Wednesday, May 2, 2012

TASWIRA ZA BASI LA NBS LILILOPATA AJALI LEO MAJIRA YA SAA KUMI ASUBUHI LIKIELEKEA ARUSHA

Leo majira ya saa 4.00 asbh kumetokea ajali mbaya ya basi la NBS linalotokea Tabora kwenda Arusha, basi hilo lilipasuka Taili la mbele na kugonga mti na kuung'oa na kisha kupinduka.
hadi sasa kuna maiti sita zilizowasilishwa Mortuary na Dereva wa gari hilo pia ni marehemu ila bado maiti yake haijatolewa kwani amebanwa hadi basi hilo likatwe ndiyo atolewe


TUME YA KURATIBU MAONI YA KATIBA MPYA YAKABIDHIWA OFISI KATIKA JENGO JIPYA LA WIZARA YA MAMBO YA NDANI

 Katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue kushoto akimtembeza Mwenyekiti wa Tume ya kuratibu maoni ya Katiba mpya Waziri mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba  katika ofisi mpya ya Tume hiyo iliyopo katika jengo jipya la Wizara ya mambo ya Ndani ghorofa ya kwanza katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika leo kwenye Wizara ya mambo ya ndani jijini Dar es salaam, katikati ni Celina Kombani Waziri wa Sheria na Katiba.
Katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue kushoto akimueleza jambo  Mwenyekiti wa Tume ya kuratibu maoni ya Katiba mpya Waziri mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba wakati wa makabidhiano ya  ofisi ya Tume hiyo iliyopo katika jengo jipya la Wizara ya mambo ya Ndani ghorofa ya kwanza , wa pili kutoka kushotoni Celina Kombani Waziri wa Sheria na Katiba na Angela Kairuki mbunge wa CCM viti maalum Dar es salaam
 Ofisi inavyoonekana kwa ndani.
 Mwenyekiti wa Tume ya Kuratibu maoni ya Katiba Mpya Waziri mkuu mstaafu Jaji Joseph Wariomba wa tatu kutoka kulia akiwa pamoja na viongozi wengine wakibadilishana mawazo kabla ya kuanza kwa hafla hiyo.
 Baadhi ya wajumbe wa Tume ya Kuratibu maoni ya Katiba mpya wakiingia kwenye ukumbi wa mikutano tayari kwa kuanza  kwa hafla ya makabidhiano ya ofisi watakayoitumia.
 Baadhi ya wajumbe wa Tume ya Kuratibu maoni ya Katiba mpya wakiingia kwenye ukumbi wa mikutano tayari kwa kuanza  kwa hafla ya makabidhiano ya ofisi watakayoitumia.Picha Kwa Hisani ya Full Shangwe Blogu

WAKE WA VIONGOZI WATEMBELEA KAMBI YA CHANETA KIBAHA

Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akimkabidhi Mwenyekiti wa Chama za Netiboli Tanzania (CHANETA), Anna Bayi moja kati ya katoni 40 za maji ya kunywa wakati wake wa viongozi  walipotembelea kambi ya timu ya taifa ya netiboli, Taifa Queens kwenye shule ya sekondari ya Filbert Bayi, Kibaha Mai 1, 2012.  Kulia ni Mke wa Mkamu wa Rais, Mama Zakia Bilal  na watatu kulia pia ni  Mke  wa Makamu wa Rais, Mama Asha  Bilal kushoto ni Mama Hasna Kawawa.
Wake wa Viongozi Wakuu wa Serikali ambao ni wananchama wa New Millenium Group wakihuhudia mazoezi ya timu ya taifa ya netiboli, Taifa Queens kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari ya Filbert Bayi iliyopo Kibaha, Mai Mosi 2012.  Kutoka kushoto ni Regina Lwassa, Zakia Bilal, Mwenyekiti wa CHANETA, Anna Bayi, Tunu Pinda, Anna Mkapa, Asha Bilal na Khadija Mwinyi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri mkuu Pinda akutana na viongozi wa kampuni ya DuPont ya Marekani

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Bw. James Borel (kushoto kwake) ambaye ni Makamu wa Rais Mtendaji  wa Kampuni  ya DuPont  ya  Marekani inayo jishughulisha na kilio baona timu yake, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Mai 2, 2012.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Miss Tabata kufanyika Juni 1 Dar West

Na Mwandishi Wetu 
 
Shindano la kumsaka mrembo wa Tabata, Miss Tabata 2012, litafanyika Juni 1 katika ukumbi wa Da West Park, Tabata.
 
Mratibu wa shindano hilo Joseph Kapinga amesema kuwa onyesho hilo pia kutakuwa na sherehe kabambe ya kusherehekea miaka 10 ya Miss Tabata.
 
