Friday, May 18, 2012

MWILI WA MAFISANGO KUAGWA KESHO TCC CLUB, CHANG'OMBE

Aliyekuwa kiungo maili wa Simba na timu ya Taifa ya Rwanda (Amavubi),  Patrick Mutesa Mafisango (pichani) aliyefariki kwa ajali ya gari alfajili ya leo katika eneo la Veta Keko jijini Dar es Salaam, anatarajiwa kuagwa kesho.

Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Simba Godfrey Nyange Kabulu amesema kuwa mwili wa marehemu Mafisango utaagwa katika viwanja vya Sigara (TTC CLUB), Chang'ombe jijini Dar es Salaam kuanzia majira ya saa 2:00 asubuhi na kusafilishwa Mei 19 kwenda kwao Congo DRC kwa mazishi.

Habari katoka katika eneo la tukio zimesema kuwa ajali hiyo imetokea baada ya kumkwepa mwendesha pikipiki na kisha gari la Mafisango kupinduka.

Watu wengine watano waliokuwa na Mafisango walijeruhiwa vibaya wakati wakitoka katika Ukumbi wa Maisha Klabu Masaki jijini Dar es Salaam akiwa na marafiki zake wavulana watatu na wasichana wawili .
“Msiba huu ni pengo kubwa kwa Simba kutokana na umuhimu wake akiwa uwanjani hivyo basi sina mengi ya kusema zaidi ya kuwa na pigo mara baada ya kuondokewa na mchezaji mahili katika timu yetu”alisema Kabulu.

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha mchezaji huyo na kusema kuwa ni Msiba mkubwa kwa familia ya Soka kwani Mafisango kwa kipindi chote alichocheza mpira hapa nchini akiwa na timu ya Azam na baadaye Simba, aliifanya kazi yake ya kucheza mpira kwa bidii.

Ofisa habari wa TFF Boniface Wambura alisema kuwa kifo cha nyota huyo ni pigo kubwa si tu kwa familia yake na timu alizochezea, bali ukanda mzima wa Afrika Mashariki na Kati ambapo changamoto zake zilikuwa dhahiri uwanjani.

Wambura alisema wakati mauti yanamkuta, Mafisango alikuwa ameitwa Amavubi kwa ajili ya mechi za mchujo za Kombe la Dunia, Kanda ya Afrika zinazochezwa mapema mwezi ujao.

“TFF inatoa pole kwa familia ya Mafisango, klabu ya Simba, Shirikisho la Mpira wa Miguu Rwanda (FERWAFA) na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito”alisema Wambura 
 
 
 
 

WASHIRIKI WA BIGBROTHER STARGAME 2012 WAZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI BAADA YA KUREJEA

Aliyekuwa Mwakilishi wa Tanzania katika Shindano la msimu wa 7 wa  Big Brother Stargame 2012 wapili kulia Bw.Julio Batalia  akizungumza na  waandishi wa habari kwenye mkutano uliofanyika kwenye hoteli ya Southernsun jijini Dar es salaam , wa pili kutoka kulia ni Mshiriki wa Big Brother Stargame 2012 Bi,Hilda Reiffenstein, kulia ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Multichoice Tanzania Bi Furaha Samalu wa mwisho kulia na kushoto ni Meneja Uhusiano wa Maltchoice Tanzania Barbara Kambogi
Alikyekuwa Mshiriki wa Big Brother Stargame 2012 Bi,Hilda Reiffenstein akizungumza na wanahabari kwenye hoteli ya Southersun jijini Dar es salaam leo, kulia ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Multichoice Tanzania Bi Furaha Samalu wa mwisho kutoka kushoto ni Meneja Uhusiano wa Maltchoice Tanzania Barbara Kambogi na Bw.Julio Batalia aliyekuwa mshiriki wa Bigbrother Stargame 2012
Afisa Mahusiano wa Multichoice Tanzania Barbara Kambogi wakwanza(kushoto) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ambapo ametolea ufafanuzi mfumo uliotumika mwaka huu katika kuchagua nchi itakayotoka katika shindano hilo  Afisa Mahusiano wa Multichoice Tanzania Barbara Kambogi wakwanza(kushoto) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ambapo ametolea ufafanuzi mfumo uliotumika mwaka huu katika kuchagua nchi itakayotoka katika shindano hilo  
Waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo leo.PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE 
 

