WAZIRI MKUU ALIPOFUNGUA CHUO CHA VETA KONGOWE
RAIS JAKAYA KIKWETE AZINDUA MRADI WA MAJI PAWAGA, UMEGHARAMIWA NA KANISA LA ANGLICAN KWA ZAIDI YA BILIONI MBILI

TASWIRA ZA RAISI KIKWETE ALIPOWASILI MKOANI IRINGA KUFUNGA WIKI YA MAJI KITAIFA

Rais
Kikwete akiwapungia mkono watu mbalimbali wakiwemo viongozi mbalimbali
wa Serikali mkoa wa Iringa (hawapo pichani) waliofika kumpokea mara
baada ya kuwasili leo mchana kwenye uwanja wa ndege wa Nduli.Rais
Kikwete amewasili leo kwa ajili ya kufunga maadhimisho ya wiki ya maji
Kitaifa iyanayofanyika katika uwanja wa Samora mkoani Iringa
Rais Kikwete akivalishwa skafu na vijana wa skauti,shoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dr Christina Ishengoma
Rais Kikwete akisalimiana na viongozi wa kamati na Ulinzi
Rais
Kikwete akisalimiana na Kamanda wa UVCCM mkoa wa Iringa ambaye pia ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya ASAS, Salim ‘Asas’ Abri muda mfupi
baada ya kuwasili mjini Iringa.
Rais Jakaya Kikwete Ameteua Makatibu Tawala wa Mikoa Saba na Kufanya Uhamisho wa Wengine Watatu
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete,
leo, Jumatano, Machi 21, 2012 ameteua Makatibu Tawala wa Mikoa saba na
kufanya uhamisho wa wengine watatu.Ifuatayo chini ni taarifa kamili
iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y.Sefue ikitangaza
uteuzi huo:-
A: MAKATIBU TAWALA WA MIKOA
(i) Dkt. Faisal Hassan Haji ISSA, ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa KILIMANJARO. Kabla ya hapo Dkt. Faisal alikuwa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Rasilimali Watu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
(ii) Bibi Mariam Amri MTUNGUJA, ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa MBEYA. Kabla ya hapo Bibi Mtunguja alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea.
(iii) Bwana Eliya Mtinangi NTANDU, ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa MOROGORO. Kabla ya hapo Bwana Ntandu alikuwaKatibu Tawala Msaidizi, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Dar es Salaam.
(iv) Bwana Severine Bimbona Marco KAHITWA, ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa GEITA. Kabla ya hapo Bwana Kahitwa alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Uchambuzi wa Sera, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Dodoma.
(v) Eng. Emmanuel N.M. KALOBELO, ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa KATAVI. Kabla ya hapo Eng. Kalobelo alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmasharui ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi.
(vi) Bwana Hassan Mpapi BENDEYEKO, ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa RUVUMA. Kabla ya hapo Bwana Bendeyeko alikuwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro.
(vii) Dkt. Anselem Herbert Shauri TARIMO, ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa SHINYANGA. Kabla ya hapo Dkt. Tarimo alikuwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma.Uteuzi huu unaanzia tarehe 21 Machi, 2012. Wataapishwa Ikulu, Jumamosi tarehe 24 Machi, 2012 saa nne asubuhi.

B: UHAMISHO
(i) Bibi Mgeni BARUANI – Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro
anahamishiwa Mkoa wa NJOMBE.
(ii) Bibi Mwamvua A. JILUMBI – Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga
anahamishiwa Mkoa wa SIMIYU.
(iii) Bibi Bertha O. SWAI, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya anahamishiwa
Mkoa wa PWANI.
Balozi Ombeni Y. Sefue
KATIBU MKUU KIONGOZI
IKULU,
MWANDISHI MWANAMKE ASHINDA KUONJA LADHA BIA ZA TBL MWANZA
Mshindi
wa tatu wa shindano la kuonja na kutambua ladha ya bia za Kampuni ya
Bia Tanzania (TBL), ambalo liliwashirikisha baadhi waandishi wa habari
Mkoa wa Mwanza, Emmanuel Chacha (kulia) wa ITV na Redio One, akipokea
zawadi yake kwa furaha kutoka kwa Meneja wa kiwanda cha bia, TBL,
Mwanza, Richmond Robert mwishoni mwa wiki.
Mwandishi
wa habari wa Kampuni ya Business Times Ltd, Mwanza Jovin Mihambi
akikabidhiwa zawadi ya ushindi wa pili na Meneja wa kiwanda cha bia (TBL
) Mwanza Richomnd Robert, katika shindano la kuonja na kutambua ladha
ya bia.
Emmanuel Chacha wa ITV/ Redio Oneakifanya vitu vyake kwenye shindano la kuonja bia na kutambua ladha ya aina ya bia
Waandishi
wa habari Mkoa wa Mwanza, wakishindana kuonja na kutambua ladha ya bia
mwishoni mwa wiki katika Kiwanda cha Bia cha Kampuni ya Bia Tanzania
(TBL) cha Mwanza. Kutoka kulia ni Emmanuel Chacha wa ITV/ Redio One ,
Hellen Kabambo wa gazeti la Changamoto.
Waandishi
wa habari wakimsikiliza Afisa Ubora wa Bia( TBL ) Jeremiah Kmammbi
kuhusu bia inavyohifadhiwa .Waandishi walitembelea kiwanda hicho cha bia
mwanza kabla ya kushiriki shindano la kuonja bia na kutambua ladha ya
aina ya bia.
Waandishi
walioshinda shindano la kuonja na kutambua ladha ya bia wakiwa katika
picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa zawadi zao. Kutoka kushoto ni
Meneja wa kiwanda cha Bia (TBL) Mwanza, Richomd Robert,, Jovin Mihambi
wa Business Times, Jacquline Wanna wa gazeti la Kasi Mpya amnbaye
alishika nafasi ya kwanza sawa na Henry Kavirondo , Emmanuel Chacha wa
ITV na Redio One (katikatia), mshindi wa kwanza Henry Kavirondo wa
Chanel Ten na Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa TBL, Editha Mushi.
No comments:
Post a Comment