Saturday, May 26, 2012

 

 

 

 

 

TAIFA KATIKA TASWIRA:MSHITAKIWA(John Mnyika) na MSHITAKI(Hawa Nghumbi) WAKIBADILISHANA MAWAZO MAHAKAMANI

Mbunge wa Ubungo kwa tiketi ya Chadema, John Mnyika(Kushoto) akiwa na aliyekuwa mgombea wa ubunge kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi Mkuu 2010,Hawa Nghumbi, wakati wakisubiri hukumu, katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, kuhusu kesi  ya kupiga matokeo yaliyompa ushindi Mnyika iliyofunguliwa na Hawa Nghumbi kwenye mahakama hiyo.
 
 
 

Mwanamke Mkazi wa Rufiji Ajeruhiwa Mguu Alipokua Akipambana na Mamba

Mwanamke Mkazi wa Rufiji, Khadija Boma (40), kifanyiwa tiba na Muuguzi Geraidina Amani juzi katika wodi 2 ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), Dar es Salaam, baada ya kujeruhiwa mguu alipokuwa akipambana na Mamba katika Mto Kipoka juzi, Rufiji. Mama huyo ambaye amekatwa mguu wa kulia aliong'atwa na Mamba, kabla ya kuokolewa na wananchi, alipambana naye huku akiwa na mtoto mgongoni.Picha na Khamis Mussa
 
 
 

 

TANZANIA BEGA KWA BEGA NA UNDP KUJENGA AFRIKA YENYE UHAKIKA WA CHAKULA.

 Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa UNDP nchini Tanzania Dk. Alberic Kacou akizungumza kwa niaba ya UNDP kuhusiana na kuzinduliwa kwa Ripoti ya Maendeleo ya Afrika 2012 ambapo amesema huu sasa ni wakati kwa nchi za Afrika haswa zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara kujenga mazingira ya kuelekea mustakabali wenye uhakika wa chakula.
 Mshauri wa Uchumi UNDP Bw.Amarakoon Bandara akifanya 'presentation' ya Ripoti hiyo. Kushoto ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dk. Alberic Kacou, Naibu Waziri wa Fedha Mh. Janet Mbene na Mkurugenzi wa UNDP Tanzania Bw. Phillipe Poinsot.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Fedha Mh. Janet Mbene na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Dk. Alberic Kacou (kulia) wakifuatilia maoni ya Uchambuzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Afrika 2012 kutoka kwa Maprofesa wa Vyuo vikuu nchini.
 Dr. John Mduma akifanya majumuisho ya nini kifanyike kukabiliana matatizo ya uhaba wa chakula yanayolikabili bara la Afrika na Afrika Mashariki.
Profesa Joyce Kinabo wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine akieleza uhifadhi wa Chakula kwa ajili ya matumizi ya baadae
Baadhi ya Maofisa wa Umoja wa Mataifa na Wadau wa Serikali wakichangia maoni yao kuhusiana na Ripoti hiyo.
 Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Fedha Mh. Janet Membe (MB) akisoma hotuba wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Afrika 2012. Kushoto ni Mkurugenzi wa UNDP Tanzania Bw. Phillipe Poinsot.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Fedha Mh. Janet Mbene (MB) akikata utepe kuzindua rasmi Ripoti ya Maendeleo ya Afrika 2012. Kushoto ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dk. Alberic Kacou.
 "Sasa imezinduliwa rasmi" Mgeni rasmi Mh. Janet Mbene na Dk. Alberic Kacou wakionyesha Ripoti hiyo kwa wageni waalikwa na waandishi wa habari.
Baadhi ya Wageni waalikwa wakipitia Ripoti ya Maendeleo ya Afrika 2012 kuelekea kwenye Mustakabali wenye uhakika wa Chakula kwa nchi za Afrika iliyozinduliwa rasmi leo jijini Dar es Salaam

Bara la Afrika ikiwemo Tanzania limeshakumbwa na matukio kadhaa ya kukabiliwa na uhaba wa chakula, uliokwenda sambamba na matukio ya watu wengi kupoteza maisha haswa Kusini mwa jangwa la Sahara na Ukanda wa Sahel eneo la Afrika Magharibi.

Hali hiyo imekuwa moja ya changamoto kubwa inazozikabili serikali za mataifa hayo ambapo yanapambana ili kuitatua ili kila mwananchi barani Afrika aweze kufurahia kukua kwa uchumi.

Akitoa hotuba wakati akizindua rasmi Ripoti ya Maendeleo ya Afrika 2012 leo jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Fedha Mh. Janet Membe (MB) amesema kwa muda mrefu sura ya eneo la nchi za Afrika zilizo Kusini mwa jangwa la Sahara imekuwa ni ya njaa ya kukithiri, ambapo zaidi ya mtu mmoja katika kila waafrika wane wana tatizo la upungufu wa lishe.

Amesema Ripoti hiyo inaonyesha kuwa pamoja na ukweli kwamba baadhi ya nchi zinazokuwa kwa kasi kiuchumi katika kipindi cha miaka kumi ziko Afrika, lakini bado hali ya maisha ya waafrika ni duni.

Awali Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa UNDP nchini Tanzania Dk. Alberic Kacou alisema bara la Afrika limejaliwa kuwa na ardhi yenye rutuba, maji ya kutosha na hali nzuri ya hewa kwa kukuzia mazao, lakini swali la kujiuliza ni kwanini bado kuna uhaba wa chakula.

Hata hivyo Dk. Kacou ametoa matumaini kuwa bara la Afrika bado lina uwezo wa kujijengea mazingira ya kuwa na akiba ya kutosha ya chakula kwa kipindi kijacho.

Ripoti hii ya Kwanza ya Maendeleo ya Afrika inasema kwamba ongezeko endelevu katika uzalishaji kwenye kilimo kunalinda haki ya chakula na uwezo wa watu kupata chakula.
 

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHIRIKI CHAKULA CHA JIONI KATIKA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA MJINI BOTSWANA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Mama Asha Bilal, wakiwasili  kwenye ukumbi wa tafrija ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na Rais wa Botswana Lt. General Seretse Khama, kwa viongozi wakuu wa Nchi za Afrika waliohudhuria mkutano wa siku mbili kuhusu maendeleo endelevu ya Bara la Afrika Nchini Gaborone Botswana, jana. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Asha Bilal, wakiwa kwenye tafrija iliyoandaliwa na Rais wa Botswana Lt. General Seretse Khama, kwa ajili ya viongozi wakuu wa Nchi za Afrika waliohudhuria mkutano kuhusu maendeleo endelevu kwa Bara la Afrika jana jioni.
 

Wasanii wa kikundi cha ngoma za utamaduni cha nchini Botswana wakitumbuiza kwenye hafla ya chkula cha jioni iliyoandaliwa maalum kwa wakuu wa nchi za Afrika waliohudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika kuhusu maendeleo endelevu ya Bara la Afrikamjini Gaborone Botswana.

RAIS KIKWETE APOKEA UJUMBE MAALUM KUTOKA KWA RAIS ROBERT MUGABE WA ZIMBABWE

 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akipokea ujumbe maalum kutoka kwa Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe uliowasilishwa na Waziri wa nchi ofisi ya Rais Bwana, Sidney Sekeremayi, Ikulu ndogo mjini Dodoma leo asubuhi.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Bwana Sidney Sekeremayi, ambaye ni mjumbe maalumu wa Rais Robert Mugabe Ikulu mjini Dodoma leo asubuhi. Picha na Freddy Maro
 
 
 
 
 
 

No comments:

Post a Comment