Friday, March 30, 2012

 

 

 

 

 

Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad Ajionea Uvamizi Unaofanywa Nje ya Uzio Wa Uwanja wa Amaan Zanzibar

 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na baadhi ya watendaji wa Wizara ya Habari, Wizara na Ardhi, na Vikosi vya SMZ baada ya kukagua uchafuzi wa mazingira katika eneo la uwanja wa Amaan.
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akiangalia uchafuzi wa mazingira nje ya uzio wa uwanja wa Amaan wakati alipofanya ziara ya kutembelea maeneo yaliyovamiwa. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na MBM Dr. Mwinyihaji Makame, na katikati (mwenye suti) ni Waziri wa Maji, Makaazi, Maji na Nishati Mhe. Ali Juma Shamhuna.
 Meneja wa Uwanja wa Amaan Khamis Ali Mzee, akitoa maelezo kuhusiana na uvamizi wa eneo hilo, wakati Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad alipofanya ziara ya kutembelea eneo hilo.
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akiwa katika ziara ya kutembelea maeneo yaliyovamiwa nje ya uzio wa uwanja wa Amaan. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Mhe. Abdallah Mwinyi Khamis na kushoto ni Meneja wa Uwanja wa Amaan Khamis Ali Mzee.
Baadhi ya watendaji wa Wizara ya Habari, Wizara na Ardhi, na Vikosi vya SMZ wakimsikiliza Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad baada ya kukagua uchafuzi wa mazingira katika eneo la uwanja wa Amaan.Picha zote na Salmin Said -Ofisi Ya Makamu wa Kwanza wa Rais Wa Zanzibar
--

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad ameutaka uongozi wa Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati kulipima upya eneo la uwanja wa Amaan ili likabidhiwe uongozi wa uwanja huo kwa ajili ya kuliendeleza.

Hatua hiyo imekuja kufuatia uvamizi unaofanywa nje ya uzio wa eneo hilo ambao pia husababisha uharibifu wa mazingira kwa kuchimbwa mchanga pamoja na kutupwa taka kiholela.

Maalim Seif ametoa agizo hilo baada ya kutembelea maeneo yaliyofanyiwa uvamizi huo na kutaka hatua za haraka zichukuliwe ili kudhiti uharibifu usiendelee.

Ameitaka Wizara hiyo kulipima tena eneo la nje ya uwanja huo lililobakia na kulimikisha kwa Wizara ya Habari, utamaduni, utalii na michezo, ili liweze kutumika kwa shughuli za maendeleo kama ilivyokusudiwa ikiwa ni pamoja na kujenga viwanja vya michezo ya ndani (Indoor games).

Ameusisitiza uongozi wa uwanja wa Amaan kuliwekea udhibiti eneo hilo mara wanakapokabidhiwa nyaraka za umiliki, ili kuepusha uvamizi mwengine usije kujitokeza.

Makamu wa Kwanza wa Rais pia amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi kukaa pamoja na watu wanaojishughulisha na upasuaji wa magogo katika eneo hilo, ili kusaidia ulinzi wa eneo linalochimbwa mchanga, sambamba na kuangalia uwezekano wa kubadilisha mfumo wa usafirishaji wa magogo na bidhaa zitokanazo na magogo hayo kwa kutumia usafiri wa magari badala ya ule wa magari ya punda na ng’ombe uliozeleka.

Amesema hatua hiyo itasaidia kudhibiti uchimbaji wa mchanga katika eneo hilo pamoja na kusimamia marufuku ya uingiaji wa wanyama katika eneo la mji.

Katika hatua nyengine Maalim Seif ameutaka uongozi wa uwanja wa Amaan kukaa pamoja na Wizara ya Habari pamoja na ile inayohusiana na vikosi vya SMZ ili kujadiliana juu ya namna ya kutatua tatizo la ulinzi katika uwanja huo, baada ya kubainika kutokuweko maelewano mazuri kati ya taasisi hizo, hali iliyopelekea walinzi wa JKU kuondoka katika eneo hilo.

Awali meneja wa Uwanja wa Amaan bw. Khamis Ali Mzee amebainisha kuwa walinzi wa JKU waliondoka baada ya kuwalalamikia kwa kutotekeleza majukumu yao ipasavyo.

Nae Mkuu wa Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) Kanal Sudi Haji Khatib amesema walilazimika kuwaondosha askari wao katika eneo hilo baada ya kukosa mashirikiano mazuri kutoka kwa uongozi wa Uwanja wa Amaan.

Waziri wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati Mhe. Ali Juma Shamhuna kwa upande wake ameahidi kulishughulikia suala la upimaji wa eneo hilo ndani ya kipindi cha mwezi mmoja na kuchukua hatua zinazostahiki.

Meneja wa Uwanja wa Amaan Bw. Khamis Ali Mzee alidai kuwa sehemu ya eneo linalolalamikiwa aliwahi kupewa mtu kwa ajili ya kuliendeleza lakini ameshindwa kufanya hivyo na kusababisha kuwa sehemu ya kutupia taka (jaa).

Amesema kwa vile uongozi wa uwanja umeshapata muwekezaji atakayeiendeleza hoteli ya uwanjani kuwa na hadhi ya “nyota nne hadi tano”, ni vyema eneo hilo likabidhiwe kwa uongozi wa uwanja huo ili liweze kuwekwa katika hali nzuri, sambamba na kulinda hadhi ya hoteli hiyo.
 
Na 
  Hassan Hamad 
Ofisi Ya Makamu Wa Kwanza Wa Rais Zanzibar
 
 
 
 
 
 

Waziri Terezya akutana na Balozi wa EU

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt Terezya Huvisa akizunumza na  Balozi Mpya wa Umoja wa Ulaya Nchini Tanzania  Bw Filiberto Ceriani Sebregondi alipokwenda kujitambulasha kwa waziri,leo Mtaa wa  Luthuli Mjini Dar es Salaam.

 

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AKUTANA NA MABALOZI WA VATICAN NA UHOLANZI NCHINI


 Waziri Mkuu,Mizengo Pinda  akizungumza na Balozi wa  Uholanzi nchini, Dk. AD Koekkoek ofisini kwake jijini Dar es salaam Machi 30, 2012.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimianana Balozi wa Vatican nchini, Montecillo Padilla kabla ya mazungumzo, ofisini kwake jijini Dar es salaam Machi 30,2012.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Balozi wa Vatican chini, Montecillo Padilla, ofisini kwake jijini Dar es salaam Machi 30,2012.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

 

No comments:

Post a Comment