Friday, February 17, 2012

 

 

UJUMBE WETU WA LEO

BASI LA ABOOD LAPATA AJALI ASUBUHI YA LEO MAENEO YA MBEZI

Basi la kampuni ya Abood likiwa limepinduka maeneo ya Mbezi likiwa linatoka Mkoani Morogoro kuelekea Dar es salaam asubuhi ya leo.Chanzo cha ajali hii hakikujulikana ila inasemekana ni kutokana na dereve kuovertake gari mbele na hatimaye kumshinda na kupinduka.
Wananchi wakitazama jinsi basi la abood lilivyopinduka huku wengine wakiokoa abiria waliopo kwenye basi hilo asubuhi ya leo


 

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL ATEMBELEA SHUGHULI ZA UCHIMBAJI WA MAKAA YA MAWE RUANDA (W)

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya uchimbaji Makaa ya Mawe, Tancoal, Graeme Robertson, wakati alipotembelea mradi wa Uchimbaji Makaa ya Mawe unaoendelea eneo la Ruanda Wilaya ya Mbinga, wakati akiwa katika ziara yake ya mkoa wa Ruvuma jana.
 Ukifanywa utafiti wa kugundua upatikanaji wa makaa ya mawe kabla ya kuanza uchimbaji.
 Makaa yakichekechwa na kupatikana makaa bora na mabaki kuwekwa mahala maalum palipoandaliwa ili kuepuka uchafuzi wa mazingira.
 Magari yakiwa mgdini chini yakiendelea na kazi ya uchimbaji wa Makaa ya mawe hayo ambayo soko lake kubwa limekuwa ni nje ya nchi kama Zambia, Ghana na kwingineko.
 Mke wa Makamu wa Rais, Mama Asha Bilal (katikati) akiwa na Mke wa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma (kushoto) na Mke wa Mbunge wa Mbinga, wakati walipotembelea shughuli hiyo ya uchimbaji.
Sufianimafoto, naye hakusita kupiga picha ya kumbukumbu mahala hapa muhimu kwenye utajiri mkubwa wa Taifa la Tanzania. 
 

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani laTaifa (NECTA) Dk. Joyce Ndalichako Azungumza Juu Ya Kufutwa Kwa Mitihani Kwa Baadhi Ya Skuli Zanzibar

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) Dk. Joyce Ndalichako, akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar matokeo ya kufutwa kwa mitihani kwa baadi ya Skuli kutokana na kufanya udanganyifu.mkutano huo umefanyika Hoteli ya Bwawani Zanzibar.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) Dk. Joyce Ndalichako, akionesha ripoti ya uchunguzi uliofanywa na Taasisi ya Uchunguzi ya Vyombo vya Usalama kuhusi undanganyifu wa baadi ya miandiko iliotumika katika mitihani ya watahiniwa wa Kidatu cha Nne.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Matihani la Taifa (NECTA) Dk. Joyce Ndalichoka, akionesho karatasi za mitihani ambozo zimekuwa na miandiko zaidi ya mmoja na kufanana maneno ya majawabu.
Mwandishi wa Nipashe Charles Mwakenja, akiuliza swali katika mkutano huo, Baraza lina mpango gani wa kupunguza hiyo adhabu waliotowa kwa Wanafunzi.
Mwalim Haji na Mwalim Hassan wakifuatilia makaratasi ya mitihani ya Watahiniwa wa kidatu cha Nne, yalioletwa na Katibu Mtendaji waBaraza la Mitihani ikiwa ni vielelezo kuonesha hakuna Mwanafunzi alioonewa katika adhabu hiyo.
Viongozi wa Chama cha Walimu Zanzibar , wakiangalia moja ya karatasi za mitihani ambazo zimekutwa na makosa na kufutiwa watahiniwa wake, wakiwa katika ukumbi wa hoteli ya bwawani.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Dk Joyce Ndalichoka, akitowa maelezo ya kufutiwa mitihani watahiniwa wa kidatu cha Nne, wa mwaka 2011.
 
 
 No comments:

Post a Comment