Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe akihutubia maelfu ya wananchi Masasi mjini
Mbunge wa jimbo la Ubungo (CHADEMA) John Mnyika akipandisha bendera ya chama nje ya ofisi ya CHADEMA Kijiji cha Mkangaula
Pichani
ni Mwenyekiti Freeman Mbowe akikata utepe wa kufungua Ofisi ya CHADEMA
Kijiji cha Mkangaula. Ilikuwa ni baada ya Katibu Mkuu, Dkt. Slaa kutoa
hotuba ya ufunguzi na John Mnyika kupandisha bendera ya chama nje ya
ofisi hiyo, ikiwa ni ishara ya kupiga hatua katika mapambano ya awamu ya
pili.
Mbunge wa Ubungo(CHADEMA)John Mnyika akitoa 'somo' kwa wanakijiji wa vijiji vya Kata ya Lumesule. Mapema
Mbunge wa Ubungo(CHADEMA)John Mnyika alikaribishwa na kuzungumza na
Katibu wa Tawi wa CUF, Bi. Zaituni. Wananchi walimwelewa vyema. Kadi
zikauzwa vizuri. Akaacha uongozi wa muda wa tawi lenye wanachama wa 34.
Katika Kijiji hicho cha Lumesule,
Mwananchi mmoja kwa jina la Yasin Mohamed alihoji Ya Mbunge wa
Ubungo(CHADEMA)John Mnyika (Kulia)ilikuwaje CHADEMA wakaachia Dkt. Slaa
ashindwe urais, wakati alichaguliwa kwa kura nyingi na wananchi na wao
wanajua alishinda uchaguzi huo wa mwaka 2010.
John
Mnyika akiwa katika vijiji vya Kata za Makukwe na Mkwedu, wilayani
Newala. Kwa George Mkuchika ambako alikutana na kiashiria cha wazi
kuhusu udhaifu wa Waziri Mkuchika (Mbunge wa Newala) katika kusimamia
majukumu yake, baada ya wananchi katika Kijiji cha Tengulengu, Kata ya
Mkwedu kumlalamikia kuwa Diwani wa Kata hiyo, Juma Dadi hajawahi
kufungua ofisi yake zaidi ya mwaka mmoja sasa. Pamoja na kuwasilisha
malalamiko yao kwa barua Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Newala na
kwa Mbunge wao, Mkuchika, hakuna hatua zozote zilizochukuliwa.
Unaweza
kuona pia wanawake wakiitikia PEOPLES POWER, nao wakaipiga ya nguvu
kweli kweli kuonesha umoja na mshikamano katika Falsafa ya Nguvu ya
Umma ya CHADEMA, katika kudai uwajibikaji, kupigania haki, uhuru na
mabadiliko ya kweli ya mfumo na utawala nchini.
Sehemu ya Umati mkubwa wa wananchi kwenye mkutano huo
Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Slaa akizongwa na wananchi wa Kijiji cha Namahinga, Masasi aliokuwa akisalimiana nao.
Opresheni
Okoa Kusini katika picha, hapa ilikuwa Masasi Mjini. Waweza kuona
katika baadhi ya picha watu walivyopanga mstari kupigania kadi.Picha na Habari na Kurugenzi ya Habari- CHADEMA
Tawi la CHADEMA Washington DC Nchini Marekani Lazidi Kuvuna Wanachama Wapya
Linda Bezuidenhout (LB) furaha baada ya kuvua kamba kuvaa kwanda na kuchukua kadi kuwa mwanachama kamili wa Chama Cha Demokrasia Chadema.
Mwenyeketi
wa tawi la Tawi la Chama Cha Demokrasia CHADEMA Washington DC Mhe.
Kalley Pandukizi, pamoja na katibu wake Mhe. Libe Mwang'ombe
akimkabidhi rasmi mwanacham mkareketwa ambae ni mwana
mitindo Linda Bezuidenhout (LB) kati ya uwanachama wa chama
cha Demokrasia Chadema katika ofisi ya tawi la Tawi la
Chama Washington DC.
Mwenyeketi
wa Tawi la Chama Cha Demokrasia CHADEMA Washington DC Kalley
Pandukizi akiwa na katibu wachama hicho,Ndugu Libe Mwang'ombe alipotoa
kadi rasmi kwa Beautician maharufu na designer wa kitanzan
Linda Bezuidenhout (LB)
Viongozi wa tawi la chadema Washington DC wakipata Champagne
Mwenyeketi
wa tawi la Tawi la Chama Cha Demokrasia CHADEMA Washington DC Mhe.
