Wednesday, May 23, 2012

WASHIRIKI WA REDDS MISS CHANG'OMBE HAO JIANDAE KUJUA NANI ATAIBUKA KIDEDEA

Mashindano ya kuwania taji la Redds Miss Tanzania 2012 yanazidi kupamba moto kwa ngazi za vitongoji nchini kote huku vitongoji kadhaa vikiwa tayari vimesha fanya mashindano yake na vingine vikiendelea na maandalizi. 

Wakati wiki hii Mashindano hayo yakitraji kufanyika katika Vitongoji vya Kurasini Jijini Dar es Salaam tayari Wanyange wanaowania taji la Redds Miss Cha'gombe 2012  nao wapo katika mazoezi tayari kwa fainali zao zitakazo fanyika mapema mwezi ujao.
Pichani ni warembo wa Chan'gombe wakiwa katika picha ya pamoja iliyopigwa muda mfupi baada ya kumaliza mazoezi yao Mei 22,2012  katika ukumbi wa TCC Chan'gombe jijini Dar es Salaam.
Warembo hao 11 wanataraji kupanda jukwaani mapema mwezi ujao kuwania taji hilo na kuwania tiketi ya kushiriki Miss Temeke 2012. 
 
 
 

Mkazi wa Arusha ashinda piki piki bahati nasibu ya Simba

Mwandishi wetu
SHABIKI wa timu ya soka ya Simba mkoani Arusha, Abubakar Hamis ameibuka kidedea katika droo ya bahati nasibu katika kampeni ya changia simba inayoendeshwa kwa ushirikiano baina ya Kampuni ya Push Mobile Media na klabu ya Simba.
Katika bahati nasibu hiyo Hamis ambaye ni dereva taxi amejinyakulia zawadi ya pikipiki yenye thamani ya zaidi ya shilingi milion tatu.
Kwa mujibu wa Meneja Kampeni wa Simba sms, Talib Rashid shabiki huyo ni miongoni mwa mashabiki zaidi ya 40 wa klabu hiyo kongwe hapa nchini waliojishindia zawadi mbalimbali ikiwamo pesa taslimu.
"Droo kubwa itafanyika Julai na mshindi atajinyakulia bajaji," alisema Rashid na kuongeza mashabiki wanatakiwa kuandika neno Simba na kutuma kwenda 15678 kuingia katika bahati nasibu hii.
Afisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema ushindi wa shabiki huyo ni uthibitisho tosha kwamba mashabiki wao wanashinda katika bahati nasibu hiyo.
"Naomba wanachama na mashabiki wetu wajitokeze kushiriki katika bahati nasibu hii kwani ni moja ya kuichangia klabu ya Simba iweze kujiendesha na kufanya vizuri zaidi ndani na nje ya Tanzania," alisema Kamwaga.
Mshindi atazawadiwa zawadi yake ndani ya wiki mbili kuanzia sasa na kampuni ya Push Mobile Media itagharimia gharama za usafiri na kulala wakati wa kuja hapa jijini.
Alisema kuwa kwa sasa wamebakiza piki piki moja na bajaj ambazo drow yao itachezeshwa siku moja
 

January Makamba Atembelea Vodacom

Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia January Makamba akilakiwa na Mkuu wa Mahusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Joseline Kamuhanda. Makamba alitembelea makao makuu ya Vodacom katika ziara ya kujifunza shughuli za kampuni hiyo. Katikati ni Meneja wa Mahusiano ya Nje wa Vodacom Salum Mwalim.
 Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia January Makamba akizungumza na watendaji wakuu wa kampuni ya Vodacom (hawapo pichani) wakati alipotembelea makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es salaam katika ziara maalum ya kujifunza shughuli za mawasiliano nchini. Kulia na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi an Teknolojia January Makamba akikaribishwa makao makuu ya Vodacom Tanzania na Ofisa Mkuu wa Mahusiano na Mauzo kwa Wateja Wakubwa waVodacom Tanzania Mwamvita Makamba. Naibu Waziri Makamba alifanya ziara ya utambulisho Vodacom na kukutana na Uongozi wa kampuni hiyo.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia January Makamba na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza wakibadilishana uzoefu kabla ya Naibu Waziri kufanya mazungumzo na watendaji wakuu wa Vodacom Tanzania alipofanya ziara ya utambulisho makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es salaam.
 
 

Airtel Sasa Yaja na Viwango Vipya na Nafuu Vya Kupiga Simu Kwa Wateja Wake Wakiwa Zanzibar

 Meneja uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akifafanua jambo kwawaandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa viwango vipya nafuu vya mawasliano kwa wateja wa Airtel walioko zanziba (unguja na Pemba) ofa hiyo itajulikana kama Airtel Nusu shilingi na itawawezesha wateja wa Airtel kuongea kwa Gharama nafuu kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 4 usiku kwa NUSU shilingi tu kwa sekunde , na kuanzia saa 4 usiku hadi 11.59 asubuhi ni ROBO shilingi tu kwa sekunde Airtel-Airtel Pia wateja watafaidika na kupata huduma ya Internet bure usiku, wapili kushoto ni Meneja Mauzo wa Airtel kanda ya Pwani Bi Aminata Keita.
Wakwanza kushoto ni meneja Mauzo wa Airtel Zanzibar Hagai Samson na Meneja uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando wakifafanua jambo kwawaandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa viwango vipya nafuu vya mawasliano kwa wateja wa Airtel walioko zanziba (unguja na Pemba) ofa hiyo itajulikana kama Airtel Nusu shilingi na itawawezesha wateja wa Airtel kuongea kwa Gharama nafuu kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 4 usiku kwa NUSU shilingi tu kwa sekunde , na kuanzia saa 4 usiku hadi 11.59 asubuhi ni ROBO shilingi tu kwa sekunde Airtel-Airtel Pia wateja watafaidika na kupata huduma ya Internet bure usiku, wakwanza kushoto ni Meneja Mauzo wa Airtel kanda ya Pwani Bi Aminata Keita
 
 

CHINA YAFANYA MKUTANO NA NCHI ZA G-77

Bi Fauzia Mwita, kutoka Idara ya Mazingira Zanzibar, akishiriki katika majadiliano ya kuweka msimamo wa pamoja wa nchi zinazoendelea katika mkutano wa kundi la G77 na China, katika mkutano wa mabadiliko ya Tabia nchi unaoendelea mjini Bonn.
Mkurugenzi wa Mazingira Zanzibar, Bw. Sheha Mjaja akifuatilia mjadala wa kuweka msimamo wa pamoja wa nchi zinazoendelea katika mkutano wa kundi la G77 na China, kwenye Mkutano wa mabadiliko ya Tabianchi unaendelea mjini Bonn.
Bw. Ladsalus Kyaruzi (Kulia) na Mhandisi Alphonce Bikulamchi Maafisa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais wakishiriki katika majadiliano ya kuweka msimamo wa pamoja wa nchi zinazoendelea katika kundi la G77 na China.katika mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi unaoendelea mjini Bonn nchini Ujerumani. (Picha na Evelyn Mkokoi)
 

No comments:

Post a Comment