KILIMANJARO PREMIUM LAGER YATOA UBANI WA MILIONI MOJA KWA MSIBA WA MAFISANGO

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe akiwafariji kina mama waombolezaji  wakati alipokwenda kuhani  msiba wa mchezaji wa Simba Sports Club, Patrick Mafisango huko Chang'ombe jijini Dar es Salaam jana. Mafisango alifariki kwa ajali ya gari alfajiri ya jana. Bia ya Kilimanjaro premium Lager, inayodhamini Simba na Yanga, imetoa ubani wa milioni moja katika msiba huo.

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe (kushoto), akiwa katika mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa Timu ya Simba, Geofrey Nyange 'Kaburu' wakati alipokwenda kuhani msiba wa mchezaji wa Simba Sports Club Patrick Mafisango huko Chang'ombe jijini Dar es Salaam jana. Mafisango alifariki kwa ajali ya gari alfajiri ya jana. Bia ya Kilimanjaro Premium Lager inayodhamini timu za Simba na Yanga imetoa ubani wa milioni moja katika msiba huo

KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI YAWAPA SEMINA YA UENDESHAJI WA MITANDAO NA MAADILI KATIKA KUPASHA HABARI ZA MASOKO

Mmiliki wa Mtandao wa Lukaza Blog Josephat Lukaza akipokea cheti chake kutoka kwa Ephraim Mafuru Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL), katikati ni Teddy Mapunda Mkurugenzi wa Mawasiliano (SBL) kulia ni David Shayo wa (SBL)


 Mkurugenzi wa mtandao wa www.fullshangweblog.com akipokea cheti chake kutoka kwa Ephraim Mafuru Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) mara baada ya kumalizika kwa semina ya Mablogger kuhusu usimamizi na maadili ya upashaji wa habari na masoko katika  uendeleshaji wa blogu na mitandao mingine, iliyofanyika leo kwenye makao makuu ya kampuni hiyo yaliyoko Oysterbay jijini Dar es salaam, katikati ni mkurugenzi wa mawasiliano wa kampuni hiyo Teddy Mapunda
 Mkurugenzi wa Fullshangweblog kushoto akizungumza na mkurugenzi wa 8020fashion Shamimu Mwasha  mara baada ya semina hiyo, kulia ni Mkurugenzi wa blogu ya Father Kidevu.
mkurugenzi wa 8020fashion Shamimu Mwasha akipokea cheti chake Ephraim Mafuru Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) katikati ni mkurugenzi wa mawasiliano wa kampuni hiyo Teddy Mapunda.
Mroki Mroki  kutoka blogu ya Father Kidevu kushoto akipokea cheti chake.
 Mwendeshaji wa Blogu ya Mtaa kwa Mtaa Othman Michuzi kushoto akipokea cheti chake.
 Mkurugenzi wa Blogu ya Jiachie Ahmed Michuzi kushoto akipokea cheti chake.
 Mkurugenzi wa kampuni ya R&R Caroline Gul kushoto  akipokea cheti chake.
 Mkurugenzi wa mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti Teddy Mapunda akifafanua jambo katika semina ya uendeshaji wa mitandao na maadili ya upashaji wa habari za masoko katika blogu na mitandao mingine.

