Thursday, January 26, 2012

26 Waziri Mkuu Mizengo Pinda Afungua Mkutano wa Majadiliano ya Kisera Kuhusu Matumizi ya Umma na Wiki ya Umaskini 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Balozi wa Marrkani nchini, Bw. Alfonso Lenhardt baada ya kufungua Mkutano wa majadiliano ya Kisera kuhusu Matumizi ya Umma na Wiki na Wiki ya Umaskini kwenye ukumbi wa hoteli ya Blue Pearl - Ubungo Plaza jijini Dar es salaam Januari 26,2012.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Waziri wa Fedha,Mustafa Mkulo baada ya kufungua Mkutano wa Majadiliano ya Kisera kuhusu Matumizi ya Umma na Wiki ya Umaskini kwenye ukumbi wa Hoteli ya Blue Pearl- Ubungo Plaza jijini Dar es salaam Januari 26,2012

Makamu Wa Pili Wa Rais Wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Azindua Mpango Wa Mikopo kwa Vijana

Makamu Wa Pili Wa Rais Wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Akimkabidhi Hundi Ya Shilingi Milioni 30,000,000/- Mwenyekiti Wa Zanzibar Vijana Saccos Ndugu Ahmed Baluu
Makamu Wa Pili Wa Rais Wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Akizindua Mpango Wa Mikopo Kwa Vijana Zanzibar Hapo Katika Ukimbi Wa Zamani Wa Baraza La Wawakilishi Kikwajuni Mjini Zanzibar.
----
Ongezeko kubwa la idadi ya watu ambalo haliendi sambamba na kasi ya ukuaji Uchumi limesababisha Serikali na Mashirika yake kushindwa kuajiri idadi ya Vijana wote wanaomaliza Elimu yao ya lazima na ile ya Vyuo Vikuu.

Akizindua Mpango wa Mikopo kwa Vijana Zanzibar Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozoi Seif Ali Iddi alisema Vijana wanalazimika kufahamu sula hili na ni vyema wakajiandaa kukabiliana nalo.

Balozi Seif alisema suala la kupambana na umaskini ni la kila mtu hivyo hapana budi kujituma kwa bidii huku ikizingatia kwamba sekta Binafsi ndie muajiri Mkuu.
Makamu wa Pili wa Rais aliwashauri Vijana popote walipo waamue kujiajiri kwa vile yapo maeneo mengi ya ajira katika sekta za Kilimo, Utalii, Biashara za Wajasiri amali.
Balozi Seif alisisitiza kwamba Serikali inajitahidi kuweka mazingira mazuri ya Sekta Binafsi ili watakaoamua kujiajiri waweze kupata Elimu na Utaalamu kupitia Vyuo vyuo vya Waajasiri amali vilivyopo na vitakavyoanzishwa.

Aliwakumbusha Vijana kujiandaa vizuri na kuwa waaminifu katika kukopa na kurejesha mikopo hiyo kwa wakati ili mfuko wao uwe madhubuti na Vijana wengine waweze kufaidika nao.
“ Sera ya Mpango huu ni ukopeshaji na sio ugawaji wa sadaka ukiwa na lengo la kuwasaidia Vijana wasio na ajira ila wako tayari ”. Alisisitiza Balozi Seif.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliiomba Wizara ya Ustawi wa Jamii, Maendeleo ya Vijana Wanawake na Watoto kuwa makini katika usimamizi na uendeshaji wa mpango huo kwa kuzingatia misingi iliyowekwa.

Balozi Seif alisema Serikali iotaendelea na juhudi za kutafuta Washirika wa Maendeleo wa ndani na nje ili kuiunga mkono katika juhudi zake na kusaidia Mipango yake.
Akizungumzia kuhusu suala la Ukimwi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisisitiza kuchukuliwa kwa kwa hatua madhubuti za kukinga maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi.

Alisema ukimwi bado upon a unaendelea kuathiri maisha ya wtu wengi hasa Vijana na matokeo ake Taifa linapoteza nguvu kazi muhimu kutokana na maradhi hayo yaliyokosa dawa hadi hivi sasa.

Mwakilishi wa Benki ya Maendeleo Vijijini CRDB Tanzania ambae pia ni Meneja Uendeshaji wa Benki hiyo Bwana Samson Kenja alisema bado ipo changa moto kubwa katika utoaji wa huduma za Mikopo kwa Wananchi hasa kundi kubwa la Vijana.

Bwana Kenja amesema Uongozi wa Benki ya CRDB umeahidi kutoa Mafunzo kwa Vijana waliokuwa wameshajikusanya ili kuwajengea uwezo wa kujiwezesha Kiuchumi.
Alisisitiza kwamba mahitaji ya Vijana bado ni makubwa, hivyo Uongozi wa Benki yake utaendelea kujikita katika utoaji wa Mikopo kwa lengo la kuwajengea uwezo Vijana waliojikusanya katika Makundi ya Saccos.

Katika Risala yao iliyosomwa na Aziza Abeid Vijana hao wameipongeza Serikali kwa jitihada zake za kuajengea uwezo Vijana katika mfumo wa Kujiwezesha Kiuchumi na kukabiliana na hali ngumu ya Uchumi.

