Monday, April 2, 2012

WANAUDOM CHAMBER WATOA ZAWADI YA PASAKA KWA KITUO CHA WATOTO YATIMA CHA MIYUJI KILICHOPO MJINI DODOMA JANA

 Hii ni moja ya Picha Kubwa iliyochorwa katika ukuta wa bweni ambalo wanalala watoto wa kituo cha Miyuji kilichopo katika Eneo la Miyuji Mkoani Dodoma.Kituo kinachoendeshwa na Kusimamiwa na Kanisa Katoliki
Mbuzi huyo alikua ni Moja ya Zawadi ya Pasaka kutoka kwa wanafunzi wa UDOM waliyopelekewa Watoto Waishio katika Mazingira magumu katika Kituo Cha Kulelea Watoto cha Miyuji kinachosimamiwa na Kanisa Katoliki kilichopo Miyuji Mkoani Dodoma
Wanafunzi wa UDOM wakiwa wamewasili katika Kituo Cha Watoto Cha Miyuji na Kiroba Cha  sabuni ya Unga kama Moja ya Zawadi walizowapelekea watoto hao wakati walipotembelea kituo hiko cha miyuji kilichopo Maeneo ya Miyuji Mkoani Dodoma....Zawadi nyingine tulizoenda nazo ni pamoja na mbui kwa ajiri ya kitoweo cha pasaka,chumvi,mafuta ya kupikia na unga kilo hamsini>>>
Watoto waishio Katika kituo Cha Kulelea watoto Cha Miyuji Wakiwa wamekusanyika mara baada ya Wanafunzi wa UDOM  chamber kuwasili katika Kituo hiko kilichopo maeneo ya Miyuji Mkoani Dodoma hapo Jana
Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) wakiwa pamoja na watoto waishio kituoni hapo katika moja ya Mashamba ya machungwa yaliyopo kituoni hapo wakti wanafunzi wa UDOM walipokwenda kuwatembelea Watoto hao hapo jana..watoto pamoja na walezi wao hujishughlisha na ulimaji wa mbogamboga na pia pia hufuga mifugo mbali mbali kama ng'ombe na mbuzi kwa ajiri ya kitoweo...pia wana mashamba ya mahindi ambayo huwasaidia kwa chakula
Picha Juu Ni wanafunzi wa UDOM  ambao ni wana UC wakishiriki kuimba na kucheza  pamoja na Watoto hao katika kituo hilo ambapo wanafunzi wa UDOM walienda kuwatembelea watoto hao jana na kucheza nao baadhi ya michezo
 
Tulipata picha ya pamoja na watoto wanaoishi katika kituo hicho cha nyumba ya matumaini miyuji jana...(picha zote na Faddy Gaib Linga)

No comments:

Post a Comment