KIJANA SHABANI ISSA APATIWA MATIBABU NA SASA ANAENDELEA VIZURI.SHUKRANI KWA WOTE WALIOSAIDIA KATIKA HILI.MUNGU AWAZIDISHIE PALE MLIPOTOA
Mnamo Tarehe 15 Mwezi wa 3 2012 Blogu ya Lukaza iliwahi kupost habari ya Kijana Shabani Issa ya kuomba msaada wa Kwenda kupata Matibabu kutokana na hali yake ya Jicho kuwa na Uvimbe hivi sasa Kijana Shabani Issa anaendelea Vizuri baada ya Kupata matibabu katika Hospitali ya St Benedict Ndanda iliyopo Mkoani Mtwara.Kwa habari ya Kwanza ya Kijana Issa Kuomba Msaada BOFYA HAPA
Kijana Shabani Issa Akiwa katika Hospitali ya St Benedict iliyopo Mkoani Mtwara baada ya kufanyiwa upasuaji.
Shabani Issa afanyiwa upasuaji jana(27/3/2012)
St.Benedict's hospital Ndanda mkoani Mtwara.Anaendelea vizuri mpaka
sasa.Namshukuru yeye aliyesimamisha mbingu bila kuweka nguzo kwa mema
yake yote ktk shida ya kijana huyu.Nawashukuru wadau walioweza kuchangia
kwa namna moja au nyingine.Najua wengine walijua ni uongo natafuta
namna ya kuneemesha tumbo na wao nawashukuru pia.Naishukuru hospital ya
Ndanda hasa dr.Mathew Ng'onye na Z.A Umbaro kwa jitihada zao ktk
kufanikisha upsuaji salama.Mungu awabariki sana
Mtandao Wa
Lukaza Blog Unapenda Kutoa shukrani Kwa Wadau Wote Waliowezesha Kijana
Huyu Kupatiwa Msaada wa Kupata Matibabu Katika Hospitali ya Mtakatifu
Benedict iliyopo Mtwara Mungu Awazidishie pale mlipotoa Kwa Kujali na
Kuonyesha Upendo.
NAFASI KWA WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA TANO MWAKA 2012
|
Majina ya wanafunzi waliochaguliwa kuingia kidato cha tano na
Chuo cha Usimamizi wa Maji kwa mwaka 2012 yametangazwa na Kamishna wa
Elimu ya Sekondari. Pamoja na majina hayo, ripoti pamoja na uchambuzi
wa matokeo ya mitihani ya kidato cha nne kwa mwaka 2011 imetolewa.



TANZANIA YASHIRIKI VYEMA KWENYE MAONESHO YA UTALII YALIYOFANYIKA NCHINI UJERUMANI

Hawa
ni washindi wa mashindano ya watu wenye mustachi yaandi ndeve ndefu
zaidi duniani kama wanavyoonekana walipotembelea banda la Tanzania.

Banda la TTB lilivyokuwa likionekana wakati wa maonesho haya
Bodi
ua Utalii Tanzania iliratibu vyema maonesho ya utalii yaliyofanyika
nchini ujerumani katika jiji la Berlin kuanzia tarehe 7 – 11 Machi
2012.
Maonesho ya ITB ndio maonesho makubwa duniani yanayowakutanisha wafanya biashara za utalii duniani.
Katika maonesho haya Bodi ya Utalii iliwaza vyema
kutengeneza utalii ambao ni hazina kubwa kwa nchi ya Tanzania.Picha na
Habari Kwa Hisani ya Father Kidevu Blogu
No comments:
Post a Comment