Wednesday, August 22, 2012

Amsha amsha ya Tamasha la Fiesta 2012 ndani ya mji wa Tanga

Mkuu wa Vipindi wa Clouds Fm Sebastian Maganga (wa kwanza kulia) akitoa maelekezo kwa watangazaji wa redio hiyo Lovenes Love na Adam Mchomvu wakati walikuwa wakiongea na wasikilizaji wa redio ndani ya Tanga katika amsha amsha ya Tamsaha la Fiesta 2012 linalotegemea kufanyika tarehe 26.8.2012 Uwanja wa Mkwakwani. Tamasha hilo litakalopambwa na msanii maarufu wa kimataifa kutoka nchini Kenya Prezzoo.
Mtangazaji wa Clouds Fm Adam Mchomvu akionyesha t-shirt ambazo zimetoka kwa ajili ya kusherekea tamasha hilo la Fiesta 2012.
Mwanadada Loveness Love akisababisha ndani ya amsha amsha ya tamasha la Fiesta linalofanyika wikend hii ndani ya Tanga.
Mkuu wa Vipindi wa Clouds Fm Sebastian Maganga akiendeleza harakati za kukamata matukio ndani ya kitaa cha Chumbageni, pale Clouds Fm ilipotembelea vijana hao wa maskani na kupata mawili mawili matatu kuhusiana na tamasha hilo.
Mazungumzo ya haopa na pale yakiendelea.
...vijana wakimsikiliza Mkuu wa Vipindi wa Clouds Fm Sebastian Maganga, pembeni yake ni Adamu Mchomvu.
Vijana walipata mzuka wa kufunguka na kuonyesha vipaji vyao.
...Mzuka ulipata na kuanza kuchana.
Mmoja ya maproducer wakali wa msanii Moraka akiongea machache mara baada ya kukutwa akiwa amekaa na vijana wenzake ndani ya maskani ya Chumbagenino.
Moja ya staili niliyokutana nayo.
Picha ya Kumbu kumbu kwa vijana wa Chumbagenino.
Mara baada ya Clouds Fm kutoka Kitaa cha Chumbageni maskani ya Chumbagenino Clouds Fm ilihamia kitaa kingine ambapo alijitokeza kijana mmoja na kuomba awe mtangazaji hapa alikuwa alimfanyia mahojiano Mwanadada Loveness Love.
Aha... Sudi Brown (kushoto) akiwa na Mchomvu.
Ukumbusho Muhimu sana.
Aha...mambo yalinogeshwa na kuwekwa sawa. Unaweza kufuatilia kinachoendelea katika amsha amsha za tamsaha la Fiesta 2012 kupitia Kajunason Blog.

Kamati ya Taasisi 4 za kiraia yaipa serikali siku 7 kuruhusu gazeti la MwanaHalisi Kuchapishwa

Mwnyekiti wa MISA-Tanzania Mohamed Tibanyendera, akizungumza na waandsihi wa habari kuhusu hatua wanazozichukua dhidi ya Serikali kutokana na kulifungia gazeti la MwanaHalisi.
---
Kamati ndogo iliyoundwa na taasisi nne za kiraia nchini ambayo inaratibu kupigania haki ya kufunguliwa kwa gazeti la MwanaHalisi, leo imeipa serikali siku saba kuliruhusu gazeti hilo kuendelea kuchapishwa.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa kamati hiyo Marcossy Albanie, amesema hawana sababu yakwenda mahakamani juu ya jambo hilo kwasababu hata serikali haikutumia njia hiyo ya mahakamani kwani ilikuwepo badala yake wametumia sheria kandamizi ya vyombo vya habari inayopigiwa kelele na wadau wa habari.

Kamati hiyo inayoungwa mkono na taasisi tano za kiraia baadhi ya taasisi hizo ni MISA TANZANIA, TANZANIA HUMANRIGHTS DEFENDERS COALITIONS NA KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU (LHRC) imeitaka serikalikutekeleza madai yafuatayo:-
  1. Kuitaka serikali kulifungulia gazeti la Mwanahalisi maramoja.
  2. Serikali badala ya kushughulikia Watetezi wa haki na wanahabari wanaofichua uovu ishughulike na wahalifu waluiomteka Dkt. Ulimboka.
  3. Serikali iache kabisa na ukandamizaji huu wa haki na uhuru wa habari.

