Thursday, June 28, 2012

Matukio mbali mbali hospitali ya Muhimbili leo baada ya Dkt Ulimboka Kufikishwa Muhimbili akiwa mahututi

Madaktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam wakimpakia kwenye Gari Daktari Mwenzao aliepatwa na Mkasa wa Kutekwa Nyara na watu wasiojulikana na ambao walimjeruhi vibaya sana,Dk. Steven Ulimboka aliepatwa na mkasa huo usiku wa kuamkia leo huko katika msitu wa Mabwepande,jijini Dar
Wanahabari wakihangaika kupata picha ya Dk. Steven Ulimboka alieinginzwa kwenye gari hiyo tayari kwa kupelekwa kwenye Taasisi ya Mifupa (MOI) kwa matibabu zaidi.
Madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakilisukuma gari lililokuwa limempakia Dk. Steven Ulimboka.
Madaktari na Wauguzi wa Muhimbili wakiwa wamesimama huku wakizungumzia hali iliyompata mwenzao.
Mwanahabari akitafuta taswira.
hakuna kazi iliyokuwa ikifanyika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakati Dk. Ulimboka alipofikishwa hospitalini hapo.Picha Zote Kwa Hisani ya Michuzi Blog
You might also like:

Matukio mbali mbali hospitali ya Muhimbili leo baada ya Dkt Ulimboka Kufikishwa Muhimbili akiwa mahututi

Madaktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam wakimpakia kwenye Gari Daktari Mwenzao aliepatwa na Mkasa wa Kutekwa Nyara na watu wasiojulikana na ambao walimjeruhi vibaya sana,Dk. Steven Ulimboka aliepatwa na mkasa huo usiku wa kuamkia leo huko katika msitu wa Mabwepande,jijini Dar
Wanahabari wakihangaika kupata picha ya Dk. Steven Ulimboka alieinginzwa kwenye gari hiyo tayari kwa kupelekwa kwenye Taasisi ya Mifupa (MOI) kwa matibabu zaidi.
Madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakilisukuma gari lililokuwa limempakia Dk. Steven Ulimboka.
Madaktari na Wauguzi wa Muhimbili wakiwa wamesimama huku wakizungumzia hali iliyompata mwenzao.
Mwanahabari akitafuta taswira.
hakuna kazi iliyokuwa ikifanyika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakati Dk. Ulimboka alipofikishwa hospitalini hapo.Picha Zote Kwa Hisani ya Michuzi Blog
 
 
 

KUGUNDULIKA KWA MAITI ZA WATU 43 RAIA WA ETHIOPIA NA WENGINE 82 KUPATIKANA WAKIWA HAI

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishana Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Bw, Zelothe Stephen, Kulia akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Rehema Nchimbi kuhusu Vifo vya wahamiaji Haramu Raia wa Ethiopia, Kushoto akisikiliza ni Mkuu wa polisi Wilaya ya Kongwa Bw. Davis Nyanda.

Na.Luppy Kung’alo wa Jeshi la Polisi Dodoma
 
DODOMA, JUNE 27, 2012.  Jeshi la Polisi mkoani Dodoma limewakamata wahamiaji haramu Themanini na Mbili (82) wote wanaume wenye  asili ya Ethiopia jana  majira ya 08:OOHRS asubuhi baada ya kuonekana wakitanga tanga katika vijijji vya  Chitego na Mkoka Tarafa ya ZOISA Wilayani  Kongwa mjini hapa.
 
Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma. Bw. Zelothe Stephen kuhusu vifo  vya Wahamiaji Haramu arobaini na tatu (43) vilivyotokea jana mjini humo alisema Raia hao wote wanatoka  Kanda ya Kusini nchini Ethiopia kwenye vijiji vya Kambata, Hadia na Sirite.
 
Alisema Kukamatwa watu hao walioingia nchini bila kibali kupitia mpaka wa Tanznia na Kenya wakielekea nchini Malawi kulifanikwa baada ya wananchi wema kuwaona na kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi ambapo walifika na kufanya Operesheni Maalum ya Kuwasaka na kuwakamata.
 
”Wananchi kutoka vijiji hivyo ambavyo vipo umbali wa kilometa 141 toka Dodoma mjini waliweza kuona maiti nyingi zimetupwa kando ya barabara ya Kiteto – Dodoma  na baadaye kuwaona watu wengine walio hai katika harakati za kupita Porini kuelekea kijiji cha Izava Wilayani Chamwino hivyo kuingiwa na hofu na kutoa taarifa hizo.”aliongeza Kamanda Zelothe.
 
