Taswira Za Mkutano Wa CHADEMA Wilayani Same,Wazidi Kuvuna Wanachama Wapya Kutoka CCM na Katibu Mkuu wa Chama Cha TLP Same Ajiunga na Chadema
James Ole Millya akihutubia
Katibu
Mkuu wa TLP Same, Heriel Msolo(kulia) akirudisha kadi jana Mbele ya
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana BAVICHA, Ngd Jhon Heche(wa pili
kushoto)na Aliekuwa mbunge wa Arusha Mjini(CHADEMA), Godbless
Lema(Kushoto)
Vijana wakigombea ofa ya kadi 10 za Millya
James Ole Millya akisalimiana na mwanachama wa CCM aliahamia CHADEMA Same jana
Aliekuwa mbunge wa Arusha Mjini(CHADEMA), Godbless Lema akiwasili Same
Wananchi wa Same wakigombea foleni ya kupatiwa kadi za CHADEMA jana
--
Habari na Seria Tuma
CHADEMA
wanaziara ya kichama Wilayani Same kwa siku nne,kuanzia jana hadi
jumatatu chini ya Mwenyekiti wa Baraza la Vijana BAVICHA, Ngd John
Heche.
Wana
mikutano maeneo tofauti ya Wilaya katika kuimarisha chama hicho.Mkutano
wa jana ulifanyikia viwanja vya Kwasakwasa Mjini Same kuanzia saa 9
hadi saa 12 jioni
Viongozi
waliohudhuria ni pamoja na aliekuwa mbunge wa Arusha Mjini, Godbless
Lema, Mwenyekiti Bavicha, John Heche, Mweyekiti CHADEMA Kilimanjaro,
Augustino Matemu na kiongozi wa vijana Babati, Wilson Mattaka.
Wengine
ni James Ole Millya aliekuwa Mwenyekiti UVCCM Arusha, aliekuwa Mjumbe
wa NEC CCM kutoka Arusha, Ndg Ally Bananga na aliekuwa Diwani wa
Sombetion (CCM). WOte hawa walihamia CHADEMA mapema mwezi huu
Katika
mkutano huo kadi nyingi sana zilitolewa na kuasiniwa na John
Heche..tena zikigombewa kununua. Lema litoa ofa ya kadi 10 kwa kina
mama na Millya nae akatoa ofa ya kuwalipia vijana kumi..
Aliekuwa
Katibu Mkuu wa TLP Same, Ndg Heriel Msolo alirudisha kadi ya TLP na
kupewa kadi ya CHADEMA na Mwenyekiti wa BAVICHA, John Heche
Lema
aliwataka watanzania kutokubali kugwanywa na wanasiasa kwa misingi ya
udini na ukabila au ukanda na kueleza kwamba CHADEMA haipiganii
maslahi ya kundi lolote katika hayo. Akasema hata yeye
hapiganiimaslahi yake binafsi bali ya watanzania.
John
Heche aliwataka watanzania kujitokeza kutoa maoni yao kwa tume ya
Katiba na kuelekeza kuwa wakatae au wazifanyie mabadiliko makubwa
nafasi za uDC au uRC na nyinginezo za kuteuliwa na mtu mmoja. Akadai
pia madaraka ya rais ni makubwa na mamabo mengi yameachwa kwa mtu
mmoja. hali inayohitaji marekebisho ili kuwe na uwajibikaji wa pamoja..
Beatrice; Mtanzania aliyeshinda Medali ya Shaba ya Upishi Dernmark katika masomo
Beatrice Stefano Mpangala, 23, mtanzania aliyekuwa
akisomea masomo ya Upishi katika chuo cha Elimu ya Juu cha katika
Aabenraa nchini Denmark amefaulu vyema masomo yake na
kutunukiwa Medali ya Shaba
Beatrice ambaye ni Binti wa
Sophia Mpangala wa Kibaha Mail Moja mkoani Pwani.