WAANDISHI WA HABARI WAOMBWA YAFUATAYO SERIKALI ISIPOTEKELEZA HAYO:
  1. Kutochapisha habari yoyote itakayo wahusu Waziri wa Habari wa Wizara hiyo na Naibu wake, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo.
  2. Kusimama kidete kuunga mkono harakati hizo hadi zinapata ufumbuzi wake.
Ikumbukwe kesi Na.34/2009 iliyofunguliwa tangu 2008 kupinga sheria ya magazeti ya 1976 iliyotumika kufungia MwanaHalisi haijasikilizwa mpaka sasa.
 
 
 

Wananchi wa shehia ya Kilombero iliyoko Wilaya ya Kaskazini B wameuomba Uongozi wa Jimbo lao, Wilaya na Serikali Kuu kuangalia uwezekano wa kuwapatia huduma ya Umeme

 
   Mwananchiwa Kijiji cha Kilombero Nd. Bakari Mtumwa Silima  akiwasilisha kilio cha Wananchi waKijiji  hicho cha ufinyu wa Huduma yaMaji safi mbele ya Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi hapo Skuli yaKilombero Wilaya ya Kaskazini B.
   NduguBakari Omar wa Shehia ya Kilombero akielezea kadhia inayowapata Watoto waokatika kivuko kinachojaa maji msimu wa masika wakati wanapokwenda kwenye masomoyao.
 Mbunge wa Jimbo la Kitope BaloziSeif Ali Iddi akijibu na kufafanua baadhi ya kero zinazowakabili wananchi waShehia ya Kilombero katika harakati zao za kila siku za maisha.Kulia ya Balozi ni Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini B Nd. Khamis Jabir Makame na Kushoto yake ni Mkewe Mama AshaSuleiman Iddi
Mbunge waJimbo la  Kitope Balozi Seif Ali Iddi akipeana mikono na Wananchi wa Shehia ya Kilombero mara baada ya kupokea kerona matatizo yanayowakabili Wananchi  hao
--
 
Wananchi wa shehia ya Kilombero iliyoko Wilaya ya Kaskazini B  wameuomba Uongozi wa Jimbo lao, Wilaya na Serikali Kuu kuangalia uwezekano wa kuwapatia huduma ya Umeme itakayosaidia kutanzua tatizo la maji linalowakabili kwa muda mrefu sasa.

Ombi hilowamelitoa mbele ya Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi aliyefika Kijijini hapo kusikiliza matatizo na kero zinazowakabili wananchi hao hapo katika  viwanja vya skuli ya Kilombero.

Ndugu Bakari Mtmwa Silima akiwasilisha Kero za Wananchi hao alimueleza Balozi Seif kwamba licha ya juhudi zinazochukuliwa naViongozi wa Jimbo hilo lakini bado  huduma ya Maji safi inaendelea kuwa mtihani kwao.

Nd. Bakari alisema harakati za uchimbwaji wa Kisima cha maji safi kwa ajili ya Wananchi wa Shehia hiyo unaendelea vyema lakini tatizo linalojitokeza ni upatikanaji wa huduma za umeme kufikia eneo hilo.

“ Utaratibu wa kupelekea umeme Kilombero juu  kilipo kisima hicho unafikia masafa ya Kilomita moja. Lakini mbali ya huduma hiyo ya maji pia sisi wananchi tunahitaji huduma hiyo kwa matumizi ya kawaida”. Alisisitiza Ndugu Bakari Mtumwa.

Naye Ndugu Bakari Omar alielezea kilio kinachowapata watoto wa eneo hilo cha ukosefu wa kivuko wakati wanapokwenda skuli hasa wakati wa msimu wa mvua kubwa.

