo
karibu na Kambi ya Jeshi Kikosi cha Anga.
Wananchi wakiwa upande wa pili wa
barabara kutaka kujua hatma ya usalama wao.
Watu walikuwa ni wengi. Awali eneo
lingine katikati ya Njia Panda segerea na Minazi Mirefu (Banana)
wanafunzi wa shule ya Msingi Minazi Mirefu waliwahi kuandamana
barabarani hapo kushinikiza kuwekwa kwa matuta baada ya wenzao kadhaa
kugongwa na serikali ikaweka matuta hayo na hivi sasa hali ni shwari
katika eneo hilo.
Uhaba wa madawati bado ni changamoto shule za msingi Musoma
Wanafunzi wa shule ya Msingi Etaro wakiwa darasani wakimfuatilia mwalimu.wanafunzi wengi katika shule hii wanakaa chini kutokana na uhaba wa madawati. |
Wanafunzi wakiendelea na masomo yao huku wengine wakitumia magoti yao kama sehemu za kuandikia huku wakiwa wamekaa chini. |
Uhaba wa madawati katika shule
za msingi
na sekondari umeendelea kuumiza vichwa vya wapenda elimu pamoja na
wazazi kwa ujumla nchini.
Upungufu wa madawati katika
shule za
msingi umeendelea kudidimiza kiwango cha elimu nchini huku ukichangia
kuongezeka kwa utoro kwa kusababisha wanafunzi wengine kukata tamaa ya
kusoma na mazingira ya shule kwa ujumla ambayo si rafiki kwao.
Matokeo ya wanafunzi kukaa
chini
husababisha wanafunzi kuandika wakiwa wameinama na wengine hata kulala
kifudi fudi na wengine kuchuchumaa na hivyo kushindwa kuandika vizuri na
pia kuchoka mapema.Hali hii kupelekea matokeo mabaya nyakati za
mitihani hasa ya kitaifa.
Hali halisi ndiyo hii wilayani Musoma vijijini |
Wanafunzi wengine wakiyageuza madawati mabovu angalau wapate sehemu ya kukaa |
Wengine wanatumia viatu vyao kukalia, na wasio na viatu wanakaa kwenye vumbi.Picha Na Haki Elimu |
No comments:
Post a Comment