Tuesday, May 8, 2012

 

 

 

RAISI MSTAAFU BENJAMINI MKAPA ATINGA KWA PILATO KISUTU KWAAJILI YA KUTOA USHAHIDI KATIKA KESI YA PROF MAHALU



Mkapa akiingia Mahakama ya Kisutu kutoa ushahidi.

Akisindikizwa kuelekea kizimbani.

Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa akitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo, kutoa ushahidi wake katika kesi inayomkabili aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa  Costa Mahalu,  anayekabiliwa na shtaka la uhujumu uchumi.

Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa akiondoka Mahakama hapo baada ya kutoa ushahidi wake.
Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, leo amepanda kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam na kuhojiwa na mawakili wa serikali na wanaomtetea aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini Italy, Costa Mahalu, kwenye kesi ya ufujaji fedha katika ununuzi wa jengo la ubalozi inayomkabili balozi huyo.Jengo hilo lilinunuliwa kwa shilingi, bilioni 2.9.Source Global Publisher Tz NA FULL SHANGWE BLOGU

 

MAWAZIRI WA JAMHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA WAAPA ASUBUHI HII IKULU

 Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika viwanja vya Ikulu asubuhi hii ili kuanza kazi ya kuapisha mawaziri wapya aliowateua hivi karibuni Fullshangweblog ikiwa katika viwanja vya Ikulu inashuhudia kuapishwa huku kwa mawaziri na kukuletea moja kwa moja kutoka viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam.
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza na Katibu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue kabla ya kuanza kwa kuapiswa mawaziri hao.
 Dk. Harrison Mwakyembe akila kiapo kuwa waziri wa Uchukuzi mbele ya Rais Jakaya Kikwete kwenye viwanja vya Iku asubuhi hii.
 Shamsi Vuai Nahodha akila kiapo kuwa waziri wa Ulinzi mbele ya Rais Jakaya Kikwete.
Dk Husein Mwinyi akila kiapo kuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii mbele ya Rais Jakaya Kikwete.
 Profesa Jumanne Maghembe akisaini kiapo mara baada ya kuapa kuwa waziri wa  maji na umwagiliaji
 Hawa Ghasia akila kiapo
 Mh. Mathias Chikawe waziri wa Sheria na Katiba.
Mh. George Mkuchika akipongezwa na Rasi mara Baada ya kula kiapo.Kwa Hisani ya Full Shangwe Blogu
 
 
 

GRAND MALT YAPANDA MITI 30 KATIKA KITIVO CHA ELIMU CHA CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM) ASUBUHI YA LEO

Meneja Wa Kinywaji Kisicho Na Kilevi Cha Grand Malt Bi Consolata Adam akipanda Moja ya Miti hiyo katika Kitivo Cha Elimu Cha Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOM) asubuhi ya leo.Zoezi la Upandaji Miti La Grand Malt lilikwenda Sambamba na Zoezi la Uzinduzi wa Excel With Grand Malt Ambapo Itashirikisha Vyuo Viwili UDOM na CBE vyote vikitokea Mkoa Wa Dodoma
Mmoja wa Wanafunzi Wa Kitivo Cha Elimu Cha Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Anne Sango akipanda moja ya Miti iliyotolewa na Grand Malt katika Kitivo hiko Cha elimu cha Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOM) asubuhi ya Leo
Mmoja wa wanafunzi wa Kitivo Cha Elimu Cha Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOM) akipanda mti katika zoezi la upandaji miti lililofanya na Grand Malt asubuhi ya leo Chuoni Hapo
Mmoja wa Wafanyakazi wa Grand Malt Mkoani Dodoma akiweka miche ya Miti tayari kwa Kupanda katika Kitivo Cha Elimu Cha Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) asubuhi ya Leo
 Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania kanda ya Kati Bwana Nick Tesha alipokua akitoa shukrani kwa wanafunzi wakitivo cha elimu Cha Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) kwa kujitokeza katika Zoezi la Kupanda kwa malengo ya kutunza mazingira.Zoezi hilo lilifanyika asubuhi ya leo katika kitivo cha Elimu Cha Chuo Kikuu Cha Dodoma.
Meneja wa Kinywaji Cha Grand Malt Bi Consolata Adam (Katikati) akinywa kinywaji kisicho na Kilevi Cha Grand Malt Mara baada ya Zoezi la Upandaji Miti Kumalizika katika Kitivo Cha Elimu Cha Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) asubuhi ya Leo
 Meneja wa Kinywaji Cha Grand Malt Bi Consolata Adam Akiwa katika Picha ya Pamoja na Baadhi ya Wanafunzi na wafanyakazi wa kampuni ya Bia Tanzania Mkoani Dodoma mara baada ya zoezi la upandaji miti kumalizika katika Kitivo Cha Elimu Cha Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) asubbuhi ya leo
Meneja wa Kinywaji Cha Grand Malt Bi Consolata Adam (katikati) akisikiliza maelekezo kutoka kwa Waziri wa Habari wa Kitivo Cha Elimu Cha Chuo Kikuu Cha Dodoma Mh Rajabu P juu ya Zoezi la Upandaji miti iliyopandwa na Klabu ya mazingira ya Kitivo hiko cha Elimu asubuhi ya leo
 
