TAASISI YA WANAFUNZI WANAOSOMA SHAHADA YA KWANZA YA SOSHOLOJIA YA CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOMSSO) YAPATA VIONGOZI WAPYA LEO MCHANA
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Kutoka
Mwaka wa 1 alipokua akitoa maelekezo ya nini kifanyike kabla ya Zoezi
la Kupiga kura na Kutangaza washindi
Mgombea wa Nafasi ya Mwenyekiti
katika taasisi ya wanafunzi wanaosoma Shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya
Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOMSSO) Bw Edgar Kelvin ambaye anasomma mwaka
wa 2 alipokua akinadi sera zake kabla zoezi la kupiga alijaanza
Mgombea wa pili wa nafasi ya
Mwenyekiti katika taasisi ya Wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya
Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOMSSO) Bi Loyce Haule ambaye
anasoma mwaka wa 2 akinadi Sera zake
Mgombea wa Tatu wa Nafasi ya
Mwenyekiti katika taasisi ya Wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya
Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOMSSO) Bw Mwakindaga Emmanuel
ambaye anasoma mwaka wa 2 akinadi sera zake
Mgombea Wa Nafasi ya Makamu
Mwenyekiti katika taasisi ya Wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya
Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOMSSO) Bw Mtono Juma ambaye
amepita bila kupingwa kutoka na kuwa mgombea pekee wa nafasi hiyo na ni
mwanafunzi kutoka mwaka wa kwanza
Mmoja wa Wanafunzi Kutoka Mwaka wa 3
Sophia Mkingiye akiuliza Maswala mara baada ya Wagombea kumaliza kunadi
sera wakati walipokua wakiomba kura kwa wajumbe na wanachama
Mwanafunzi wa Mwaka wa 2 ambaye
anasoma shahada ya kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma Bi
Hadija Hassan alipokua akiuliza swali wakati kwa wagombea wa nafasi ya
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanafunzi wanaosoma shahada ya Kwanza ya
Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma Wakati Wa Uchaguzi wa Kuwachagua
Viongozi wapya wa Nafasi mbalimbali Katika Taasisi hiyo Mchana wa Leo
Baadhi ya wanafunzi wanaosoma Shahada
ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma waliohudhuria katika
uchaguzi wa kuchagua viongozi wa taasisi ya Wanafunzi wanaosoma Shahada
ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOMSSO) katika
uchaguzi uliofanyika ndani ya Chuo Kikuu Cha Dodoma mchana wa leo
Zoezi la Kuesabu kura likiendelea hapo
Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Bw
Emmanuel Misungwi Alipokua akitoa Shukrani wa wanachama na wadau wa
taasisi hiyo Kwa Kipindi Chote alichokua madarakani kwa mazuri na mabaya
ambayo taasisi imepitia na kushukuru kwa wanachama kushiriki zoezi la
kupiga kura na kupata viongozi wapya wa Taasisi ya Wanafunzi wanaosoma
Shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOMSSO)
Baadhi ya Viongozi wapya wakiwa
katika picha ya pamoja na viongozi waliomaliza muda wao leo mara baada
ya zoezi la kupiga kura kumalizika na hatimaye kuwapata viongozi wa
taasisi ya wanafunzi wanasoma shahada ya kwanza ya Sosholojia ya Chuo
Kikuu Cha Dodoma mchana wa leo
Mwenyekiti
wa Taasisi ya Wanafunzi wanaosoma Shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya
Chuo Kikuu Cha Dodoma aliyemaliza muda wake leo Mh Emmanuel Misungwi
(Katikati) Akiwa katika Picha ya Pamoja na Mwenyekiti mpya wa Taasisi
hiyo Mh Edgar Kelvin (Wa kwanza kulia) na Aliyekuwa Mwenyekiti Wa
UChaguzi Wa Kwanza Kushoto
FINA REVOCATUS AIBUKA KIDEDEA NA KUWA REDD'S MISSS IFM 2012
Washiriki walioingia kwenye tano Bora.
Mshindi wa Redd's Miss IFM 2012,Fina Revocatus (katikati) akiwa na Mshindi wa Pili,Jane Augustino (kushoto) na wa Tatu Theresia Issaya muda mfupi baada ya kumalizika kwa shindano lao hilo lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Hoteli ya Blue Peal,Ubungo Jijini Dar.
Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva,Diamond akifanya vitu vyake wakati wa onyesho hilo la urembo lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Hoteli ya Blue Peal,Ubungo Jijini Dar.
RAIS KIKWETE KUFUNGUA MKUTANO WA AFDB AMBAO UTAGARIMU BILIONI 12
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkutano wa (AFDB) Bw. Ngosha
Magonya katikati akiongea na waandishi wa habari mapema leo jijini
Arusha.
Baadhi ya wanakamati wa kamati ya maandalizi ya mkutano wa AFDBwakiwa katika viwanja vya AICC jijini Arusha leo.
NA GLADNESS MUSHI WA FULLSHANGWE-ARUSHA
Benki ya maendeleo ya
Afrika (AFDB)inatarajia kutumia kiasi cha Shilingi bilioni 12 katika mkutano
wake unaoanza Jumatatu jijini Arusha na kufunguliwa na Raisi Jakaya Kikwete huku kiasi cha fedha hizo zikitumika kukarabati
Kumbi mbalimbali za jengo la Kimaitaifa la ukumbi wa AICC kwa kuwa baadhi ya
kumbi za jengo hilo zinaonekana kupitwa na wakati kutokana na utandawazi uliopo
kwa sasa ndani ya nchi zilizoendelea
Akizungumza jijini hapa na waandishi wa habari mwenyekiti wa
kamati ya kitaifa ya mkutano wa benki ya AFDB kwa mwaka 2012 Bw Ngosha Magonya ambapo alisema kuwa mkutano huo utakuwa na
faida kubwa sana
Alifafanua kuwa kupitia mkutano huo ambao utaanza Jumatatu ijayo
utakuwa na faida kubwa sana kwa jiji la Arusha kwa kuwa hata kiwango cha uchumi
kitaaimarika sana kwa kuwa wageni mbalimbali kutoka katika maeneo ya nchi
mbalimbali duniani watabadilishana hata uzoefu
“kwa kipindi hiki ambacho kuna mikutano ndani ya jiji la
Arusha tunatarajia kuwepo na utoafuti wa khali ya juu sana hasa katika mchakato
wa uchumi na kwa hali hii pia tunatarajia hata kufanya maendeleo
mbalimbali ikiwemo kufanya marekebisho
kwa jengo la kimataifa la AICC”alisema bw Magonya
Katika hatua nyingine alifafanua kuwa mbali na kuweza kuimarisha
uchumi wa mkoa wa Arusha pia wanatarajia kutumia fursa mbalimbali za
kuhakikisha kuwa wanakutanisha wafanyabiashara mbalimbali huku malengo yakiwa
ni kuendeleza uchumi kwa walengwa.
Pia alifafanua kuwa mbali na kuweza kuwasaidia
wafanyabiashara hao katika michakato ya kukuza uchumi pia benki hiyo ina
mikakati mbalimbali ya kuendeleza barabara ambazo zitaweza kutumika kama njia
ya mawasiliano hapa Tanzania hali ambayo nayo itachangia kwa kiwango kikubwa
sana hata kuimarisha uchumi wa nchi ya Tanzania
Aliongeza kuwa hapo awali benki hiyo ilikuwa imeshajenga
barabara ya Arusha –Namanga kwa sasa ana mpango wa kujenga barabara ya Arusha –
Holile ndani ya Mkoa wa Kilimanjaro hali ambayo itachangia sana maendeleo hasa
ya mawasiliano
Alimalizia kwa kusema kuwa wafanyabiashara hasa wa mkoa wa
Arusha wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanatumia vema fursa za mkutano huo ili
kuweza kuimarisha biashara zao za kila siku.
TAIFA KATIKA TASWIRA:Marais wastaafu wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi (kulia), Benjamin Mkapa (kushoto), Rais mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume (katikati) sambamba na marais wengine wakiwasili kwenye Viwanja vya Chuo Kikuu cha Witwatersrand, Johannesburg, Afrika Kusini
Marais
wastaafu wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi (kulia), Benjamin Mkapa
(kushoto), Rais mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume (katikati)
sambamba na marais wengine wakiwasili kwenye Viwanja vya Chuo Kikuu cha
Witwatersrand, Johannesburg, Afrika Kusini kwa ajili ya kuhudhuria
Mkutano wa kujadili maendeleo ya matumizi ya nishati, Karne ya 21 kwa
nchi za Afrika. (Na Mpigapicha Wetu).
No comments:
Post a Comment