Alisema kivuko kinacholigawa eneo la kitongoji chao naskuli ya Kilombero huzidiwa na maji wakati wa masika na kutishia maisha ya wanafunzi hao wakati wanapotaka kuvuka.

Akijibu hoja za Wananchi hao wa Shehia ya Kilombero , Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi aliwataka Wananchi hao kuendelea kuwa na ustahamilivu na juhudi zitaendelea kufanywa ili kuona huduma ya maji safi inapatikana kwa uhakika katika eneo hilo.

Alisema Uongozi wa Jimbo, Wilaya na Hata Serikali Kuu unaelewa tatizo la usumbufu wa huduma ya maji safi unaowapata Wananchi wa Kilombero.

 “ Ukweli usiofichika kwamba maji ni uhai wa kilakiumbe. Kwa kulifahamu hili mimi binafsi ninaposikia kiliocha maji katikamaeneo maeneo yoyote Nchini huamua kulivalia njuga hadi lifikie ufanisi”.Alisisitiza Balozi Seif.

Balozi Seif aliwahakikishia Wananchi hao kwamba yeyena viongozi wenzake wa Jimbo watafanya jitihada za kuwasiliana na Taasisi mbalimbali ili kuona namna gani wanaweza kusaidiana kulitatua tatizo la Umeme ambalokwa sasa linahitaji uwezo wa ziada.

“ Licha ya uchimbwaji wa Kisima hicho cha maji kuondoatatizo la Wananchi hao lakini bado kazi iliyopo hivi sasa ya huduma ya umemeinahitaji gharama kubwa”. Alisisitiza Balozi Seif.

Alisema upo uzoefu unaoonyesha kwamba tatizo laukosefu wa maji safi katika maeneo mengi linaonekana kusababishwa na nguvu ndogo zinazotokana na mashine  zinazowekwa kwenye visima vya maji.

Akizungumzia kivuko kiliopo kati ya  Kilombero Skuli na Kilombero Juu Balozi Seif aliagiza kupatiwa makisio ya gharama za kazi ya Matengenezo ya eneo hilo muda wowote kuanzia sasa ili kukamilisha kazi hiyo na kutoa faraja kwa watoto na wakaazi wa eneo hilo.

Balozi Seif alisema hatua ya kuondosha usumbufu huoinawezekana kukamilishwa ndani ya wiki moja baada ya  kupatikana kwa Kifusi na  Makalvati.

Mapema Mke wa Mbunge wa Jimbo Hilo la Kitope Mama Ash aSuleiman Iddi aliwakumbusha Wananchi hao kuendelea kuthamini juhudi zinazochukuliwa na Viongozi wao katika kuwatatulia kero zinazowakabili.

Uchimbaji wa kisima cha Maji safina salama kwa ajili ya Shehia hiyo ya kilombero unaendelea katika eneo la Kilombero juu ukigharamiwa na Mbunge wa Jimbo hilo.
 
Na
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar
 
 

VIONGOZI WA CHADEMA WASHIRIKI SIKUKUU YA IDD NA WAKAZI WA MKOA WA MOROGORO

 Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wakishiriki katika chakula cha mchana kilichoandaliwa na wenyeji wao wa mkoa wa Morogoro, ikiwa ni sehemu ya kuuadhimisha sikuu ya Idd el Fitr, baada ya kusitisha Opereshini Sangara jana ili kuungana na waislamuu nchini kote kuadhimisha sikukuu hiyo. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu, Dk. Willibrod Slaa, mwanachama Arcado Ntagazwa, Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Said Issa Mohamed na Mwenyekiti wa Mkoa wa Tabora, Kansa Mbarouk.
  Viongozi wa Chama cha Demokarsia na Maendeleo (Chadema), wakiongozwa na Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe (wa nne kutoka kushoto), wakishiriki chakula kilichoandaliwa na wenyeji wao mjini Morogoro, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha sikukuu ya Idd el Fitr, baada ya kusitizsha kampeni za Operesheni Sangara katika mkoa wa Morogoro jana, ili kuungana na waislamu kote nchini kusherehekea sikukuu hiyo. Kutoka kushiti ni mwanachma wa chama hicho, Arcado Ntagazwa, Katibu Mkuu, Willibrod Slaa, Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Said Issa Mohamed.Picha na Joseph Senga
--
Taarifa Juu Ya M4C Ya CHADEMA Morogoro
-- CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza mafanikio kiliyopata katika majimbo sita (na nusu) ya Mkoa wa Morogoro katika operesheni kinayoendesha mkoani humo, huku pia kikitoa tuhuma nzito dhidi ya mahasimu wao wa kisiasa CCM kwa kuendesha na kusimamia hujuma dhidi ya chama kikuu hicho cha upinzani nchini.

