Thursday, May 10, 2012

 

Mkuki na Nyota Wazindua Kitabu cha Kemia cha KiswahiliMkurugenzi Mtendaji wa Mkuki na Nyota Publishers, Walter Bgoya.
KAMPUNI ya Uchapishaji wa Vitabu na machapisho anuai kwa mara ya kwanza imezindua kitabu cha somo la Kemia kilichochapishwa kwa lugha nyepesi ya kiswahili. Kitabu hicho kilichopewa jina la Furahiya Kemia (Enjoy Chemistry) kilichochapishwa kwa ushirikiano na Taasisi ya HakiElimu kimezinduliwa Mei 9, 2012 na Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu, Bi. Elizabeth Missokia.Akizungumza katika uzinduzi huo, Bi. Missokia alisema kuzinduliwa kwa kitabu hicho kutaleta chachu ya wanafunzi kupenda masomo ya sayansi hasa Kemia ambayo yamekuwa yakiwatatiza wanafunzi wengi kutokana na lugha ya kigeni inayotumiwa.Alisema ndani ya kitabu hicho wanafunzi wataweza kusoma na kuelewa vizuri somo la Kemia kwa lugha nyepesi ya Kiswahili jambo ambalo linaibua morali ya wanafunzi kuona masomo ya sayansi ni ya kawaida kujifunza kama yalivyo masomo mengine.Awali akizungumza kabla ya uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Mkuki na Nyota Publishers, Walter Bgoya alisema kitabu hicho kimechapishwa kwa lugha mbili yaani Kiswahili na Kiingereza ili kuwarahisishia wanafunzi kujifunza sayansi ya Kemia kwa lugha mama ya Kiswahili.Aidha alisema kitabu hicho kimepitiwa na kukubaliwa na Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) kwamba kinaweza kutumika kutokana na kuwa na maneno rahisi na sahihi ya Kiswahili ambayo yatawarahisishia wakati wa kujifunza mada anuai za Kemia hasa kidato cha kwanza.Pamoja na hayo, Bgoya aliishukuru taasisi ya HakiElimu kwa kusaidia kuchapishwa kwa kitabu hicho na kuwataka wadau wengine waungane na juhudi hizo za kuinua lugha ya Kiswahili katika matumizi ya kufundishia hata masomo ya sayansi.Naye akitoa maoni yake juu ya kitabu cha Furahiya Kemia mmoja wa walimu wa Sayansi, John Bosco alisema kitabu hicho kitakuwa daraja litakalo wawezesha wanafunzi kuvuka na kuyapenda masomo ya sayansi hasa kemia. Alisema kitabu hicho kina mazoezi ya kutosha kiasi cha kumfanya mwanafunzi apende kujifunza kwa dhati.

 

 

 

 

KUMEKUCHA MISS HIGHER LEARNING DODOMA
TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO MKUU WA MAJAJI WANAWAKE DUNIANI.


Rais imteulewa Chama cha Majaji na Mahakimu WanawakeDuniani (AIWJ),Mheshimiwa Jaji EusebiaMunuo,(katikati)akisikiliza kwamakini wajumbe wengine wakichangia mada kwenye Mkutano huo, mara baadaya kukabidhiwa rasmi nafasi ya kuwa Raisi
wa Chama hicho.
Raisi Mteule wa Chama cha Majaji na Mahakimu,Mhe. Eusebia Munuo akikabidhiwa Bango na aliyekuwa Raisi wa Chama hicho, Lady Brenda M. Hale.
Sherehe, ndere mo na vifijo katika Ukumbi waMikutano, mara baada Mheshimiwa Jaji Munuo kutangazwa rasmi kuwa Raisi mpya wa Chama hicho naTanzania kukabidhiwa rasmi nafasi ya kuwa Mwenyejiwa Mkutano ujao wa Chama hichoMwaka 2014
Ujumbe wa Majaji naMahakimu kutoka Tanzania, wakiwa kwenye picha ya pamoja, mara baada ya kukabidhiwa rasmi Bango la Chama hicho cha Majaji Duniani(AIWJ)nakupe wa nafasi ya kuwa Mwenyejiwa Mkutano Mkuu ujao wa Chama hicho utakofanyika Mwezi Mei, 2014 MjiniArusha – Tanzania.
 ---
Chama cha MajajiWanawakeduniani  (IAWJ) kilikuwanamkutano wake Mkuuuliofanyika London Uingerezatarehe2-5 Mei 2012.

Kwenye Mkutano huo Tanzania,iliwakilishwa naMajaji naMahakimu ambao ni wanachama wa IAWJ (International Association of Women Judges)na Chama cha MajajinaMahakimu Tanzania (TAWJA).

Katika mkutano huo,viongozi mbalimbali walichaguli wakushika nyadhifa kukiongoza chama hicho kwa kipindi cha miakamiwili.

Mhe.JajiEusebiaMunuo, ambae pia ni Jaji waMahakama yaRufani Tanzania alichaguliwa kuwa Rais wa chama hicho.

