Tuesday, June 5, 2012

Bongo Star Search kuanza ziara ya Kusaka vipaji mkoani Dodoma June 15

 

 

 


Na Mwandishi Wetu

ZIARA ya kusaka vijana watakaoshiriki katika shindano la Epiq Bongo Star Search mwaka huu inaanzia mkoani Dodoma Juni 15 katika Ukumbi wa Royal Village.

Akizungumzia ziara hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Benchmark Production Ritha Paulsen alisema kuwa washiriki wanatakiwa kufika katika ukumbi huo kuanzia saa 12 asubuhi.

Alisema kuwa kampuni yake inatarajia kuchukua vijana watatu hadi watano kutoka mkoa huo watakaouwakilisha mkoa huo katika fainali zitakazofanyikia Dar es salaam.

Alisema kuwa wakiwa mkoani humo wanatarajia kuona vipaji vya wasanii wa kila aina kwa kuwa EBSS inalenga kukuza vipaji vya vijana wenye uwezo wa kuimba aina zote za nyimbo.

“ Kama ambavyo imeshafahamika kuwa mwaka huu mshindi wa EBSS atapata kitita cha shilingi milioni 50 taslim hivyo ni kwamba tunawaomba wakazi wa mkoa wa Dodoma wenye vipaji kuja kwa wingi siku hiyo” alisema Ritha

Ritha ataongozana na majaji wengine ambao ni Salama na Master Jay.

RAIS KIKWETE AKUTANA NA WABUNGE WA TANZANIA KATIKA BUNGE LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI LEO JIJINI ARUSHA

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Wabunge wa Tanzania Katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya kukutana nao leo Juni 4, 2012 katika hoteli ya Ngurdoto Mountain Lodge jijini Arusha. Wabunge hao wapo Arusha tayari kwa kikao chao cha kwanza na wenzao wa Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi kesho ambapo wanatarajiwa kuchagua Spika wa Bunge hilo pamoja na kuapishwa tayari kuanza majukumu yao
 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza  na Wabunge wa Tanzania Katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya kukutana nao leo Juni 4, 2012 katika hoteli ya Ngurdoto Mountain Lodge jijini Arusha.Wabunge hao wapo Arusha tayari kwa kikao chao cha kwanza na wenzao wa Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi kesho ambapo wanatarajiwa kuchagua Spika wa Bunge hilo pamoja na kuapishwa tayari kuanza majukumu yao.PICHA NA IKULU






No comments:

Post a Comment