“Shindano la mwaka huu litakuwa ni la aina yake kwa sasabu hii itakuwa ni mwaka wetu wa 10 kuanda Miss Tabata. Tutakuwa na burudani nyingi kutoka nje na ndani ya nchi. Pia tutahakikisha tunashirikisha warembo bomba wenye hadhi ya kushinda taji la Miss World,” Kapinga alisema mratibu huyo wa Bob Entertainment na Keen Arts.
 
Kapinga alisema kuwa warembo waliyowahi kushinda mataji tofauti tofauti la shindano hilo pia watakuepo kusherekea miaka 10 ya Miss Tabata.
 
Warembo watakaoshiriki kwenye shindano wanaendelea na mazoezi kila siku katika ukumbi wa Dar West Park.
Warembo hao ni Neema Saleh (18), Noella Michael (19), Queen Issa (20), Hycalisa Joseph (18), Phillios Lemi (19), Wikllihemina Mvungi (20) na Nightness Rajab (19). Wengine ni Suzanne Pancras (19), Caroline David (21), Khadija Nurdin (19), Jamila Omary (18), Advent  Mamkwe (21), Nadya Marjeby (21), Axer Peter (20), Rahama Hassan (19), Mercy Mlay (21) na Diana Simon Laizer (20).
 
Kapinga aliwaomba warembo wenye sifa kuendelea kujitokeza waweze kupata wawakilishi bora katika shindano la Kanda ya Ilala.
 
"Bado milango iko wazi, mrembo yoyote anayejiamini kwamba ana vigezo anakaribishwa. Tunataka shindano la mwaka huu liwe na ushindani zaidi,” mratibu huyo aliongeza.Warembo 10 watachaguliwa kushiriki mashindano ya Miss Ilala na baadaye Miss Tanzania.Mrembo anayeshikilia taji la Tabata ni  Faiza Ally.

Warembo wa Tabata wamekuwa wakifanya vizuri katika mashindano ya Miss Tanzania ambapo mwaka juzi Consolata Lukosi alishinda nafasi ya tatu kabla ya kutangazwa kuwa balozi wa kinywaji cha Redds. Katika shindano la mwaka juzi Julliet William pia alishinda nafasi ya tatu katika ngazi hiyo ya taifa.
 
Juliet ndiye anayeshikilia taji la dunia la Miss Progressive International.

MATUKIO KATIKA PICHA MARA BAADA YA MBUNGE WA SEGEREA MAKONGORO MAHANGA KUSHINDA KESI LEO

Mbunge wa jimbo la Segerea (CCM) na naibu Waziri wa Kazi na Ajira Mhe. Makongoro Mahanga akilakiwa na wafuasi wa wake baada ya kuibuka kidedea katika kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa jimbo hilo  iliyokuwa inamkabili katika mahakama kuu ya Tanzania dhidi ya mgombea wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA  Bw. Fredi Mpendazoe.
Baadhi ya wafuasi wa Fredi mpendazoe na wafuasi wa Makongoro Mahanga wakiwa nje ya mahakama mara baada ya hukumu ya kesi hiyo kutolewa.
Wafuasi wa Freddy  Mpendazoe wakiwa na picha ya aliyekuwa mgombea  wao baada ya kushindwa kesi hiyo.
Askari wa jeshi la polisi wakiwa makini kulinda usalama mara baada ya kesi hiyo kuamuliwa katika mahakama kuu leo. (PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE)

EVANS BUKUKU'S COMEDY CLUB ILIVYOWABAMBA MASHABIKI NDANI YA NYUMBANI LOUNGE JIJINI DAR ES SALAAM

 Mchekeshaji wa maarufu nchini kutoka kundi la Vuvuzela Entertainment, Evans Bukuku akifanya vitu vyake ndani ya kiota cha Nyumbani Lounge jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wageni waliojitokeza kushuhudia.
 ...aha... aha wengine waliamua kuweka kumbukumbu.
Kila mmoja alikuwa na furaha.
 ...yani wewe hapa ni kazi tu
 ...wakifuatilia kwa ukaribu.
 Mchekeshaji wa maarufu nchini kutoka kundi la Vuvuzela Entertainment, Evans Bukuku akiwa katika sura ya kazi.
Mambo yakihifadhiwa.
Mchekeshaji maarufu nchini kutoka kundi la Vuvuzela Entertainment, Evans Bukuku akiwa pamoja na Enika wa kundi hilo wakionyesha maujuzi yao ya kuimba. Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog

WASHINDI WA KWANZA WA JENERATA NA BAJAJ PROMOSHENI YA "VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO" WAPATIKANA


 Meneja wa Bia ya Serengeti Lager Allan Chonjo akiongea na waandishi wa habari wakati wa kutangaza washindi wa Promosheni Vumbua Hazina chini ya Kizibo inayoendesha na kampuni ya bia ya Serengeti kupitia bia zake za Tusker Lager, Plisner Lager na Serengeti Lager, kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya Serengeti (SBL) Teddy Mapunda.