Alisema baada ya kupata Taarifa hizo, Jeshi la  Polisi lilifika katika eneo hilo ambako walishirikiana na wananchi wa eneo hilo, hadi kufikia jioni hiyo walifanikiwa kuwakamata  raia hao wa Ethiopia wapatao 82  ambao walikuwa wakizungumza  lugha ya kiingereza cha kubabaisha.
 
 
Kamanda Zelothe Stephen alisema kwa mujibu ya maelezo ya raia hao walisema kwamba walianza safari yao takribani miezi mitano iliyopita wakitokea Ethiopia kuelekea nchini Malawi, kupitia nchini Kenya ambako walidai kuwa ndiko kituo kikubwa cha wao kukusanywa na kuanza safari ya pamoja.
 
Walipofika Arusha walitawanywa katika vikundi vidogo na kuhifadhiwa kwenye nyumba mbalimbali huku wakipewa chakula kidogo na maji na kwamba siku ambayo hawakumbuki walikusanywa usiku na kupakiwa kwenye lori moja lililofunikwa kote na kuanza safari kuelekea Malawi.” alisistiza Bw. Zelothe
 
Aidha Mkuu huyo wa Polisi Mkoani Dodoma alisema kuwa raia hao wakiwa njiani  baadhi yao walianza kuzirai na kufariki, hivyo walifanya jitihada za kupiga kelele na kumgongea dereva lakini hakuwa tayari kusimama hadi walipokuja kutelekezwa usiku wa manane kwenye eneo la tukio hilo na lori hilo kutoweka.
 
Akizungumzia Hali za maiti katika eneo zilipotupwa, alisema  maiti nyingi  zilionekana zikiwa tayari zimeanza kuharibika ambapo jumla ya  maiti (22 ) zilisafirishwa kwenda kuhifadhiwa katika Hospitali ya Serikali ya Mkoa wa Morogoro na nyingine (21) zimehifadhiwa kwenye Hospitali ya Serikali Mkoa wa  Dodoma kusubiri uchughuzi wa Daktari na taratibu.
 
Wakati huo huo Kamanda Zelothe amesema  huduma za kibinadamu zimekuwa zikitolewa kwa  raia hao wa kigeni, na  mahali waipohifadhiwa ni jirani na kituo cha Polisi Kati Mkoani Dodoma kwa ushirikiano na taasisi nyingine ikiwa ni pamoja na Idara ya Afya, Red Cross, Uhamiaji na Uongozi wa Mkoa.
 
Kamanda Zelothe Stephen aliwashukuru wananchi wa Vijiji vya Chitego na Mkoka  kwa kutekeleza zana ya Polisi Jamii na Ulinzi Shirikishi kwa kutoa taarifa za tukio hilo, aidha wito kwa wananchi wote kuendelea kutoa taarifa za matukio mbalimbali wasiyoyaelewa katika kamati za Ulinzi na Usalama katika ngazi za Kijiji, Kata, Tarafa. Wilaya na Serikali Kuu ili kuweza kudhibiti uhalifu katika maeneo yetu.
 
Mweneyikiti wa Jumuia ya Madaktari nchini Dk Stephen Ulimboka, amepigwa na kujeruhiwa vibaya na watu wasiofahamika.

Dkt Ulimboka anadaiwa kuvunjwa mbavu, miguu yote miwili, kung’olewa meno yote ya mbele na kuumizwa vibaya katika sehemu mbalimbali za mwili wake.

Tukio hilo la kikatili na kusikitisha limetokea usiku wa kuamkia leo jijini Dar es Salaam, na linadaiwa kufanywa na watu wa sio julikana ambapo kabla ya kufanya unyama huo walidaiwa kumteka na kumpiga kabla ya kumtelekeza katika eneo la msitu wa Pande Mabwepande.

DKT. ULIMBOKA ASIMULIA TUKIO
Akisumulia tukio hilo Dkt Ulimboka alisema kuwa  jana usiku alipigiwa simu na mtu aliyejitambulusha kwake kuwa anaitwa Hemed, aliyemwambia kuwa anahitaji kuongea naye, na ndipo walipopanga kuonana katika eneo la Leaders Kinondoni.

Dk Ulimboka aliyekuwa akiongea kwa tabu, aliendelea kusimulia kuwa wakati akiongea na mtu huyo anayekiri kuwa alikuwa akifahamiana naye kabla, alikuwa na wasiwasi kwani kila mara alikuwa akipokea simu na kuwasiliana na watu wengine ambao hawakuwapo eneo hilo.

