Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad Akabidhi Bendera Ya Zanzibar Watoto Wanaowawakilisha Watoto Wenzao Mayatima Wakiwa na Viongozi Wao Wanaokwenda nchini Uturuki Kuiwakilisha Zanzibar
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad
akiwakabidhi bendera ya Zanzibar, Watoto wanaowawakilisha Watoto wezao
Mayatima wakiwa na Viongozi wao wanaokwenda nchini Uturuki kuiwakilisha
Zanzibar katika Kongamano la Kimataifa la Kuadhimisha Siku ya Watoto
Yatima litakalofanyika mjini Istambul Uturuki kuanzia tarehe 28/05 hadi
03/06/2012. na kuwajumuisha Watoto wanaotoka Nchi mbalimbali Nduniani
kushiri katika Kongamano hilo.Picha na Salmin Said,-Ofisi ya Makamu wa
Kwanza wa Rais Zanzibar
Waumini wa madhehebu ya Hindu kutoka Tanzania, Kenya, Afrika Kusini, Botswana, India na Uingereza wakiandamana kwenye mitaa mbalimbali ya Jiji la Arusha
Waumini wa
madhehebu ya Hindu kutoka Tanzania, Kenya, Afrika Kusini, Botswana,
India na Uingereza wakiandamana kwenye mitaa mbalimbali ya Jiji la
Arusha kuashiria ufunguzi wa hekalu lao la Swaminarayan Mandir jana.
(Picha na Marc Nkwame).
UBINGWA WA SIMBA KUSHEREHEKEWA DAR LIVE MEI 27
Kombe la Ubigwa wa Simba ambalo wapenzi watapata nafasi ya kupiga nalo picha siku ya sherehe hizo ndani ya Dar Live.
Kamwaga akiwa na kombe la ubingwa.
Nahodha wa Simba, Juma Kaseja, akielezea sherehe hiyo.
Mpiga picha wa Global Publishers, Issa Mnally (kushoto) akiwa amebeba kombe hilo na mmoja wa wazee wa Simba, Juma Issa Matali.
Mratibu wa Burudani wa Ukumbi wa Dar Live, Juma Mbizo (kushoto) akiongea na waandishi juu ya sherehe hizo.
Ezekiel Kamwaga (kulia) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani).
Juma Kaseja akiwa na makombe mbalimbali ambayo Simba wameyatwaa miaka ya nyuma na sasa.
Waandishi wa habari wakiwa kazini katika hafla hiyo.
----
KLABU
ya soka ya Simba ya jijini Dar es Salaam imepanga kufanya sherehe kubwa
ya kutwaa ubingwa wa soka wa Ligi Kuu ya Vodacom katika Ukumbi wa Taifa
wa Burudani wa Dar Live siku ya Mei 27, Jumapili, wiki hii.
Akiongea
na waandishi wa habari leo mchana, Ofisa Habari wa klabu hiyo, Ezekiel
Kamwaga, alisema kuwa wameamua kufanya sherehe hizo ndani ya ukumbi huo
kutokana na ubora wake.
Aidha
Kamwaga alisema kuwa siku hiyo pia watawatambulisha wachezaji wapya
waliosajiliwa kwa msimu ujao wa ligi na kuwataka wapenzi wa Simba na
wananchi wengine kujitokeza kwa wingi siku hiyo.
No comments:
Post a Comment