Meneja wa Bia ya Serengeti Premium Lager Allan Chonjo akiongea na waandishi wa habari wakati wa kutangaza washindi wa Promosheni Vumbua Hazina chini ya Kizibo inayoendesha na kampuni ya bia ya Serengeti kupitia bia zake za Tusker Lager, Plisner Lager na Serengeti Lager, kutoka kulia ni Meneja wa bia ya Tusker Ritah Mchaki, Mrisho kutoka shirika la Bahati Nasibu ya Taifa na  Teddy Mapunda mkurugenzi wa Mawasiliano (SBL)


Droo ya kwanza kabisa ya promosheni inayoendelea ya kampuni ya bia ya Serengeti Breweries LTD (SBL) inayojulikana kama‘Vumbua hazina chini ya kizibo’ imefanyika leo katika ofisi za kampuni hiyo, maeneo ya Oysterbay jijini Dar Es salaam.



Kampuni ya bia ya Serengeti ni kampuni tanzu ya kampuni ya DIAGEO PLC (UK) ya Uingereza na kupitia bidhaa zake, Serengeti Premium Lager, Tusker Lager na Pilsner Lager inaendesha promosheni hii tangu wiki iliyopita. Promosheni hii ya aina yake iliyosheheni zawadi mbalimbali kubwa na ndogo kama vile Jenereta , Pikipiki , Bajaji , Gari na zawadi zingine nyingi zikiwemo pesa taslimu na bia za bure.





Droo hii leo, ilihudhuriwa na waandishi wa habari, wasimamizi kutoka Bodi ya Bahati Nasibu Tanzania, wadau kutoka ndani na nje ya kampuni hii, wakiwemo kampuni ya kuendesha Bahati Nasibu ya PUSH MOBILE na wahakiki na wakaguzi kutoka PriceWaterHouseCoopers (PwC) kuonesha jinsi washindi wote watapatikana kihalali.





Akiongea katika hafla hii, meneja wa bia ya Serengeti Premium Lager, Bw. Allan Chonjo amesema kwamba “Tayari tumeweza kupata washindi waliopata pesa taslimu na wakafanikiwa kupata pesa zao kupitia MPESA ndani ya masaa 24.  Pia, washindi wamepatikana ambao wamejishindia zawadi za vinywaji vilivyopo katika promosheni hii.  Naomba nisisitize, kwamba promosheni hii inalenga kuinua na kubadilisha maisha ya watanzania hususani wateja wa bidhaa zinazozalishwa na kampuni yetu ikiwa ni sera mojawapo ya kampuni hii kuisaidia jamii kwa njia mbalimbali kupitia bidhaa zake zenye ubora wa kipekee.  Pia ningetaka niseme ni njia ya pekee ya kuwashukuru watanzania kwa ushirikiano wao kwetu”.





Mshindi wetu wa droo ya kwanza ni John Gati mwenye umri wa miaka thelathini na mbili kutoka Musoma ambaye amejishindia jenereta  pamoja na Godfrey Shao mwenye umri wa miaka ishirini na nne kutoka Mwanza aliyejinyakulia Bajaj.  Baada ya kuchezeshwa droo kwa umakini kabisa na Rita Mchaki -Meneja wa bia ya Tusker Lager alipiga simu kwa washindi  na ilikuwa dhahiri kwamba washindi walishtuka na kufurahia ushindi wao.  Baada ya maongezi machache, waliweza kujieleza vizuri majina yao kamili na wanapopatikana ili waweze kupatikana siku chache zijazo kwenye hafla fupi ya kuwakabidhi zawadi zao.

BREAKING NEWS:Makongoro Mahanga ashinda kesi ya uchaguzi jimbo la Segerea

Mbunge wa Jimbo la Segerea Na Naibu Waziri , Dk. Miltoni Makongoro Mahanga,
 
Makongoro Mahanga aibuka mshindi katika kesi ya kupinga ubunge dhidi yake iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea ubunge katika jimbo la segerea kupitia tiketi ya Chadema Mh Fred Mpendazoe. Katika Uchaguzi uliofanyika Mwaka 2010 na kumfanya Mahanga Kuibuka Mshindi kupitia ushindi huo Aliyekuwa Mgombea ubunge kwa tiketi ya Chadema alifungua kesi kwaajili ya kupinga Matokeo ya Ushindi wake kwa vigezo kuwa Uchaguzi huo ulikiuka taratibu na sheria za uchaguzi ambapo Hukumu Iliyotolewa leo Imemtangaza Mahanga kuwa Mshindi wa Kesi hiyo lakini Hakimu alitoa nafasi na Kusema endapo mlalamikaji akulidhika na Hukumu hiyo anaruhusiwa kukata rufaa. 
Hata hivyo Mpendazoe ametakiwa Kulipa gharama zote za Kesi Hiyo

No comments:

Post a Comment