WANAFUNZI UDOM WAANZA KUCHEKA MARA BAADA YA MAJINA YA MKOPO KUTOKA
Wanafunzi
wa UDOM wakiwa Makini kuangalia majina yao kwaajili ya kuanza zoezi la
kusaini na kupewa pesa zao za kujikimu baada ya msoto wa zaidi ya wiki
tatu huku hali ikiwa mbaya chuoni hapa.Wanafunzi hao wameonekana kuwa na
furaha na matumaini ya kupata pesa zao kutokana na kukaa zaidi ya wiki
tatu bila kupata pesa zao na kupelekea wanafunzi hao kuwa na maisha
ma
gumu.
Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal (kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Chuo kipya cha Jeshi la Ulinzi la Wananchi (NDC), Meja Jenerali Charles Makakala
Makamu wa
Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal (kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu
wa Chuo kipya cha Jeshi la Ulinzi la Wananchi (NDC), Meja Jenerali
Charles Makakala, baada ya kufungua rasmi mkutano wa siku nne wa
kubadilishana uzoefu baina ya Serikali za Tanzania na China kuhusu
mafunzo ya ulinzi katika chuo hicho kilichopo Kunduchi, Dar es Salaam,
jana. (Picha na Muhidin Sufiani).
Bodaboda zapigwa marufu katikati ya Jiji Dar es Salaam
Gari ya Mamlaka ya Udhibiti wa nchi Kavu na Majini (SUMATRA) zikiwa
zimepakia Pikipiki zilizokamatwa jijini Dar es Salaam zikitumika kufanya
biashara ya kubeba abiria bila Leseni.Picha Kwa Hisani ya Amani Tanzania Blogu
KAMATI YA MISS TANZANIA YATEMBELEA MAZOEZI YA MISS KURASINI JIONI HII
Warembo
wanaoshiriki katika shindano la Miss Kurasini wakimsikiliza Mkurugenzi
wa kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundega wakati wa mazoezi ya shindano
la Miss Kurasini kwenye ukumbi wa Equator Grill leo jioni.
Mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundega akiongea na warembo
wanaoshiriki katika shindano la Miss Kurasini hawapo pichani ,wakati wa
mazoezi yao yanayofanyika kwenye ukumbi wa Equator Grill Mtoni kwa
Azizi Ali jijini Dar es salaam, Shindano la kumsaka malkia wa kitongoji
hicho linatarajiwa kufanyika siku yajumamosi katika ukumbi huohuo.
No comments:
Post a Comment