Wednesday, August 8, 2012


KAMPUNI YA STEPS YASHIRIKIANA NA WASANII KUWAKAMATA WEZI WA KAZI ZAO




MSANII MOHAMED NICE 'MTUNISI' AKIZUNGUMZA JINSI WALIVYOKAMATA MZIGO FEKI WA KAZI ZA WASANII MBALIMBALI KWA KUSHIRIKIANA NA KAMPUNI YA STEPS ENTATAINMET YA JIJINI DAR ES SALAAM INAYOSAMBAZA KAZI ZA WASANII NCHINI




MTUHUMIWA WA KURUDUFU KAZI ZA WASANII AKIWA CHINI YA ULINZI BAADA YA KUKAMATWA




MSANII MOHAMED 'NICE' AKILIA KWA UCHUNGU BAADA YA KUKUTA KAZI ZAO ZILIZOKUWA ZIKIUZWA KATIKA MOJA YA DUKA MTAA WA MAGILA NA LIKOMA LEO










Msanii wa filamu nchini Mohamed Nice 'Mtunisi' kushoto na Jacob Stevin 'JB' wakiwa katika duka ambalo lilikuwa linauza kazi zao ambazo ni feki ambapo walikamatwa kwa kushirikiana na Kampuni ya usambazaji ya Steps Entantainment ya jijini Dar es salaam




Moja ya gari lililokuwa limejaa kazi za wasanii mbalimbali nchini zinazouzwa kiholera baada ya kurudufu kinyume na sheria na kukosesha wasanii mapato mazuri.




Baadhi ya watu wakiwa wamezagaa kushudia ukamatwaji wa kazi za wasanii mtaa wa Magili na Likoma Dar es salaam leo.




Baadhi ya wasanii pamoja na askari polisi wakiwa wamelizingira duka lililokuwa linauza kazi feki za wasanii




Gari lenye namba za T 608 BWD lililokamatwa na kazi mbalimbali za wasanii zikiwemo zinazosambazwa na Kampuni ya Steps ya jijini Dar es salaam linalofanya kazi na wasanii hao




BAADHI YA KAZI FEKI ZA WASANII ZILIZOKAMATWA LEO




MSANII MOHAMED NICE 'MTUNISI' KUSHOTO AKITOA MAELEZO MBALIMBALI KWA MAOFISA USALAMA WALIOFIKA KATIKA UKAMATAJI WA KAZI FEKI ZA WASANII








BAADHI YA WANANCHI WAKISHUDIA TUKIO HILO




MSANII KAPTEN RADO AKIKAGUA KAZI ZAKE MPYA AMBAPO KAZI YAKE MPYA IJULIKANAYO KAMA 'HATIHANI' ILIYOINGIA MTAANI LEO ILIKUWA IMESHA CHAKACHULIWA NA KUINGIZWA SOKONI




MSANII WA MZIKI WA TAARABU,MZEE YUSUFU KUSHOTO AKIANGALIA MOJA YA KAZI YAKE ILIYOKUWA FEKI ZILIZOKAMATWA NA WASANII WENYEWE KWA KUSHIRIKIANA NA KAMPUNI YA STEPS ENTANTAINMENT YA JIJINI DAR ES SALAAM.




WASANII MZEE YUSUFU KUSHOTO NA MOHAMED NICE WAKIWA KATIKA DUKA LILILOKAMATWA KWA KUUZA KAZI FEKI ZA WASANII MSAKO HUO ULIWASHIRIKISHA KAMPUNI YA STEPS ENTATAINMENT PAMOJA NA WASANII WENYEWE.




BAADHI YA MIZIGO YA DVD MPYA KABISA ZILIZO FEKI ZIKIWA ZIMEKAMATWA LEO.Picha na.www.burudan.blogsports.com


KAMPUNI ya Steps Entatainment ya jijini Dar es salaam inayosambaza kazi za wasanii kwa kushirikiana na wasanii wamekamata kazi mbalimbali za wasanii hawo zinazorudifiwa kinyume na taratibu na kutofaidika kwa wasanii wanaotoa kazi hizo

Msemaji wa Kampuni ya Steps Kambarage Ignatios amesema kuwa ukamataji huo si wa zimamoto watahakikisha wanashilikiana na wasanii wenyewe kukamata kazi zao mana wasanii wengi wanadai kuwa kazi zao zinatoka sana kumbe zinachakachuliwa na kuwapa faida watu ambao wanakaa tu na kusubili kazi za wasanii ameiomba serekali kuchukua atua kali ili iwe fundisho kwa watu wanaorudufu na kunyonya kazi za wasanii hawo

Na mmoja ya wasanii waliojitokeza katika kamatakamata hiyo iliyofanyika makutano ya mtaa wa Magila na Likoma Kariakoo, Msanii Mohamedi Nice 'Mtunisi' amesema watu hawa wana akili za ziada kwani katika kava ya mbele wanaweka stika yetu halali na dvd ndio inakuwa imechakachuliwa akiangua kilio na kusema wasanii wakifa wanakufa masikini kumbe ni watu wachache ndio wamekuwa wakinufaika na kazi zao bila kushiriki chochote

Baadhi ya wasanii walioshiliki katika kamata kamata hiyo ni pamoja na Jacobo Stevin 'JB' Mzee Yusuph wa kundi la Taarabu la Jahazi Simoni Mwapagata ( Rado) Mussa Msuba wa iliyokuwa Segere Orginal Seles Mapunda ,Mohamed Nice 'Mtunisi' na wengine wengi wasanii hawo wameungana pamoja kwa ajili ya kutetea kazi zao ili zisirudufiwe kiolela na kuiomba serekali kupitisha sheria kali kwa mtu anaekamatwa na kazi kama hizo zilizokamatwa







MASOUD KIPANYA








Naibu Waziri Afrika Mashariki Apata Ajali Kibaha Jioni Hii




Anaitwa Abdullah Juma Abdalla Saddallah na familia yake kupata ajali mbaya eneo la Tumbi Kibaha wakati akitoka Bungeni na familia yake.

