Taswira Za Yale Maandamano Ya Wanaharakati Wanaodai Kura ya Maoni Dhidi ya Muungano Zanzibar
Mdau
wa kikundi cha Wazanzibari wanaodai kuitishwa kura ya maoni dhidi ya
Muunganoakisindikizwa na polisi kuondoka sehemu ya maandamano
Kiongozi
wa kikundi cha Wazanzibari wanaodai kuitishwa kura ya maoni dhidi ya
Muungano Rashid Salum Adiy akizungumza muda mfupi baada ya kushikwa na
polisi kwa kufanya maandamano kinyume na sheria
Kiongozi wa kikundi cha Wazanzibari wanaodai kuitishwa kura ya maoni dhidi ya Muungano Rashid Salum Adiy akizungumza na simu.
Jeshi la Polisi likitoa tahadhari kwa wananchi waliofika katika viwanja
vya baraza la wawakilishi wakidai kuwepo kwa kura ya maoni juu ya
Muungano
Kikosi maalum cha Polisi cha kuzuia fujo kikijipanga kukabiliana na wanaharakati waliofika baraza la Wawakilishi jana
Baadhi ya Wanaharakati waliokuwepo kwenye viwanja vya baraza la
wawakilishi wakisubiri hatima yao ya kutaka kuonana na Spika wa Baraza
la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho.
Hashim na wenzake wakiwa katika gari la Jeshi la Polisi likiwachukua na
kuwapeleka Madema, baada ya kukusanyika katika viwanja vya baraza la
wawakilishi wakidai kuwepo kwa kura ya maoni itakayoamua kuwepo au
kutokuwepo Muungan.Picha na Habari na Mdau Othman Maulid
Mbunge wa Ludewa (CCM), Deo Filikunjombe Akisaini Karatasi inayokusanya Saini za wabunge Za Kutokuwa na imani na Waziri Mkuu
Mbunge wa Ludewa (CCM), Deo Filikunjombe akisaini karatasi inayokusanya
saini za wabunge za kutokuwa na imani na Waziri Mkuu kwa lengo la
kuwasilisha kwa Spika mjini Dodoma. Kulia ni Naibu Kiongozi wa Upinzani
Bungeni, Kabwe Zitto.Picha na
Mohamed Mambo
WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA NA MATUKIO BUNGENI LEO
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wabunge, John Mnyika wa
Ubungo (kushoto), Kabwe Zitto wa Kigoma Kaskazini na Hamad Rashid wa
Wawi, kwenye jengo la Utawala la Bunge Mjini Dodoma Aprili 21, 2012.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Hoja ya Zitto ya kutaka Waziri Mkuu Pinda apigiwe Kura ya Kutokuwa na Imani naye yakwama kutokana na kanuni za Bunge
Spika wa Bunge, Anne Makinda |
Na Mwandishi Wetu-Dodoma
Spika wa Bunge, Anne Makinda amesema hoja ya kutaka kumpigia kura ya kutokuwa na imani Waziri Mkuu Mizengo Pinda, inayokusudiwa kupelekwa bungeni na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), ni batili na haina nguvu kwa kuwa haijakidhi matakwa ya kanuni.
Amewataka wabunge kuzisoma kikamilifu kanunzi zinazohusiana na hoja hiyo.
Wakati
Spika Anna akieleza hivyo, wabunge nao wamesema wana imani na utendaji
kazi wa Waziri Mkuu Mizengo Pinda na wasingepanda kumwondoa katika
wadhifa huo, lakini tatizo kubwa ni mawaziri wake.
Pia, wamesema hoja ya kutaka kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye, inalenga kumshinikiza kuwawajibisha mawaziri wanaotuhumiwa kwa vitendo vya wizi na kushindwa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Wakijadili taarifa za Kamati za Hesabu za Mashirika ya Umma, Serikali za Mitaa na Serikali Kuu, wabunge waliwashutumu mawaziri kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao kiasi cha wengine kwenda mbali zaidi kwa kuwatuhumu kuwa mawaziri wengi ni wezi na kwamba, wamekuwa wakijali maslahi binafsi kuliko ya wananchi wanaowaongoza.
Mawaziri waliokuwa wakishutumiwa na kutakiwa kuachia ngazi ni Mustafa Mkullo (Fedha), Dk. Cyril Chami (Viwanda na Biashara), George Mkuchika (TAMISEMI), Omar Nundu (Uchukuzi), ambapo wabunge waliwataka kuachia ngazi.
Kutokana na tuhuma hizo, Zitto Kabwe (Kigoma Kaskazini-CHADEMA), alitoa pendekezo la kuwataka wabunge 70 kusaini ili kuwasilisha hoja ya kutokuwa na imani na waziri mkuu.
Habari zilizopatikana bungeni jana zimesema wabunge 62 kati 70 wanaotakiwa, wamesaini pendekezo hilo huku wanne wakitoka CCM na mbunge pekee wa UDP, John Cheyo ndiyo hajasaini.
Wakizungumza na waandishi wa habari jana, Zitto na Deo Filikunjombe (Ludewa-CCM), ambao ndiyo wanaratibu shughuli hiyo, walisema tatizo kubwa la wabunge si Waziri Mkuu Pinda bali mawaziri wasio waaminifu.
Zitto alisema tayari kazi ya kukusanya saini inaendelea na wana imani hadi kufikia leo jioni wangekuwa wamekamilisha idadi ya 70 kama kanuni inavyosema.
Amesema wabunge wa vyama vyote wamesaini ispokuwa UDP na kwamba, uongozi wa CUF umetoa maelekezo maalumu kwa wabunge wake kusaini.
Alisema miongoni mwa wabunge waliosaini wanne wanatoka CCM na kwamba, hoja hiyo ni ya wabunge wote bila kujali itikadi za vyama na lengo ni kutengeneza Bunge la utendaji badala ya kulalamika.
Iwapo hoja hiyo itapitishwa na Bunge, Pinda atakuwa Waziri Mkuu wa kwanza kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye.
Zitto amesema kuwa wanatarajia kuwasilisha hoja hiyo kwa Spika wa Bunge, Jumatatu kwa ajili ya hatua zaidi.
No comments:
Post a Comment