MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AZINDUA JENGO LA UTAWALA LA SHULE YA SEKONDARI MNOLELA, AKAGUA UJENZI WA BWENI LA WASICHANA SEKONDARI YA KINENG’ENE-LINDI
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Lindi mjini, Salum Baruani, wakati
alipowasili kwenye Shule ya Sekondari Mnolela, lindi kwa ajili ya
kuzindua Jengo la Utawala la shule hiyo, jana januari 21, 2012, wakati
akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Lindi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akifurahia ngoma ya asili wakati alipowasili kwenye shule ya
Sekondari ya Mnolela, alipofika kuzindua Jengo la Utawala la shule hiyo,
akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Lindi jana, Januari 21, 2012.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akifunua kitambaa ikiwa ni ishara ya kuweka jiwe la Msingi katika jengo
jipya la Utawala la Shule ya Sekondari Mnolela, iliyopo kijiji cha
Luhokwe, wakati akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Lindi jana Januari
21, 2012.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiongozana na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Lindi, kuelekea kukagua
ujenzi wa jengo la Bweni la wasichana shule ya Sekondari ya Kineng’ene,
akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Lindi, jana Januari 21, 2012.

Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal
na mkewe, Mama Zakhia Bilal, wakifurahia ngoma ya asili baada ya Makamu
kumaliza kuwahutubia wananchi wa Uwanja wa Fisi, mkoani Lindi jana
Januari 21.
Edward Lowassa na Zitto Kabwe

Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa
akisalimiana na Mbunge wa Kigoma Kaskazini(CHADEMA), Zitto Kabwe kwenye
msiba wa Mbunge wa Arumeru na Naibu Waziri wa Fedha Mstaafu Marehemu
Jeremia Sumari jana.Picha na Mdau Richard Mwaikenda
BASI LA NEW FORCE LAUA STENDI YA MABASI MBEYA
ABIRIA
aliyefahamika kwa jina moja la Amina mkazi wa wilaya ya Mbozi mkoani
Mbeya alikufa papo hapo katika ajali iliyotokea juzi usiku katika Kituo
cha Mabasi yaendayo Mikoani kutokea Mbeya baada ya basi la New Force
kuparamia ukuta wa mgahawa uliopo mkabala na Ofisi za Mabasi ya Kampuni
hilo.
Tukio hilo limetokea majira ya
saa 5:00 usiku wa Ijumaa ya Januari 20 mwaka huu katika Kituo hicho cha
Mabasi yakitokea mikoa mingine.
Mashuhuda
wa tukio hilo wamesema kondakta wa basi hilo aliyejulikana kwa jina la
Januari Kapinga aliingia ndani ya basi hilo lenye namba za usajili T 853
AVQ aina ya Yutong lililokuwa likitokea Dar es Salaam baada ya abiria
wote kushuka ndipo alipolikurupua kwa nguvu na kumshinda hatimaye
kuparamia ukuta.
Abiria aliyefariki alikuwa
safarini kuelekea masomoni mkoani Tabora na wakati gari likiparamia
ukuta wa mgahawa huo alikuwa akipata chakula cha jioni
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi imesema licha ya mmoja huyo kupoteza maisha, lakini watano wamejeruhiwa.
Aidha kondakta wa basi hilo
alitoroka na kwenda kusikojulikana na juhudi za Jeshi la Polis kumtafuta
zinaendelea na hadi sasa dereva wa basi hilo anashikiliwa na Polisi kwa
mahojiano zaidi.
Kwa
upande wake Noah Mwakatumbula Mwenyekiti wa Kituo cha Mabasi mkoani
Mbeya yaendayo mikoani amewataka madereva waliopewa dhamana ya kuendesha
vyombo hivyo na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania waache mara
moja tabia ya kuacha funguo za vyombo vyao vya usafiri. Habari hii kwa hisani ya MbeyaYetu.Blog
Lunyamila achoka, amcharukia Papic

