TANZANIA YAWA TISHIO INDABA
Naibu Waziri wa Utalii wa Afrika Kusini Bibi Tokozile Xasa (watatu
kushoto) pamoja na Kurugenzi Mwendeshaji Biashara na viwanda wa Afrika
Kusini Bibi Elizabeth Thabethe (wa kwanza kushoto) katika picha
ya pamoja na baadhi ya waoneshaji kutoka Tanzania wakiongozwa na Mkurugenzi
Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Dk. Aloyce Nzuki (wan ne kushoto)
alipotembelea Banda la Tanzania katika maonesho ya INDABA mjini Durban
Afrika Kusini.
Na: Geofrey Tengeneza, Durban.
Banda la Tanzania katika maonyesho ya Utalii ya Kimataifa ya INDABA
yanayoendelea jijini Durban Afrika Kusini limeendelea kuvutia viongozi
na watu wa kada mbalimbali kutoka ndani na nje ya Afrika Kusini wanaotembelea
maonyesho hayo. Miongoni mwa waliotembelea banda hilo shindwa
kuzuia hisia zao hususan kwa maelezo na vielelezo vinavyoonesha uzuri
na upekee wa vivutio vya utalii vya Tanzania na shughuli za utalii
zinavyoendeshwa nchini ni Naibu Waziri wa Utalii wa Afrika Kusini Bibi
Tokozile Xasa na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Viwanda na Biashara la Afrika
Kusini Bibi Elizabeth Thabethe ambao kwa pamoja walitembelea Banda
la Tanzania na kujionea vielelezo mbalimbali sambamba na kupata maelezo
yaliyowafurahisha sana kuhusu utalii wa Tanzania kwa ujumla.
Akizungumza na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Dk
Aloyce Nzuki na waoneshaji wa Tanzania kwa ujumla Naibu huyo waziri
alifurahishwa na kuvutiwa na jinsi Tanzania kupitia Bodi ya Utalii ilivyojipanga
katika kuitangaza Tanzania duniani na jinsi ambavyo Tanzania imekuwa
ni mshiriki mzuri wa maonesho ya INDABA na kukiri kuwa Tanzania imekuwa
ikitoa changamoto kubwa kwa nchi nyingine wanachama wa SADC katika sekta
ya Utalii. “Tanzania ni nchi tishio katika sekta ya utalii miongoni
mwa nchi za SADC, ni nchi inayonivutia sana “ alisema Bibi Tokozile
Xasa
Jumla ya makampuni 49 kutoka sekta binafsi na taasisi sita za serikali
zinashiriki katika maonesho hayo ambayo ni makubwa kuliko yote barani
Afrika. Maonesho haya hufanyika kila mwaka jijini Durban Afrika Kusini.
Katika maonesho kama haya mwaka jana Banda laTanzania lilitunukiwa tuzo
ya kuwa Banda Bora kuliko yote katika maonesho hayo miongoni mwa nchi
za SADC.
MKUTANO WA KIMATAIFA WA MABADILIKO YA TABIANCHI WAFANYIKA UJERUMANI
Bi.
Christiana Figeres, Executive Secretary wa United Nations Framework
Convention on Climate Change (UNFCCC) akifungua mkutano wa kimataifa wa
sayansi na taaluma wa mabadiliko ya tabia nchi, Mjini Bonn Ujerumani.
Pichani
Kulia, Bw Richard Muyungi Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mazingira Ya
Ofisi wa Makamu wa Rais, ambae Pia ni mwenyekiti wa Dunia wa kamati ya
sayansi na Taaluma ya Mabadiliko ya Tabia Nchi, pamoja na washiriki
wengine katika ufunguzi wa mkutano wa kimataifa wa mabadiliko ya Tabia
nchi unaoendela mjini Bonn Ujerumani
Mbele
Kulia, Bwana Alfonce Bikulamchi, Afisa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu
wa Rais akifuatilia kwa umakini ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa
Sayansi na Taaluma wa masuala ya mabadiliko ya Tabia Nchi unaondelea
Mjini Bonn Ujerumani. Picha na Evelyn Mkokoi, Bonn
MAMA SALMA AZINDUA 'OKOA MAISHA YA MAMA NA MTOTO'
Jukwaa la Vyombo vya Habari Afrika lilivyorindima Uturuki
Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Willy Edward akiwasilisha mada
katika mkutano wa Jukwaa la Vyombo vya Habari Afrika na Uturuki kuhusu
'Vyombo vya Habari kama kichocheo cha ushindi wa vita dhidi ya migogoro
na ugaidi' mjini Ankara, Uturuki wiki iliyopita. Mkutano huo
ulioandaliwa na ofisi ya Waziri Mkuu, ulishirikisha wawakilishi wa
vyombo vya habari na wadau wengine kutoka nchi 54 za Afrika.
Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Willy Edward (kushoto) akipokea
tuzo maalumu kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Jamhuri ya
Uturuki (Idara ya Habari na Maelezo), Murat Karakaya iliyotolewa kwa
niaba ya Naibu Waziri Mkuu Uturuki, Bulent Arinc aliyemwakilisha Waziri
Mkuu wa nchi hiyo, Recep Tayyip Erdogan, baada ya kuwasilisha mada
katika mkutano wa Jukwaa la Vyombo vya Habari Afrika na Uturuki kuhusu
'Vyombo vya Habari kama kichocheo cha ushindi wa vita dhidi ya migogoro
na ugaidi' mjini Ankara, Uturuki wiki iliyopita. Mkutano huo
ulioandaliwa na ofisi ya Waziri Mkuu, ulishirikisha wawakilishi wa
vyombo vya habari na wadau wengine kutoka nchi 54 za Afrika.
Naibu Waziri Mkuu Uturuki, Bulent Arinc akifungua mkutano wa Jukwaa la
Vyombo vya Habari Afrika na Uturuki mjini Ankara, Uturuki wiki
iliyopita. Mkutano huo ulishirikisha wawakilishi wa vyombo vya habari na
wadau wengine kutoka nchi 54 za Afrika.
Mhariri wa Habari wa gazeti la Nipashe Jumapili, Beatrice Bandawe(wa
pili kushoto) akifuatilia mkutano wa Jukwaa la Vyombo vya Habari Afrika
na Uturuki mjini Ankara, Uturuki wiki iliyopita.
Mkurugenzi wa Raia Mwema aliyepata pia kuwa MhaririMtendaji wa gazeti
hilo na Kampuni ya New Habari Corporation 2006, John Bwire (kushoto) na
Mhariri wa Makala wa Habari Leo, Selemani Nzaro wakifuatilia mkutano wa
Jukwaa la Vyombo vya Habari Afrika na Uturuki mjini Ankara, Uturuki wiki
iliyopita. Mkutano huo ulioandaliwa na ofisi ya Waziri Mkuu Uturuki,
ulishirikisha wawakilishi wa vyombo vya habari na wadau wengine kutoka
nchi 54 za Afrika.
Profesa, Dk. Mohamed Bakari, raia wa Kenya anayefundisha Chuo Kikuu cha
Fatih nchini Uturuki, akipokea tuzo maalumu iliyotolewa kwa niaba ya
Naibu Waziri Mkuu Uturuki, Bulent Arinc baada ya kuwasilisha mada katika
mkutano wa Jukwaa la Vyombo vya Habari Afrika na Uturuki kuhusu 'Afrika
ya Leo: Sera za Siasa, Uchumi na Mambo ya Nje' mjini Ankara, Uturuki
wiki iliyopita. Mkutano huo ulishirikisha wawakilishi wa vyombo vya
habari na wadau wengine kutoka nchi 54 za Afrika.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia wakati Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo
Leo, Willy Edward (mbele kwenye video) akiwasilisha mada katika mkutano
wa Jukwaa la Vyombo vya Habari Afrika na Uturuki kuhusu 'Vyombo vya
Habari kama kichocheo cha ushindi wa vita dhidi ya migogoro na ugaidi'
mjini Ankara, Uturuki wiki iliyopita. Mkutano huo ulioandaliwa na ofisi
ya Waziri Mkuu Uturuki, ulishirikisha wawakilishi wa vyombo vya habari
na wadau wengine kutoka nchi 54 za Afrika
No comments:
Post a Comment