Katika mkutano na waandishi wa habari jana Mjini Morogoro, CHADEMA kimesema kuwa kwa kutumia Operesheni Sangara-Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) inayoendelea mkoani humo, kimefanikiwa kufika katika kata 195 kati ya kata 237 za mkoa mzima wa Morogoro, ambapo kimefanya mikutano katika vijiji 471 ambapo wananchi wamekichangia takriban milioni 17.8 katika mikutano hiyo.


Mbali ya takwimu hizo, chama hicho kimesema kuwa katika siku 13 (hadi jana) katika mkoa huo kimeweza kuvuna wanachama wapatao 31,537, kimeunda matawi ya kudumu zaidi ya 100, mapato ya mauzo ya kadi yakiwa ni Tshs. Milioni 15.7, huku pia kikikabidhiwa takriban kadi 7650 za vyama vingine kutoka kwa Watanzania ambao waliamua ‘kuvua gamba na kuvaa gwanda’ katika mikutano ya hadhara ya chama hicho


Pia chama hicho kimetoa tamko la kuwataka Watanzania wote bila kujali tofauti zao katika jamii kushiriki katika shughuli ya sense ya watu na makazi, kikisema kuwa ni muhimu idadi ya watu kujulikana na kuelewa namna wanavyoishi na kupata huduma za kijamii ili iwe rahisi kuweza kupanga mipango mbalimbali, huku kikisema kuwa idadi hiyo ya watu itakisaidia pia chama hicho kikishika dola kama kinavyojiandaa sasa.


Kauli dhidi ya hujuma


Akizungumza mbele ya waandishi wa habari jana, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Willibrod Slaa alitoa tuhuma nzito dhidi ya CCM kuwa kimekuwa na mtindo wa kuingiza silaha nchini, zikiwemo bunduki bila kibali wala kuzikatia leseni, kisha kinawapatia vijana wake wanaowekwa kwenye makambi maeneo mbalimbali nchini kwa ajili ya kufundishwa mbinu za kuwashughulikia wapinzani wao kisiasa, hasa CHADEMA.


“Kwa hapa Morogoro Mjini tayari tunazo taarifa tumeshaambiwa kuna vijana kama 10-20 wanaandaliwa kufanya njama za kuhujumu CHADEMA, watavalishwa kombati kama hizi za kwetu, watafanya fujo ili ionekane ni sisi, wamepewa sumu, tindikali na sindano kwa ajili ya kukamilisha hizo hujuma wanazopanga dhidi yetu. Kwa baadhi yetu tunaowafahamu CCM hili si suala jipya, walifanya hivyo hivyo wakati wa uchaguzi mdogo Igunga, moja ya makambi ilikuwa Ilemo, Iramba.


“Lakini pia huu ndiyo mtindo wao, wana tabia ya kuingiza hata bunduki nchini bila kibali wala leseni wanapatia vijana, kisha wakishafanya hivyo wanajiandaa kuhamishia tuhuma CHADEMA, hii ndiyo sababu ya Wilson Mkama kutamka wakati ule kuwa tumeingiza makomandoo nchini, kumbe wao tayari wameshaweka vijana makambini na wanafundisha, tena waliohusika kufundisha ni polisi na usalama wa taifa. Tulitoa taarifa polisi juu ya masuala yote na ushahidi tukawapatia wafuatilie, lakini kwa sababu wanahusika mpaka leo hakuna hatua yoyote.