Na Saleh Ally
WINGA nyota wa zamani wa Yanga, Edibily Jonas Lunyamila, ameonyesha kuchoshwa na mambo yanavyoendelea ndani ya klabu hiyo hasa maandalizi ya kuwavaa Zamalek ya Misri na kumtaka Kocha Mkuu, Kosta Papic abadili mwelekeo.
Yanga inatarajia kucheza mechi yake ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Februari 17 na 19 dhidi ya Zamalek.
Lunyamila amesema, Yanga wamekuwa wakitumia muda mwingi kwa malumbano huku Papic akionekana kuwa sehemu ya malumbano hayo kila kukicha.
“Sidhani kama ni wakati wa Yanga kulumbana kila siku, kocha (Papic) kila siku anazozana na viongozi. Mara hataki kambi ya Mwanza, mara anahusika na suala la kuwakataa wachezaji fulani.
“Haiwezi kuisaidia Yanga katika kipindi hiki, anatakiwa kufanya kazi zake za kiufundi na kuwajenga wachezaji kisaikolijia. Siku zote malumbano hujenga makundi na hiyo itakuwa ni sumu kwa Yanga,” alisema Lunyamila aliyewahi kuisaidia Yanga kucheza robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 1998.
“Papic ni kocha mwenye uzoefu, atumie muda mwingi na wachezaji wake na ikiwezekana ahusike kuwaambia hali ilivyo ngumu na mwisho wajitolee halafu kama kuna makosa wanaweza kuyarekebisha hapo baadaye.”
Aidha, Lunyamila aliwataka viongozi wa Yanga nao kuangalia uwezekano wa kufanya mambo kitaalamu au kusikiliza ushauri kutoka kwenye benchi lao la ufundi ili kuepusha mabishano.
Pia akasisitiza suala la umakini na kujitolea kwa wachezaji kwa kuwa hata kama kuna ugumu, basi Zamalek inaweza kung’oka kama wakijipanga.
Zaidi kuhusiana na Lunyamila na maandalizi ya Yanga, soma uchambuzi ukurasa wa 12.

UONGOZI wa klabu ya Simba umesema upo katika mazungumzo na kampuni ya Clouds Media Group kwa ajili ya kuingia mkataba wa kuiuza mechi yao ya marudiano dhidi ya Kiyovu kutokana na kuuona mpango huo unafaa.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga, amesema wameona ni vyema na wao wakafanya mpango huo kama walivyofanya watani wao Yanga.
“Mpango uliofanywa na Yanga wa kuikabidhi mechi yao ya Zamalek kwa Clouds Media Group ambayo imeidhamini na kuitangaza ni mzuri sana, hivyo na sisi tumeona ni bora tuingie katika mpango huo ili mechi yetu iweze kutangazika.
“Unajua mpira bila ya promosheni hauwezi kuwa mzuri, hivyo kwa upande wetu tumeliona hilo na tumeamua kulifanyia kazi na kwa sasa tunaendelea na mazungumzo na Clouds Media Group ili iweze kukubaliana nasi kudhamini kwa kuinunua mechi hiyo.
“Litakuwa ni jambo jema kwetu kwani mpango huo utawawezesha watu wengi kuja kuiangalia mechi hiyo kutokana na promosheni itakayofanyika,” alisema Kamwaga.
Aliongeza kuwa wapo katika mikakati madhubuti ya kuhakikisha wanajipanga ipasavyo ili waweze kufanya vizuri katika mchezo huo ambao utakuwa na ushindani wa hali ya juu kutokana na ubora wa timu hiyo.
“Tutaangalia uwezekano wa kucheza mechi moja ya kirafiki ya kimataifa katikati ya ligi na kama itashindikana, tutatumia mechi za ligi kuu kama maandalizi ya mchezo huo,” alisema Kamwaga.
Simba inatarajiwa kuvaana na Kiyovu ya Rwanda kati ya Februari 17 na 19 jijini Kigali katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika na kurudiana kati ya Machi mbili hadi nne jijini Dar es Salaam.
0 comments
MAN U YAITUNGUA ARSENAL GOLI 2 KWA 1 NYUMBANI KWAO


Mchezaji wa Man United Welbeck akifunga bao la pili.
Katika dakika dakika 80 Welback alitingisha wavu tena kwa bao la pili na
kusababisha Man United kutoka kidedea kwa bao 2-1 dhidi ya Arsenal.
Mpira uliendelea kwa kasi, vuta ni kuvute timu zote mbili zilikuwa
zikifanya mashambulizi ya kushinda mchezo huo kwa matumaini ya kutuliza
mpira chini, kwa utulivu na makini, kipindi cha pili dakika 71 mchezaji
wa Arsenal Robin van Persie kusawazisha bao 1-1 katika mchezo huo
uliochezwa leo hii.
Kizaa zaa kiliaza tena pale timu ya Man United kubadilisha mchezo baada ya timu Arsenal kusawazisha bao hilo.
Kizaa zaa kiliaza tena pale timu ya Man United kubadilisha mchezo baada ya timu Arsenal kusawazisha bao hilo.
Mzee Yusuf atoa burudani tosha kwa Watanzania wanaoishi katika jiji la New York City

Mamia
ya Watanzania wanaoishi jijini New York jana jumamosi Jan 21,2012
wamiminika katika ukumbi wa The Portuguese American Club Moun Vernon,
New York kumuunga mkono na kumkaribisha rasmi, muimbaji marufu wa
miondoko ya rusha roho, maarufu kwa jina la Mzee Yusuf ikiwa ni mara
yake ya kwanza muimbaji huyo kuwasili na kutumbuiza jijini hapo. Picha
kwa hisani ya VIJIMAMBO
No comments:
Post a Comment