Monday, March 26, 2012

MNYAMA AIBUKA KIDEDEA KWA MAGOLI 2 KWA BILA DHIDI YA ES SETIF

Mchezaji Emanuel Okwi wa Simba akiruka juu juu kuupiga kwa kichwa mpira katikati ya mabeki wa timu ya Es Setif katika mchezo wa Kombe la Shirikisho unaofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam jioni hii, Mpira umekwisha Simba imeshinda magoli mawili yaliyofungwa na wachezaji Emmanuel Okwi goli la kwanza na Haruna Moshi "Boban" goli la pili. Mashabiki wa Simba wanashangilia kwelikweli huku na baada ya Simba kufunga magoli mwashabiki wa Yanga walianza kuondoka uwanjani kabla ya mpira kuisha ni kazi kwelikweli.
 Mchezaji wa timu ya Simba Emmanuel Okwi akiruka juu juu katikati ya mabeki  watimu ya ES Setif wakati timu hizo zilipopambana katika kombe la Shirikisho kwenye uwanja wa Taifa leo.
Mchezaji wa Simba Amir Maftaha akikabana na mchezaji wa timu ya ES Setif ya Algeria katika mchezo wa kombe la Shirikisho.Picha Kwa Hisani ya http://mamapipiro.blogspot.com/
 
 
 
 

Rais Jakaya Kikwete akimwapisha Mariam Mtunguja (kulia) kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya

Rais Jakaya Kikwete akimwapisha Mariam Mtunguja (kulia) kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya katika hafla iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam. (Picha na Fadhili Akida).

Balozi wa Ireland atembelea Kiwanda cha bia cha Serengeti (SBL)

Balozi wa Ireland nchini Tanzania Mhe. Loscan Fullan (wapili kulia) Meneja wa Fedha na Biashara wa SBL, John Collins, Brewery Manager wa SBL Colman Hanna, Meneja Mawasiliano wa SBL, Imani Lwinga na Meneja wa Ubora wa SBL, Alloyce Nduka wakionja bia za SBL wakati wa ziara hiyo ya Balozi.
Balozi wa Ireland nchini Tanzania Mhe. Loscan Fullan (kushoto) akitembezwa katika kiwanda na Meneja wa Fedha na Biashara wa SBL, John Collins (kulia) na Brewery Manager wa SBL Colman Hanna.
Balozi wa Ireland nchini Tanzania Mhe. Loscan Fullan (katuikati) akimsikiliza Brewery Manager wa SBL Colman Hanna juu ya hatua mbalimbali za uzalishaji bia SBL. Kulia ni Meneja wa Fedha na Biashara wa SBL, John Collins.
Balozi wa Ireland nchini Tanzania Mhe. Loscan Fullan (kushoto) akitoka baada ya kumaliza ziara hiyo kiwandani hapo. Pamoja nae ni Brewery Manager wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Colman Hanna na Meneja wa Fedha na Biashara wa SBL, John Collins anaeonekana kwa nyuma.

No comments:

Post a Comment