Alisema baada ya muda alishangaa kuona wanaongezeka watu wengine watano wakiwa na silaha, kisha wakamwambia kuwa anahitajika kituo cha Polisi na kumvuta na kumuangusha barabarani kabla ya kumuingiza katika gari lenye rangi nyeusi na kuondoka naye.

Dkt Ulimboka alisema kuwa wakiwa njiani walimpiga, na kumfikisha katika msitu huo wa pande na kuendelea kumpiga paka alipoteza fahamu.

MADAKTARI NAO WALONGA
Akisimulia mkasa huo mmoja wa madaktari wenzie aliyefahamika kwa jina moja la Dkt Deo, alisema kuwa alipigiwa simu na mtu hasiyemfahamu na kumfahamisha tukio hilo.

Alisema alipofika katika kituo cha Polisi cha Bunju, alimkuta akiwa katika hali mbaya na ilikuwa ngumu kumtambua kwakuwa alikuwa na majeraha mengi eneo la usoni.

Aliongeza kuwa akiwa na wenzie waliamua kumchukua na kumkimbiza katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwaajili ya matibabu.

"Hali yake kwakweli ni mbaya sana, amepigwa mno na ameumizwa kwakweli tumemleta hapa hili aweze kupata matibabu, lakini mimi nilivyomkuta mara ya kwanza nilishindwa hata kumtambua kwa jinsi alivyokuwa ameumizwa"alisema Dkt Deo

Alisema kuwa alisimuliwa na Dkt Ulimboka kwamba watu hao waliomteka na kumpiga walikuwa na silaha na kwamba alishindwa kuwatambua.

Aliongeza kuwa Dkt Ulimboka alidai kuwa wakati akiwa katika halimbaya alikuwa akisikia mazungumzo yao, wakibishana juu ya kumuua wengine wakisisitiza achomwe sindano, na wengine wakitaka kumpiga risasi.

Alisema wakati mabishano yakiendelea kati yao, Dkt Ulimboka aliinuka akiwa na lengo la kukimbia lakini watu hao walipiga risasi hewani iliyomshtua na kuangua chini.

Kwa upande wake Dkt Cathbeth Mcharo ambaye ndiye aliyempokea Dkt Ulimboka Hospitalini hapo, alisema kuwa hali yake ni mbaya na kwamba wanajitahidi kumpatia huduma za haraka.

Alisema kuwa kwa hatua za awali amefanyiwa vipimo mbalimbali, hili iweze kufahamika aina ya matibabu anayotakiwa kupatiwa.

POLISI
Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Kamanda Suleiman Kova amezungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio hilo la utekaji nyara na kujeruhi lililompata kiongozi mgomo wa Madaktari Steven Ulimboka anayedaiwa kutekwa na watu watano wakati akipata kinwaji katika klabu ya Leaders Kiondoni jijini Dar es salaam.

Kamanda Kova amesema Ulimboka aliokotwa na msamaria mwema ambaye hakutaka kumtaja jina lake kiusalama na kutoharibu upelelezi kuwa msamaria mwema huyo alimuokota Ulimboka katika msitu wa Mabwepande na kutoa taarifa kituo cha polisi cha Bunju, ambapo polisi aliyekuwa zamu alichukua maelezo yake na baadae Steven Ulimboka kuletwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.

Kamanda Kova amesema jeshi la Polisi Kanda Maalum limeunda jopo maalum kwa ajili ya uchunguzi na upelelezi wa tukio hilo la utekaji nyara, kwani ni tukio la kwanza kutoke nchini, ameongeza kwamba wahusika wote watakaobainika kuhusika na tukio hilo wachukuliwa hatua za kisheria na sheria itafuata mkondo wake ili kukomesha matukio mengine kama hayo

MUHIMBILI
Wakati hayo yakitokea inadaiwa kuwa Askari Kanzu mmoja alikumbana na kipigo kikali kutoka kwa madaktari hapo Muhimbili kwa kile kilochodaiwa kutambuliwa na Dkt Ulimboka kuwa mmoja wa watu walio mjeruhi.

Pia inadaiwa kuwa Askari huyo aliingia chooni na kufanya mawasiliano na wenzake huku Madaktari hao wakimsikiliza na kutokana na alichokua akiongea chooni humo ndipo alipotoka aliambulia kichapo kikali.

Pia baadhi ya madkatari na wauguzi walikuwa wakisukuma gari alilokuwa amepanda Dkt Ulimboka huku wakiimba nyimbo za Umoja na Mshikamano Daima miongoni mwao.

Hali ya ulinzi ilikuwa kali Hospitalini hapo kwani Picha zilikuwa haziruhusiwi kupigwa.Source Father Kidevu Blog
 
 

No comments:

Post a Comment