TASWIRA ZA NDEGE YA ATC ILIYOPATA AJALI KIGOMA LEO
Ndege
ya Shirika la Ndege Tanzania (ATC), aina ya Dash 8-300 iliyokuwa
inatoka Kigoma kwenda Dar es Salaam kupitia Tabora, ikiwa imeanguka jana
baada ya kuteleza kutokana na tope jingi kuwepo kwenye njia ya kurukia
ya Uwanja wa Ndege wa Kigoma. Abiria 35 na wafanyakazi wanne
walinusurika kwenye ajali hiyo
Wananchi
wakiangalia ajali ya ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATC), aina ya
Dash 8-300 iliyokuwa inatoka Kigoma kwenda Dar es Salaam kupitia Tabora,
ikiwa imeanguka jana baada ya kuteleza kutokana na tope jingi kuwepo
kwenye njia ya kurukia ya Uwanja wa Ndege wa Kigoma. Abiria 35 na
wafanyakazi wanne walinusurika kwenye ajali hiyo.
Hali ya ndege inavyoonekana upande wa kushoto.
Hali ilivyokuwa inaonekana ndani ya
ndege baada ya ajali kutokea jana katika Uwanja wa Ndege wa Kigoma.Picha
kwa hisani ya Full Shangwe Blogu
Uzinduzi wa Miss Tabata 2012 wafana vilivyo
Warembo
wa wanaoshiriki shindano la kumsakama Malkia wa Tabata 2012 wakipozi
mbele ya mashabiki wa burudani ya urembo jijini Dar es Salaam
waliohudhuria uzinduzi wa shindano hilo la Urembo katika Ukumbi wa Dar
West Park Tabata jana. Picha Zote na Father Kidevu Blog
Warembo wakicheza Show maalum ya utambulisho wao. Goma la Don’t Take My Number ndo liliwaongoza.
Warembo
wa wanaoshiriki shindano la kumsakama Malkia wa Tabata 2012 wakipozi
mbele ya mashabiki wa burudani ya urembo jijini Dar es Salaam
waliohudhuria uzinduzi wa shindano hilo la Urembo katika Ukumbi wa Dar
West Park Tabata jana.
Washiriki wa Shindano la Miss Ukonga 2012 ndio waliowasindikiza majirani zao wa Tabata.
Mpiga drams wa Twanga Pepeta Martin Kibosho akifanya vitu vyake jukwaani.
Mwimbaji mkongwe asiyechoka wala kuzeeka, Mumin Mwijuma akikamua na kundi lake la Twanga Pepeta.
Wanenguaji wa Bendi ya Twanga Pepeta wakishambulia Jukwaa vilivyo.
Jopo
la waandaaaji wa Shindano la Miss Chan'gombe walikuwepo kuangalia
vitisho vya Miss Tabata 2011. Kushoto ni Mmoja wa washiriki wa Miss
Chang'ombe ambaye hakika ni fimbo ya ukweli.
Mwana dada Aisha Ramadhani "Aisha Mashauzi" aliwashika vilivyo na walikatika nyonga ile mbaya kwa taarabu yake kali.
Wadau
mbalimbali wa Burudani na Urembo walihudhuria katika uzinduzi huo
ulioenda sambamba na Show kali kutoka kwao Twanga Pepeta “Kisima cha
Burudani” na Mashauzi Clasic Modern Taarab kutoka kwake Mtoto wa Kikurya
Aisha Ramadhani ‘Mashauzi’. Picha na Father Kidevu Blog
No comments:
Post a Comment