Beatrice ni chef mwanafunzi katika
Hoteli ya Vojens
ya nchini humo na alimaliza mazoezi yake kwa vitendo Hotelini hapo na
kutunukiwa Medali hiyo kwa kufanya vyema katika masomo yake.
“ Kwa hiyo mimi niko tayari kwa changamoto mpya nitakazo kabiliana nazo
katika miji mikubwa”, anasema Beatrice, ambaye ubunifu
wake katika mapichi umempa tuzo hiyo.
Nae Niels Laursen, ambaye ni Ofisa katika katika Hoteli Vojens alikofanya mafunzo hayo anasema
amejisikia fahari sana kwa mtanzania huyo mwenye vipaji lukuki vya upishi na
anapasha kuwa ni mara ya kwanza kwa mwanafunzi aliyepita hapo kufanya vyema na
kutwaa medali ya Shaba.
Beatrice akiwa na Niels Laursen
Beatrice Stefano Mpangala, 23 år, bestod
svendeprøven som kok på Fagskolen i Aabenraa. Beatrice fik
bronzemedalje. Beatrice er kokkeelev på Hotel Vojens. Beatrice
afslutter lærlingetiden den 30. november på Hotel Vojens.
- Så er jeg klar til nye udfordringer gerne i en større by, siger Beatrice, der går ind for kreativ madlavning.
Niels Laursen, vært på Hotel Vojens er naturligvis stolt at sin dygtige kokkeelev og fortæller at det er første gang, at en af hans elever er blevet belønnet med en bronzemedalje.GONGA HAPA kusoma zaidi BITE
Airtel Yatoa Msaada wa Madawati na Mipira kwa shule za Msingi za Maarifa, Mwangaza na JICA zilizopo Gongolamboto Jijini Dar
Mchezaji
wa zamani wa Klabu ya Manchester United ya Uingereza Quinton Fortune,
akikabidhi moja ya madawati yaliyotolewa na Kampuni ya simu za mkononi
ya Airtel kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Maarifa Mareitha
Mulyalya huku Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(Elimu), Mh Kassim Majaliwa akitazama. Kampuni ya Airtel Tanzania ilitoa
mipira 30, jesi seti tatu na madawati 40 kwa shule za msingi za
Maarifa, JICA na Mwangaza zote za Gongo La Mboto, Dar es Salaam.
Mchezaji
wa zamani wa Manchester United ya Uingereza Quinton Fortunewa pili
kulia, akionyesha waandishi wa habari (hawako pichani) baadhi ya vifaa
vya michezo vitakavyotumika kwenye michuano ya soka ya kimataifa kwa
vijana wenye umri chini ya miaka 17 ya Airtel Rising Stars jana kwenye
Hoteli ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam. Kati ni Waziri wa Mawasiliano,
Sayansi na Technologia Mh. Professa Makame Mbarawa, wa kwanza kulia ni
Mkurugenzi Mashindano wa TFF Sandy Kawembe, Mkurugenzi Mtendaji wa
Airtel Tanzania Sam Elangallor na Mkurugenzi Bidhaa Airtel Afrika Obina
Justine.
Mchezaji
wa zamani wa Klabu ya Manchester United ya Uingereza Quinton Fortune,
akipiga mpira kuashiria uzinduzi rasmi wa michuano ya vijana wenye umri
chini ya miaka 17 ya Airtel Rising Stars. Uzinduzi huo ulifanyika jana,
Mei 10, kwenye Hoteli ya Sea Clif, jijini Dar es Salaam.
Msanii
wa kizazi kipya Ambwene Yesaya maarufu kama AY, akiwatumbuiza wanafunzi
wa Shule ya Msingi ya Maarifa iliyopo Gongo La Mboto nje kidogo Jijini
Dar es Salaam wakati Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel ilipotoa
msaada wa madawati 30, mipira ya miguu 40 na jezi seti tatu, Alhamisi
Mei 10, 2012 ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri kwenye Ofisi ya
Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mtaa (Elimu) Mh. Kassim
Majaliwa. Shule zingine zilizofaindika na msaada ni Maarifa, JICA na
Mwangaza zote za Gongo La Mboto, Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment