TASWIRA ZA ZAMBIA WALIVYOPOKELEWA
Mwandishi
wa BBC anasema mashabiki waliokuwa wakisubiri, walilipuka kwa kelele za
shangwe, wakati nahodha Christopher Katongo alipotoka kwenye ndege
akiwa amelibeba Kombe la dhahabu la Mataifa ya Afrika.
NBC YANUNUA HISA ASILIMIA 10.87 KWENYE KAMPUNI YA MIKOPO YA NYUMBA, TMRC



Benki ya
Taifa ya Biashara (NBC) leo imekabidhi hundi yenye thamani ya Shilingi
bilioni moja kwa Kampuni mahususi ya Kutafuta Fedha na Kutoa Mikopo ya
Muda Mrefu ya Nyumba iitwayo Tanzania Mortgage Refinance Corporation
(TMRC) ikiwa ni kiasi cha kununua hisa za asilimia 10.87 kwenye
kampuni hiyo. TMRC ni taasisi ya kifedha inayomilikiwa na mabenki
mbali mbali kwa lengo la kusaidia mabenki yaweze kutoa mikopo ya muda
mrefu ya nyumba kwa wateja.
Lengo
kuu la TMRC ni kusaidia kutoa fedha kwenye soko la kifedha la
Tanzania kwa ufanisi, na kuzilenga fedha hizo kwa mabenki wanachama
kwa viwango vya ushindani. Hii itawezesha upatikanaji wa makazi kwa
watanzania, na pia kuchangia maendeleo ya masoko ya mitaji.
Shughuli
hiyo imefanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Benki ya NBC, ikiongozwa
na Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Bwana Lawrence Mafuru.
Akizungumza
kwenye tukio hilo, Bwana Mafuru alisema: “Tunaamini kuwa fedha hizi
zitaiaidia TMRC katika juhudi zake za kuwawezesha Watanzania wapate
kumiliki makazi bora. Kitendo hiki kinaonyesha dhamira ya NBC katika kusaidia sekta ya mikopo ya nyumba Tanzania ”
Hundi
hiyo imepokewa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa TMRC, Bwana Rished Bade
mbele ya viongozi wa ngazi ya juu wa kampuni hiyo pamoja na
wawakilishi kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
MISS TANZANIA KUTANGAZA MDHAMINI MPYA WA SHINDANO HILO KESHO

Tarehe
15 Februari 2012 katika ukumbi wa Savannah uliopo katika Jengo la
Benjamin Mkapa saa 5.00 asubuhi, kampuni ya Lino International Agency
inatarajia kufanya Mkutano na Waandishi wa vyombo mbalimbali vya
Habari ili kutangaza mdhamini mkuu mpya wa mashindano ya Miss Tanzania
kwa mwaka huu wa 2012.
Taarifa
iliyotumwa kwa vyombo vya habari hii leo imesema Katika Mkutano huo
atatangazwa Mdhamini Mkuu mpya wa Mashindano hayo ya urembo ya Miss
Tanzania 2012 hivyo kuashiria mbio mpya za kumpata mwakilishi wa Miss
Tanzania katika mashindano ya dunia Miss World.
Mashindano ya
Miss Tanzania yalikuwa yakidhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya
Vodacom kwa muda mrefu mpaka ilipomaliza mkataba wake mwaka jana.
No comments:
Post a Comment