Vijana hao wametoa wito kwa Vijana wanaopata mikopo kufuata taratibu zilizopo hasa za urejeshaji wa mikopo kwa lengo la kuwpa fursa Vijana wengine kutumia fursa hiyo.
Mapema Waziri wa Ustawi wa Jamii Maendeleo ya Vijana Wanawake na Watoto Mh. Zainab Mohammed ameyapongeza Mashirika,Wahisani na Taasisi tofauti za Ndani na Nje zilizo kubali kusaidia harakati za Vijana katika kujiwezesha Kiuhumi.

Mh. Zainab amesema juhudi hizo zimewezesha kupunguza wimbi la Vijana wasiokuwa na ajira katika maeneo mbli mbali hapa Nchini.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
25/1/2012.

Dina Marios:Women In Balance-Kitchen Party Gala ni 28 january 2012.

Mtayarishaji wa party hiyo na Mtangazaji wa Radio Clouds FM Dina (Kushoto)wakionesha DVD ya kitchen party gala iliyopita ambazo wanatarajia kuzitengeneza kwa wingi na zitaanza kupatikana mapema mwezi ujao,ambapo kila mwezi watakuwa wakirekodi,kwa wale watakaotaka kununua labda alipitwa zitakuwa zikipatikana.
--
Women In Balance-kitchen party Gala
Wasichana na wanawake wengi kwa sasa wanakabiliwa na changamoto nyingi sana ambazo zinapelekea kushindwa kusimama katika mahusiano yao.Teknolojia,mwamko wa elimu,wanawake kumiliki biashara binafsi,kazi,wazazi hawahusishwi ,kila mtu mjuaji ,kujisahau n.k
Matokeo yake talaka nyingi na mahusiano kuvunjika sasa tunataka kumkumbusha mwanamke wajibu wake na nafasi yake katika mahusiano.Ajitambue.
Msimu wa pili
Eneo hili limelenga kukuza ujuzi wa mwanamke katika Nyanja za kijamii zaidi.Kupitia eneo hili mwanamke atajifunza mambo mbalimbali kiasili na kisasa ambayo mwanamke anaengia au aliyeko au anaetegemea kuingia katika mahusiano na ndoa.Mambo kama malezi ya watoto ,nafasi yake katika jamii umuhimu kujiamini na mengineyo.
Wazo hili limekuja mara baada ya kuona kwamba ule muda wanawake wanaopata kuongea mambo haya kwenye kitchen party ni mchache na hautoshi kumfahamisha mwanamke mambo yote muhimu.Mambo ambayo ni lazima ayajue au hata kama anayajua kutokana na pilika pilika za maisha anajisahau.
Tukio hili kufanyika jumamosi hii ya tarehe 28 january 2012.Kuanzia saa nane mchana mpaka saa mbili usiku katika ukumbi wa Danken house uliopo mikocheni kwa warioba.
Watoa mada ni watu wenye uwezo katika swala zima la uelimishaji
Aunt sadaka;Ni mwana saikolojia aliyebobea katika maswala ya wanawake na watoto.Ana uwezo katika Nyanja hii ambao umetokana kielimi na uzoefu wa kukutana na kesi mbalimbali amabazo zinazo mguza mwanamke hivyo kuweza kuwa funzo kwa wengine.
Bi Chau ni mwanamke ambae mbali na kuwa katika fani ya sanaa kwa muda mrefu wamekua wakito amafunzokwa wanawake tokea muda mrefu.Mafunzo ya mahusiano,ndoa na familia kwa ujumla.
Mama Victor;Ni mtumishi wa Mungu katika dini ya kikristo ambae anaelimisha wanawake kwa mafunzo ya kidini.Anafundisha mwanamke kujitambua vile mungu amempa uwezo wa kuitumikia jamii yake kama mlezi na kiongozi.
Kwa ufupi hawa ndio wakufunzi katika tukio letu hili la women in Balance jumamosi hii katika msimu wa pili.
Burudani itatolewa na Nyota Waziri.
Huu ni mkakati wa mwaka mzima huu 2012 na tutakutana kila mwezi mpaka mwezi march ambapo ratiba itabadilika na wanaume kuhusishwa.
WADHAMINI WETU WA SIKU HII NI
BAILEYS (kinywaji),MGen insuarance,cocacola,cooperate image na clouds fm.
IMETOLEWA NA MRATIBU WA WOMEN IN BALANCE
DINA MARIOS.

Mgombea Uwakilishi Katika Uchaguzi Mdogo Jimbo la Uzini(CCM)Mohamed Raza Arejesha Fomu ya Kugombea Uwakilishi Katika Jimbo Hilo

MGOMBEA Uwakilishi katika uchaguzi mdogo jimbo la Uzini kwa Tiketi ya Chama Cha Mapinduzi,Muhamed Raza,akirejesha fomu ya kugombea uwakilishi katika jimbo hilo kwa msimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya ya Kati Mussa Ali Juma, baada ya kukamilisha taratibu za kuijaza fomu hiyo,hafla hiyo ilifanyika ofisi za Tume ya Uchaguzi Koani.

No comments:

Post a Comment