 Hadija Kalili wa Bongo Weekend nae  akipokea Cheti kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Epraimu Mafuru cheti cha mafunzo ya  Diageo Marketing Code yaliyotolewa na Kampuni ya Diageo. Katikati ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano wa SBL, Teddy Mapunda. Semina hii ilitolewa kwa Waendeshaji wa Blogu na mitandao ya Kijamii hususani Blogu (Magazeti tando). 
 Mahamood Zubeir wa Bin Zubeir Blog, akipokea Cheti kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Epraimu Mafuru cheti cha mafunzo ya  Diageo Marketing Code yaliyotolewa na Kampuni ya Diageo. Katikati ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano wa SBL, Teddy Mapunda. Semina hii ilitolewa kwa Waendeshaji wa Blogu na mitandao ya Kijamii hususani Blogu (Magazeti tando).
 Mhariri Mkuu wa The Habari Joachim Mushi, akipokea Cheti kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Epraimu Mafuru cheti cha mafunzo ya  Diageo Marketing Code yaliyotolewa na Kampuni ya Diageo. Katikati ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano wa SBL, Teddy Mapunda. Semina hii ilitolewa kwa Waendeshaji wa Blogu na mitandao ya Kijamii hususani Blogu (Magazeti tando).
Mablogger mbalimbali wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri katika semina ya uendeshaji wa mitandao na maadili ya upashaji wa habari za masoko katika blogu na mitandao mingine.
 Baadhi ya Bloggers Tukiwa Katika Picha ya Pamoja na Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Ephraim Mafuru wa kwanza kulia aliyekaa kwenye kiti akifuatiwa na Meneja Mahusiano Wa Kampuni ya Bia Serengeti Bi Teddy Mapunda baada ya Semina Kumalizika

WAKUU WAPYA WA WILAYA MKOANI ARUSHA WAAPISHWA NA MKUU WA MKOA WA ARUSHA

Mkuu wa wilaya ya Arusha John Mongela akiwa anaapa kiapo cha utiifu mbele ya mkuu wa mkoa wa arusha Magesa Mulongo leo
Akuu wa wilaya ya Arumeru  Nyirembe Munasa akiwa anakula kiapo cha uaminifu mbele ya mgeni rasmi
 Wakuu wa wilaya wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa mkoa  wa Arusha (picha zote na  Gladness Mushi-Arusha
 

Katika jiji la Arusha leo wakuu wapya wilaya wameapishwa ambapo  Mkuu wa mkoa wa Arusha magesa mulongo amewaotaka wasiliwe sifa na badala yake wahakikishe kuwa wanajikita zaidi katika kutatua kero za  wananchi.

Mbali na hayo aliwataka washirikiane na Madiwani katika kutatua tatizo la hati chafu ndani ya halmashauri kwa kuwa kati ya halmashauri zote jijini hapa iliyo na hati safi kidogo ni halmashauri ya Meru pekee

Pia aliwataka wakuu hao kuhakikisha hawapigwi chenga na sheria mbalimbali hasa za vijiji na ile ya asilimia ishirini kwa kila lkijiji kwa kuwa kwa sasa halmashauri zinakwepa sheria hiyo na hali hiyo inapelekea wenyeviti wa vijijiji kuwa katika hali nghumu ya kiutendaji

TASWIRA ZA RAISI KIKWETE HUKO WASHINGTON DC LEO

President Jakaya Mrisho kikwete speaks during a high level breakfast briefing on scaling up nutrition at the Dirksen office building in Washington DC May 17, 2012. Together with him at the High table are the minister of international Cooperation of Canada  Ms Beverly J. Oda, UNFP Executive Director Ms Ertharin Cousin and the CEO of Concern Worldwide, Mr Tom Arnold.
President Jakaya Mrisho kikwete speaks during a high level breakfast briefing on scaling up nutrition at the Dirksen office building in Washington DC May 17, 2012.
President Jakaya Mrisho kikwete greets the USAID Administrator Dr Raj Shah after taking part in a high level breakfast briefing on scaling up nutrition at the Dirksen office building in Washington DC May 17, 2012. right is the Tanzania Ambassador to the US Ms Mwanaidi sinare Maajar and second right is Ms Liberata Mulamula, Personal Assistant to the President (Diplomatic Affairs)
 

No comments:

Post a Comment