Mbali ya kutoa onyo kwa mtu yeyote ambaye anajipanga kukihujumu chama hicho katika opresheni hiyo inayoendelea mkoani Morogoro kabla ya kuelekea Iringa, Dkt. Slaa alisema kuwa watatoa taarifa polisi juu ya njama hizo za vijana kuandaliwa lakini hawana mpango wowote wa kushtaki CCM kwa njama zote wanazozibaini kuwa zinalenga kukihujumu chama hicho, kwani kufanya hivyo ni ‘sawa na kupeleka kesi ya nyani kwa ngedere’. Lakini alisistiza kuwa wakati utakapofika wataweka hadharani nyaraka ya baadhi ya alizodai kuwa ni njama zinazoendeshwa na CCM dhidi yao.


Tamko dhidi ya Pinda


Mbali ya hilo, Dkt. Slaa pia alisema kuwa CHADEMA kinatoa muda wa mwezi mmoja kwa Ofisi ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kutoa ufafanuzi wa kina na hadharani juu ya michango yote ambayo Watanzania walichangia katika maafa ya mafuriko ya Kilosa, Dar es Salaam, mabomu ya Gongolamboto na Mbagala, huku pia akimtaka Pinda amwagize CAG afanye ukaguzi wa harufu ya matumizi mabaya katika maafa hayo, akitolea mfano wa Kilosa ambako alisema wamebaini mambo mengi yasiyokuwa ya kawaida.


Dkt. Slaa pia aliongeza kusema kuwa wanafanya utaratibu ili chama hicho kiwaagize wabunge wa chama hicho waandae hoja mahsusi kisha ipelekwe bungeni ili kuihoji na kuitaka serikali itoe taarifa ya kina ya hali ilivyo katika maeneo yote hayo yaliyopatwa na maafa, akisema kuwa wamebaini kuwepo kwa ufisadi mkubwa katika michango ya waathirika wa matukio ya maeneo hayo, huku ahadi walizoahidiwa na serikali hazijatimizwa mpaka leo, ndiyo maana bado kuna malalamiko kutoka kwa watu.


Mbali ya hilo pia amemtaka Waziri Mkuu Pinda kutoa taarifa ya kina juu ya namna gani mpaka sasa serikali imefanyia kazi migogoro ya wakulima na wafugaji katika maeneo mbalimbali ikiwemo Kilosa na Rukwa kama alivyowahi kuahidi bungeni kuwa serikali italifanyia kazi tatizo hilo ili kuepusha maafa ambayo yamekuwa yakitokea mara kwa mara kila mara makundi hayo yanapoingia katika mikwaruzano ya kugombea maeneo ya kazi zao za kilimo au kuchungia mifugo yao.


“Wakati huo nikiwa bado bungeni, Pinda alituomba kuwa tutulie serikali itatoa kauli juu ya suala hili, kesho yake akatuahidi kupitia kwa Waziri Celina Kombani wakati huo akiwa TAMISEMI kuwa watalifanyia kazi tatizo la wafugahi na wakulima, lakini leo hii wanayofanyiwa wafugaji wa Kilosa kwa mkono wa serikali kufanywa mtaji wa viongozi kwa kuombwa rushwa baada ya kukamata wake zao wengine wana mimba au mabinti zao, hakiwezi kuvumilika. Miaka mitatu ameshindwa kushughulia tatizo hili, wakulima na wafugaji wanateseka, kwa nini asiwajibike kwa kujiuzulu,” alisema Dkt. Slaa.


“Tumekutana na waathirika wa Kilosa, kwa kweli wanaishi katika hali ambayo hutegemei binadamu anaweza kuishi, watu wale wametelekezwa na serikali, wakati wanapata matatizo hayo katika Ofisi ya Waziri Mkuu kuna kitengo cha maafa ambacho kila mwaka kinapangiwa bajeti kwa kazi hiyo, lakini mbali ya hilo, Watanzania nchi nzima walihamasika kuwachangia waathirika hao, lakini mpaka sasa nia ajabu michango hiyo walikuwa wakiisikia redioni na kuiona kwenye televisheni, tunamtaka Pinda atuambie.