 
 
 

Mjumbe Mwenye Hasira Kali Sana:"Nakuomba Uufikishe Ujumbe Huu Kwa Waziri Kigoda"

Napenda kutoa pongezi zangu kwa Mheshimiwa Kigoda kwa kuchaguliwa kuiongoza wizara ambayo kwa sasa imekumbwa na kashfa nyingi sana hususan madudu ya TBS.
   Najua kwa uteuzi huu mheshimiwa Rais alifikiria sana na alimuona Kigoda kuwa ndie mtu anayefaa kuyasafishia mbali madudu haya.

Mheshimiwa Kigoda,
Kabla hujaakaa vizuri kwenye kiti chako cha uwaziri baada ya kuapishwa nakuomba kwanza ujiulize ni kitu gani hasa kilichomuondoa unayemrithi hicho kiti?
   Mie nitakusaidia kwa kukumbusha tu pamoja na kuwa najua unalielewa hilo fika.

Aliyekuwa hapo kabla yako anaitwa Mheshimiwa Chami ambaye sasa kazi yake ni mbunge, na kilichomtoa hapo ulipo wewe sasa ni yale madudu ya EKELEGE/TBS ambayo yametambaa kila kona ya hiyo ofisi.

Haya madudu usipoyaondoa basi ujue yataanza kukutambaa na wewe. Niliwahi kumuandikia Mheshimiwa Chami email nyingi ambazo najua alikuwa hata hazisomi na hata kama alizisoma basi alikuwa anadharau tu.

Wabunge walimshauri Chami amsimamishe kazi huyu Ekelege ili apishe uchunguzi lakini alikataa na kusema kufanya hivyo itakuwa ni kumnyima haki Ekelege.

Ripoti ya wabunge ilipelekwa kwa spika kuhusu madudu haya na spika aliipeleka kwa CAG ili ifanyiwe kazi lakini Chami kila kukicha alikuwa anasema hajaiona hiyo ripoti hivyo anaisubiri ikimfikia ndio atajua afanye nini.

Hii ilidhihirisha jinsi huyu bwana asivyo mchapa kazi. Yaani wewe tuhuma zote hizi nzito na ushahidi wote huu unaotolewa kwenye vyombo vya habari na wabunge wakisapotiwa na Mie mjumbe mwenye hasira kali pamoja na mwenyekiti wangu Mjengwa bado kaka ulikuwa huoni sababu ya kufanya lolote bali unakaa tuuuuu ofisini unataka CAG akufuate akupe report.

