Sunday, May 27, 2012

 

 

 

 

MAADHIMISHO YA SIKU YA AFRIKA YAFANA, LONDON-UINGEREZA

 Mheshimiwa Balozi wa Uganda, Mama Joan Rwabyomere, akifungua Maadhimisho ya siku ya Afrika hapa nchini Uingereza, katika sherehe ambazozilifanyika katika Ukumbi wa Hotel ya Lagham Palace, London
Mheshimiwa Balozi wa Botswana, Bwana Roy Blackbeard, akihutubia katika sherehe za kuadhimisha siku ya Afrika
 Kutoka kulia, Dada Rahma Lupatu, Caroline Chipeta, Bwana David Nginila, Bwana Kiondo (maafisa wa Ubalozi wa Tanzania, London) na Dada Jestina George, maarufu kama Queen wa Blog hapa Uingereza.
 Mabalozi ,Maafisa wa Ubalozi na wawakilishi kutoka nchi mbalimbali za Afrika na wageni waalikwa katika sherehe hizo.
 Dada Jestina George na dada Rahma Lupatu, wakijivunia Utanzania wao katika sherehe hizo za siku ya Afrika
 Kikundi cha ngoma kutoka Ghana, wakitoa burudani katika sherehe za kuadhimisha siku ya Afrika hapa London
Siku ya Afrika iliadhimisha rasmi jana hapa nchini Uingereza kwa kujuisha nchi zote za Afrika zenye Balozi au Wawakilishi wao hapa nchini Uingereza. Katika sherehe hiyo rasmi ya kuadhimishwa kwa Siku ya Afrika, kulitolewa hotuba na Balozi wa Botswana na mbaye ni Mkuu wa Mabalozi wa nchi za Afrika hapa Uingereza, Mheshimiwa Roy Warren Blackbeard.

Aidha Mheshimiwa
Balozi Roy Blackbeard, alitoa salamu maalum kutoka kwa mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa nchi za Afrika, Mheshimiwa Yayi Boni, ambaye pia ni Raisi wa Benin.

Balozi Roy, alielezea changamoto nyingi zinazo tokea Barani Afrika na kwingineko na juhudi maalum zinazofanywa na Jumuiya ya Umoja wa nchi za Afrika kutatua migogoro na matatizo ya mara kwa mara yanayolikumba Bara letu la Afrika.

kabla ya kutolewa hotuba hiyo, Balozi wa Uganda Mheshimiwa Mama
Joan Rwabyomere, alifungua kwa kuwakaribisha Mabalozi, Wawakilishi, Marafiki wa Afrika na Wageni mbalimbali waalikwa na kuwashukuru kwa kufika kwao na kujumuika pamoja na waafrika wote duniani kuadhimisha siku hiyo hapa nchini Uingereza. Amani, Upendo, Ushirikiano na Mshikamano miongoni mwa nchi za Afrika vilihimizwa katika maadhimisho hayo.


WAKUU WA MIKOA NA WILAYA WATEMBELEA CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM) LEO

Baadhi ya Michoro ilichorwa na baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) ambazo leo wamepata nafasi ya kuonyesha kazi zao tofauti na masomo wanayosomea
Baadhi ya wakuu wa Mikoa na Wilaya wakiwasili katika ukumbi wa Chimwaga uliopo Chuo Hapa wakati wa maonyesho ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma yanayoendelea hadi muda huu
 Baadhi ya Wakuu wa Mikoa na Wilaya wakisalimiana na wenyeji wao wakati walipokuja kwenye maonyesho ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma ambapo wanafunzi waliweza kuonyesha uwezo wao tofauti na masomo wanayosomea
Mmoja wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) akitoa maelezo kwa baadhi ya wakuu wa wilaya na mikoa waliokuja Kuona kazi za wanafunzi wa UDOM wakati wanafunzi hao Wakionyesha Uwezo tofauti na Masomo wanayosomea
Wakuu wa Mikoa na Wilaya waliweza pia kupata nafasi ya kutembelea Jengo la Utawala la Chuo Kikuu Cha Dodoma na kufanya ziara ndani ya Chuo Kikuu Cha Dodoma Wakati walipokuja Kuangalia maonyesho ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma yanayoendelea Kufanyika Muda huu katika ukumbi wa Chimwaga uliopo Chuo Kikuu Cha Dodoma
Baadhi ya Wakuu Wa Mikoa na Wilaya walipotembelea Jengo jipya la Utawala la Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) leo
 Naibu Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma Mipango, Utawala na Fedha Prof Shaban Mlacha (Katikati) Akitoa Maelezo kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya waliotembelea Chuo Hapa leo katika Maonyesho yaliyohusisha wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma
 Wakuu wa Mikoa na Wilaya wakiwa katika Picha ya Pamoja Mbele ya Jengo la Utawala Mpya wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) 
 
 
 

ZANZIBAR HALI BADO NI TETE MABOMU YA MACHOZI YAENDELEA KURINDIMA TOKEA JANA JIONI HADI ASUBUHI YA LEO

Hizi ni baadhi ya vurugu zilizotokea jana Mjini Zanzibar huku mabomu ya machozi yakirindima na kuendelea kupigwa na polisi wakati wa vurugu zilizoshababishwa na kundi kubwa la watu kwenda kuvamia kituo cha polisi ili kushinikiza kiongozi wao aliyeshikiliwa na jeshi la polisi aachiwe huru
Picha askari wa kutuliza ghasia akiwa tayari kwa mapambano n awananchi wa zanzibar ambao inasemekana walivamia kituo cha polisi wakiwa na silaha za jadi kama vile rungu na mapanga
Hali tete bado inaendelea asubuhi ya leo mjini zanzibar huku polisi wakiwatawanya wananchi wa zanzibar lakini wananchi hao wanazidi kuongezeka kwa kutaka kiongozi wao kuachiwa huru na polisi ambapo alikamatwa jana na wananchi hao kuvamia kituo cha polisi jana jioni na hatimaye polisi kutumia mabomu ya machozi tokeaa jana jioni hadi asubuhi ya leo
Wananchi wa Zanzibar wakiwa kwenye maandamano wakati wakielekea kituo cha polisi na kabla machozi ya mabomu hayajaanza kulipuliwa na askari.Picha Zote na  Abdulaziz El Shuwehdy

JANA JIONI KUNDI KUBWA LA WATU WANAOLIUNGANISHA KUNDI LIFAHAMIKALO KWA JINA LA UAMSHO,AMBALO LIMEKUWA LIKIUPIGA VITA MUUNGANO WA TANZANIA NA ZANZIBAR,LILIVAMIA KITUO KIKUU CHA POLISI CHA MADEMA KISIWANI HUMO JIONI YA JANA NA KUSABABISHA VURUGU KUBWA,WAKITAKA KUACHILIWA KWA KIONGOZI WAO ALIEKAMATWA JIONI YA JANA KWA KUONGOZA MHADHARA BILA YA KUWA NA KIBALI CHA SERIKALI.
HALI HIYO IMESABABISHA VURUGU KUBWA KITUONI HAPO HUKU ASKARI POLISI WA KITUO HICHO WAKILAZIMIKA KUTUMIA MABOMU YA MACHOZI ILI KUWATAWANYA WATU HAO AMBAO WENGI WAO WAKO NA SILAHA ZA JADI AMBAZO NI MARUNGU,MAPANGA NA MAWE ILI KUPAMBANA NA ASKARI POLISI KITUONI HAPO VURUGU HIZO ZIMEENDELEA TENA ASUBUHI YA LEO.
 

No comments:

Post a Comment