Kalley pamoja na katibu wake Mhe. Libe Mwang'ombe wakipata picha ya
pamoja na Linda Bezuidenhout Atlanta, Georgia na wanachama wa tawi la
chadema Washington DC. Katika
miaka ya nyuma Linda aliwahi kusponsor matukio mbali mbali kwenye
miaka ya 1990 wengi wao wakimjua kwa Linda Express Nchini Tanzania
ambae ambaye hivisasa anajishughulisha na biashara ya nguo za kiume milanovita.com pamoja na zakike ambazo anadesign mwenyewe kwa brand name ya Linda kutoka Atlanta, Georgia Nchini Marekani.Picha na Mdau Wa Swahilivilla
MILIONI 421.8 ZAPATIKANA KUCHANGIA MPANGO WA ELIMU KATA YA KIPAWA JIJINI DAR ES SALAAM
Mbunge wa Jimbo la Segerea, Dk. Makongoro Mahanga (kulia), Meya wa
Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa (kushoto) na Mwenyeji wa harambee ya
kuchangia mpango wa elimu wa Kata ya Kipawa, Diwani wa Kata hiyo Bonah
Kaluwa, wakimuongoza Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa ambaye alikuwa
mgeni rasmi kuingia ukumbini Katika hafla iliyofanyika jana usiku ndani
ya hoteli ya Kilimanjaro (Kempiski hotel) jijini Dar es Salaam .
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye harambee hiyo
Diwani wa Kata ya Kipawa Bonah Kaluwa, akitoa neno la shukurani kabla ya kuanza kwa harambee hiyo.
Mgeni rasmi wa Hharambee hiyo akimpa mkono wa asante mwakilishi wa
kampuni ya Home Shopping Centre Bi Madiha Al Harthy (kushoto),Salma
baada ya kuchangia sh. milioni 22.
Mkurugenzi wa SONGAS Limited Bw;Christopher Ford(katikati),akimkabidhi
mfano wa hundi yenye thamani ya dolla za kimarekani 10,000, mgeni rasmi
wa harambee hiyo.kushoto meneja rasilimali Songas Bi Agatha Keenja.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Shinyanga, Hamisi Mgeja
(katikati) akipongezwa na Mgeni rasmi wa harambe hiyo baada ya
kuchangia sh. 500,000.
eya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa (kushoto), akimkabidhi mfano wa
hundi yenye thamani ya sh.milioni 10, Waziri Mkuu wa zamani, Edward
Lowassa, aliyekuwa mgeni rasmi katika harambee ya kuchangia mpango wa
elimu Kata ya Kipawa, iliyofanyika Dar es Salaam juzi. Fedha hizo
zilitolewa na Manispaa hiyo ambapo zaidi ya sh. milioni 400
zilipatikana.(PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE)
Na Dotto Mwaibale
WAZIRI Mkuu wa zamani , Edward Lowassa, ameendeleza kuwa mstari wa mbele
katika harakati zake za kuchangisha mamilioni ya fedha baada ya
kuchangisha Sh.421,850,000 kwa ajili ya kuboresha Mfuko wa Elimu Kata ya
Kipawa katika Manispaa ya Ilala Jijini Dar es Salaam.
Lowassa ambaye ni mbunge wa Monduli (CCM), aliendesha harambee hiyo juzi
katika hafla iliyofanyika Hoteli ya Kempiski Jijini Dar es Salaam
ambapo yeye mwenyewe alichangia Sh.milioni 10.
Katika harambee hiyo miongoni mwa makampuni yaliyochangia kiasi kikubwa
ni Lion Club Sh.milioni 70, Home Shipping Center Sh.milioni 22, African
Barrick Gold Dola 10,000, Songas Dola 10,000, Maersk Sea Line
ilichangia Sh.Miliono 90, na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja
alichangia milioni Sh.10.
Wengine waliochangia ni madiwani, viongozi wa Chama Cha Mapinduzi,
Chadema, taasisi za watu binafsi na mtu mmoja mmoja ambapo Radio Clauds
walitoa muda wa hewani wa kutangaza mpango huo wenye thamani ya sh.
milioni 12.
Akizungumza kabla ya kuendesha harambee ya kuchangisha, aliwataka
Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri kuendelea kuwahamasisha
wananchi kuwekeza katika kuchangia sekta ya elimu.