Ajali hiyo mbaya ilitokea majira ya jioni hii wakati naibu waziri huyo akitokea Bungeni kuelekea jijini D'salaam akiwa na mkewe pamoja na watoto wake wawili na a dereva wake ambaye aliumia vibaya na kukimbizwa hospital yaTumbi-KibahaMashuhuda wa ajali hiyo akiwemno Abdulaziz Video amedai kuwa chanzo cha ajali hiyo inasemekana alikuwa analikwepa Lori alilokuwa akipishana nalo na hivyo gari lake kuhama njia na kupinduka

Imeelezwa baada ya ajali hiyo umati wa wananchi wakiwemo vibaka walifika eneo hilo kutaka kupora mali mbali mbali ila hawakuweza kufanikiwa baada ya raia wema kusaidia kuepusha hali hiyo .

Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Taifa Mohamed Mpinda alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo baada ya kuhojia na mwandishi wa habari hizi na kuwa hali ya naibu waziri huyo si mbaya sana zaidi ya dereva wake ambaye ameumia kichwani.". Chanzo: Francis Godwinblog.



Maandalizi ya Sensa ya Watu na Makaazi Yanaendelea Vyema Zanzibar



Mwenyekiti Mwenza wa Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa Tanzania Balozi Seif Ali Iddi akipata maelezo kutoka kwa Kamishna wa Sensa Tannzania Hajat Amina Mrisho Said wakati alipofanya ziara fupi kukagua ghala kuu la vifaa vya Sensa liliopo Kibaha kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati hiyo.

Mwenyekiti Mwenza wa Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa Tanzania Makamu wa Piliwa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikiendesha Kikao cha Tano cha Kamati hiyo kilichofanyika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kibaha. Kushoto ya Balozi Seif ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo Zanzbar Mh. Omar Yussuf Mzee na Kulia ni Naibu Waziri wa Fedha wa Muungano Mh. Saada Mkuya.

Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia Idadi ya Watu { UNFPA } Bibi Mariam Khan akiwasailisha salamu za Shirika hilo katika Kikao cha Tano cha Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa Tanzania kilichokutana Ofisi ya Mkuu a Mkoa Kibaha chini ya Mwenyekiti wake Balozi Seif Ali Iddi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.


WAJUMBE TUME YA KATIBA WAENDELEA NA TATHMINI YA KAZI YA KUKUSANYA MAONI



Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Alhaji Said El-Maamry akiongea leo (Jumanne, Agosti 7, 2012) katika mkutano wa Tume unaoendelea unaolenga kufanya tathmini ya kazi ya kukusanya maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya. Mkutano huo unafanyika katika ofisi za Tume jijini Dar es salaam

Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mhe. Raya Suleiman Hamad akiongea leo

Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Alhaji Said El-Maamry akiongea leo

Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Ally Saleh akiongea leo (Jumanne, Agosti 7, 2012) katika mkutano wa Tume unaoendelea unaolenga kufanya tathmini ya kazi ya kukusanya maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya. Mkutano huo unafanyika katika ofisi za Tume jijini Dar es salaam.

Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Humphrey Polepole akiongea

Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Awadh Ali Said akiongea leo

Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Rishard Lyimo akiongea leo


MATUKIO MBALIMBALI KUTOKA BUNGENI DODOMA LEO



MAMA TERRY AKIWA NA MAZUNGUMZO NA MAWAZIRI, WA KWANZA KUSHOTO NI WAZIRI WA UCHUKUZI MHE. HARRISON GEORGE MWAKYEMBE NA NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII MHE. LAZARO SAMUEL NYALANDU KATIKATI BUNGENI MJINI DODOMA.




BAADHI YA WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI YA LA MARIAM GIRLS WAKISIKILIZA KWA MAKINI WAKATI WA MAJADILIANO YA BUNNGE WALIPOPATA NAFASI YA KUINGIA BUNGENI MJINI DODOMA LEO



WAZIRI WA NCHI ,OFISI YA RAIS ,ASIYE NA WIZARA MAALUM ,PROF.MARK JAMES MWANDOSYA AKITOKA NJE YA BUNGE NA KUWA NA MAZUNGUMZO NA MBUNGE DEO FILIKUNJOMBE (CCM) KWENYE VIWANJA VYA BUNGE MJINI DODOMA LEO.



MBUNGE WA VITI MAALUM (CCM MARA) MHE. ESTER BULAYA WATATU KUSHOTO AKIZUNGUMZA NA MAMISS WALIOPITA, WA KWANZA KUSHOTO NI MISS FARAJA KOTA(MRS. NYALANDU), WA PILI NI NANCY SUMARI PAMOJA NA WAFANYAKAZI WA BUNGE KULIA, NJE YA VIWANJA VYA BUNGE MJINI DODDMA LEO



WAZIRI MKUU MSTAAFU WA ZAMANI MHE. EDWARD LOWASSA AKIZUNGUMZA NA MAMISS WALIOPITA, KUSHOTO NI FARAJA KOTA(MRS. NYALANDU) NA NANCY SUMARI WALIPOPATA NAFASI YA KUTEMBELEA BUNGE MJINI DODDMA LEO


WAANDISHI WA HABARI WA VYOMBO VYO HABARI WAKIRIPOTI HABARI ZA BUNGE MJINI DODOMA..PICHA NA ANNA ITENDA – MAELEZO.

No comments:

Post a Comment