“Tunataka uwajibikaji wa serikali katika namna ambavyo waathirika wa majanga au maafa haya wamesaidiwa kama binadamu na Watanzania wanaolipa kodi kwa serikali kila siku, tena mkikumbuka yale ya Gongolamboto na Mbagala yalitokana na uzembe wa serikali kabisa, sasa hatuwezi kuona watu wanaendelea kuumia kwa uzembe wa serikali,” alisema Dkt. Slaa.


Tamko la Sensa


Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar, Said Issa Mohamed aliwataka Watanzania wote nchini bila kujali tofauti zao za kidini wala rangi au maeneo, kushiriki shughuli ya sense ya watu na makazi itakayofanyika mwishoni mwa juma hili. Akitoa wito huo, aliongeza kusema kuwa ushiriki wa wananchi katika zoezi hilo muhimu katika kupanga mipango ya maendeleo, hasa katika utoaji wa huduma mbalimbali za kijamii utakisaidia chama hicho pia katika harakati za kuwapigania.


“Hata baba ndani ya nyumba ukijua idadi ya watu wako katika familia ni rahisi kuweza kupanga mahitaji yao, lakini mbali ya hilo Watanzania wanajua namna ambavyo takwimu hizi zitatusaidia sisi CHADEMA tutakapoingia madarakani kama mabvyo tunajipanga kutokana na wao kuendelea kutukubali na kutuunga mkono, kwetu CHADEMA ukijua watu na makazi yao itakuwa rahisi kujua mahitajio ya wananchi na kuweka mfumo sahihi wa kuwatumikia,” alisema Mohamed.


Mafanikio ya Operesheni Morogoro


Naye Kamanda wa Operesheni Sangara-M4C inayoendelea mkoani Morogoro, Benson Kigaila akizungumzia mafanikio na changamoto tangu waanze, ambapo jana ilikuwa ni siku ya 13 tangu uzinduzi katika mkoa huo ulipofanyika Wilayani Kilombero, mjini Ifakara, alisema kuwa kwenye mkutano wa mwisho kwa mkoa wa Morogoro utakaofanyika kati ya Alhamis au Ijumaa wiki hii, wataweka hadharani ‘mali’ zote za vyama vingine walizokabidhiwa na waliokuwa wanachama wa vyama hivyo ambao wamehamia CHADEMA.


“Leo ni siku ya 13 tangu tumeanza operesheni hii kwa mkoa wa Morogoro, safari hii iliyoanzia Morogoro itatuchukua katika mikoa mitano, Iringa, Dodoma, Manyara kisha Singida. Hadi sasa tumekwenda majimbo sita na nusu ya Morogoro kwa sababu tumepiga nusu ya Mvomero na nusu tutaimalizia kesho. Katika siku zote hizi wananchi wameendelea kutuchangia katika mikutano yao, wametoa michango ya hali na mali, ni ishara nzuri ya kuwa wanaunga mkono mabadiliko na wanashiriki kumiliki mchakato huu muhimu.


“Kutokana na ziara hii kutwa tofauti sana na zingine za huko nyuma, inafanana fanana na ile ya Kusini, wanachama wote wanasajiliwa, uongozi unaundwa kwa kila tawi, tuna namba zao za simu, kwa hiyo hata tukiamua kuwasiliana nao kwa meseji kwa mara moja tunaweza kufanya hivyo nchi nzima, tunaunda mtandao wa kudumu wa chama kinachojiandaa kuchukua dola. Katika mikutano hiyo tumepokea kero za wananchi, tumezungumza nao, wameonesha matumaini makubwa sana kwetu,” alisema Kigaila.


Baada ya mapumziko ya siku mbili kwa ajili ya Siku Kuu ya Eid-El-Fitr, chama hicho kitaendelea na operesheni yake katika mkoa wa Morogoro leo, kwa kumalizia Jimbo la Mvomero
 
 

No comments:

Post a Comment