Lowassa alimpongea Diwani wa Kata ya Kipawa, Bonnah Kaluwa, kwa jitihada
zake alizozionyesha za kuchangia elimu na kuwataka madiwani wengine
kuiga mfano huo.
Diwani wa Kata ya Kipawa, Bonnah Kaluwa, kwaupande wake alisema shule
saba za Msingi na Sekondari zilizopo kata hiyo zinakabiliwa na matatizo
lukuki ikiwemo upungufu wa vyumba vya madarasa hali inayosababisha
wanafunzi kati ya 140 hadi 160 kusomea katika darasa moja.
“Shule za kata yangu kwa kweli zinakabiliwa na changamoto nyingi,
kwa mfano Shule ya Msingi ya Majani ya Chai ina vyumba vya madarasa nane
wakati wanafunzi waliopo ni 2,200, Shule ya Msingi ya Minazi Mirefu
madarasa yake yaliyopo ni machakavu pia hayatoshelezi,”alisema Kaluwa.
Kaluwa alisema jitihada nyingine zilizofanywa katika kutafuta pesa kwa
ajili ya kuziboresha shule hizo ambapo Machi 17 mwaka huu kuliitishwa
matembezi ya hisani yaliyoongozwa na mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
Aliongeza kuwa katika hafla hiyo kiasi cha shilingi milioni 15 kilichangwa na wadau
mbalimbali ambapo kati ya hizo Sh.Milioni 3 zilitolewa na Mke wa Rais
Mama Salma Kikwete na Clouds Media Group ambao walitoa shilingi milioni
moja na wanafunzi kadhaa wa shule za msingi na sekondari.
Mbunge wa Jimbo la Segerea Dk.Makongoro Mahanga aliwashukuru wadau
waliojitokeza kuchangia kata hiyo ambayo ipo katika jimbo lake na
kuwataka wadau wengeni kuchangia kata zingine ili kukabiliana na
matatizo hayo katika shule mbalimbali.
Baraza la Sanaa (BASATA) lawapa somo waandaaji wa Epic Bongo Star Search 2012
Na Mwandishi Wetu
BARAZA
la Sanaa la Taifa (BASATA) limeendesha semina ya siku moja kwa majaji
wa shindano la Epic Bongo Star Search 2012 kwa kuwataka kuzingatia
maadili ya kazi zao.
Akitoa somo kwa majaji hao mratibu wa matukio wa Basata Malimi Mashili aliwataka majaji hao kutambua kuwa asilimia kubwa ya washiriki wanategemea zaidi msaada wao katika kukuza vipaji.
Mashili
aliwataka majaji hao kutambua kuwa mazingira waliyotoka washiriki na
kuangalia namna ya kuwasaidia kulingana na mikoa yao kwa kuwa wapo ambao
wana vipaji lakini wanatatizwa na suala la kuyazoea mazingira.
Alisema
kuwa kwa kuwa mwaka huu EBSS itaruhusu washiriki wa miaka 16 hivyo ni
vema zaidi wakazingatia suala la sauti kulingana na umri wa mshiriki
sababu watakuwepo wenye sauti za kitoto pia.
Pia
aliwataka majaji hao kuhakikisha kuwa hawatoi aina yoyote ya upendeleo
na wala kuwa karibu zaidi na baadhi ya washiriki wa shindano hilo.
Pia alisisitiza kuwa majaji wanalo jukumu kubwa la kuwaelekeza namna ya kuimba, kuvaa, kujiheshimu na usafi wa mwili pia.
“Hiii
ni semina ya kuwekana sawa tu kwa kuwa hili shindano lipo kwa muda
mrefu na majaji mmekuwa mkifanya vema, kwa niaba ya BASATA napenda
kuchukua muda huu kuwataka muwe makini katika kuzingatia maadili haya
niliyoyasema na hata mengine pia”alisema Mashili.Naye
Mkurugenzi wa Berchmark Production inayoandaa shindano hilo Ritha
Paulsen alisema kuwa semina hiyo ni muhimu kwa majaji kwa kuwa muda mzuri wa kukumbushana mambo muhimu yahusuyo muziki.
Epiq Bongo Star Search mwaka huu inaanzia mkoani Dodoma Juni 16 katika ukumbi wa Royal Village.
Majaji wa shindano hilo waliohudhuria ni pamoja na Jaji Mkuu Ritha Paulsen, Master Jay, Salama pamoja na mratibu wa EBSS kutoka Basata Vicky Temu.
habari zaidi ingia www.elimuboratanzania. blogspot.com
No comments:
Post a Comment