Mie nadhani kwa kiongozi bora kama vile Magufuli au Mrema enzi zake ungeinuka na kwenda mwenyewe kwa CAG kuomba kuiona hiyo ripoti. Kitendo cha kila siku kusema hujaiona hiyo ripoti wakati hata Naibu wako Nyalandu anakuambia umsimamishe kazi Ekelege ni uzembe wa hali ya juu na sidhani kama huyu mtu anafaa hata kuwa Mkuu wa Wilaya.

Kile kitendo cha kudharau ushauri wa wabunge ni kitendo cha kudharau Watanzania wote kwani wao ndio waliowachagua hao wabunge wakawawakilishe.

Turudi kwenye ushauri.
Mheshimiwa Rais ameisha fanya kazi yake ambayo ni kumtoa mtu wa juu kabisa ambaye ni Chami, sasa kinachotakiwa ni wewe Mheshimiwa Kigoda kumalizia kazi aliyoianzisha Rais.

Kumbuka unapoua nyoka inabidi uponde ponde kichwa sio kukanyaga mkia. Haya madudu yalitokea kwa Ekelege na vimiradi vyake vya ukaguzi wa magari nje ya nchi ambapo kuna kampuni hewa huko Hongkong na na Uk ambapo kuna hiii kampuni ya WTM UTILITY ambayo yenyewe ndio duka kubwa la kuuza vyeti vya EKELEGE/TBS.

Hizi tenda zilitakiwa zilitolewe miaka mitano iliyopita na sasa huu mwezi wa tano ulitakiwa uwe ndio mwisho wa kuuza vyeti lakini inavyoonekana jamaa wameamua kuendelea mpaka hapo watakaposimamishwa na Serikali, lakini sio TBS kwa sababu TBS ndio wao.

Mie nitakusaidia kusafisha haya madudu kwa kukupatia ushahidi nilionao bure na nitasafiri mpaka huko kwa nauli yangu ili nikupatie ushahidi mwingi nilionao ambao Chami aliupuuzia na sasa kibarua kimeota nyasi.

Kule Iringa kuna mti mmoja unaoitwa MKAYEWA au waswahili huuita mti wa kisamvu. Huu mti ukiukata baada ya wiki moja utakuta umeota tena kwa hiyo kama unataka kuuondoa kabisa inakubidi ung'oe kabisa huu mti na mizizi yake yote ili usiote tena.

Kwa kusema hivyo, nakushauri kuwa inabidi uwaondoe wote waliohusika na hizi tenda feki za ukaguzi wa magari kuanzia kwenye hivi vikampuni kama WTM mpaka kwa huyo mwenyewe EKELEGE ambaye Chami alimkumbatia sana na mwisho wake kang'olewa yeye.

Hebu jiulize , kwa nini uhatarishe kibarua chako kulinda watu ambao wamepewa dhamana ya kukagua magari badala yake wameamua kuuza vyeti vya TBS.

Mie sidhani hata kama kuna hela lakini sio nyingi za kumfanya mtu apoteze nafasi yake ya uwaziri. (mshahara wa waziri, marupurupu ya ubunge na heshima uliyopewa ni kubwa sana )

Mie nakuomba uipitie report ya CAG na uifuate mwenyewe au hata ukimtuma dereva lakini uipate uisome na uifanyie kazi, usikae chini kama jamaa yangu Chami ambaye alikuwa anatoa sababu ambazo najua yeye mwenye hapo alipo sasa akikaa nyumbani kwake anasema ningejua????  Ningemsikiliza mjumbe mwenye hasira kali  kama sio akina Zito Kabwe na Filikunjombe.

Mwenyekiti Mjengwa
Nakuomba uufikishe huu ujumbe kwa Mheshimiwa Kigoda ili aufanyie kazi

Nakuomba umuwekee na hizi picha hapa juu ili zimpe taswira halisi ya haya madudu
Asante sana
MJUMBE MWENYE HASIRA KALI SANA

No comments:

Post a Comment