Pamoja na kuchaguliwa ktk nafasi hiyo,Mheshimiwa Jaji Munuo,pia alikabidhiwa rasmi Bango la chama hicho.Kwa kukadhiwa Bango hilo,Tanzania sasa imekabidhiwa rasmi nafasi ya kuwa mwenyeji wa Mkutano mkuu ujao w achama hicho.Mkutano huo unatarajiwa kufanyika mwezi Mei 2014 katikaUkumbi waMikutano wa AICC Arusha Tanzania.

Ujumbe wa Tanzania uliokuwepo kwenye mkutano huo ulipokea wa dhifa hu0
kwa shangwe nafuraha kubwa kama inavyonekana kwenyepicha.

Tanzania itashikilia nafasi hiyo yaUrais wa chama hicho mpaka mwaka 2014.

RAIS KIKWETE ATEMBELEA SOKO LA HISA LA MITAJI YA MAZAO LA ETHIOPIA (ETHIOPIA COMMODITY EXCHANGE

Rais Jakaya Kikwete na ujumbe wake wakiwa katika ofisi za Soko la Mitaji na Mazao la Ethiopia leo Mei 10, 2012 alipotembelea na kuelezwa mafanikio ya soko hilo ambapo wakulima wa wakubwa na wa kawaida wanafanya biashara ya mazao kitaifa na kimataifa kwa njia ya kisasa.
Rais Jakaya Kikwete akiwekewa kahawa katika kikombe  baada ya kishuhudia namna kahawa inavyoandaliwa kaisili katika ofisi za Soko la Mitaji na Mazao la Ethiopia leo Mei 10, 2012 alipotembelea na kuelezwa mafanikio ya soko hilo ambapo wakulima wa wakubwa na wa kawaida wanafanya biashara ya mazao kitaifa na kimataifa kwa njia ya masoko ya hisa na mitaji
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipiga kengele kuashiria mwanzo wa soko katika makao makuu ya za Soko la hisa na Mitaji ya Mazao la Ethiopia leo Mei 10, 2012 alipotembelea na kuelezwa mafanikio ya soko hilo ambapo wakulima wa wakubwa na wa kawaida wanafanya biashara ya mazao kitaifa na kimataifa kwa njia ya kisasa
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishuhudia wachuuzi wakiwa kazini baada ya  kufunguliwa kwa soko katika makao makuu ya za Soko la hisa na Mitaji ya Mazao la Ethiopia leo Mei 10, 2012 alipotembelea na kuelezwa mafanikio ya soko hilo ambapo wakulima wa wakubwa na wa kawaida wanafanya biashara ya mazao kitaifa na kimataifa kwa njia ya soko la hisa na mitaji.PICHA NA IKULU 

KAMPUNI YA BIA YA TANZANIA (TBL) ILIPOTANGAZA UDHAMINI KWA TIMU YA TAIFA. TAIFA STARRais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Leodger Tenga (kushoto) akibadilishana Mkataba wa Udhamini wa Bia ya Kilimanjaro kwa Timu ya Taifa "Taifa Stars" na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Robin Goetzsche (kulia) wakati wa hafla fupi iliyofanyika usiku huu kwenye ukumbi wa Kibo,ndani ya Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kilimanjaro.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Leodger Tenga (pili kushoto waliokaa) na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Robin Goetzsche (pili kulia waliokaa) wakisaini Mkataba wa Udhamini wa Bia ya Kilimanjaro kwa Timu ya Taifa "Taifa Stars" wakati wa hafla fupi iliyofanyika usiku huu kwenye ukumbi wa Kibo,ndani ya Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kilimanjaro.Wanaoshuhudia ni viongozi mbali mbali wa TFF na Kampuni ya Bia Tanzania.
Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Steven Kilindo (kulia waliokaa) na Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria, Maadili na hadhi za Wachezaji,Alex Mgongolwa wakisaini mkataba huo.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe akipiga mpira kuashiria kuwa sasa udhamini umekalika kwa Timu ya Taifa ya Tanzania "Taifa Stars" wakati wa hafla fupi iliyofanyika usiku huu kwenye ukumbi wa Kibo,ndani ya Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kilimanjaro.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Robin Goetzsche akitoa hotuba yake fupi wakati wa hafla hiyo iliyofanyika usiku huu kwenye ukumbi wa Kibo,ndani ya Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kilimanjaro.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Leodger Tenga akitoa shukrani kwa Kampuni ya Bia Tanzania kwa kuweza kuidhamini timu ya Taifa "Taifa Stars" kupitia Bia yake ya Kilimanjaro,wakati wa hafla fupi iliyofanyika usiku huu kwenye ukumbi wa Kibo,ndani ya Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kilimanjaro.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe akitoa maelezo mafupi ya Udhamini huo kwa wageni mbali mbali waliofika ukumbini hapo.Picha Kwa Hisani Ya Michuzi Blog

No comments:

Post a Comment