Sunday, July 8, 2012

WAKIMBIZI WA KITANZANIA WAREJESHWA NCHINI KWA NDEGE YA UMOJA WA MATAIFA

 Watanzania waliokuwa wakiishi ukimbizini Mogadishu Somalia wakirejea nchini jana na ndege ya Umoja wa Mataifa wakiwa na familia zao walikokuwa wakiishi tangu Januari 2001 wakikimbia vurugu zilizotokea Zanzibar baada ya Uchaguzi Mkuu, Watanzania hao ni 38 wakiwa pamoja na wake zao, Raia wa Somalia pamoja na watoto
 Baadhi ya Wanzania 38 waliokuwa wakimbizi Jijini Mogadishu wakielekea sehemu ya mapokezi mara baada ya kushuka katika ndege la Umoja wa Mataifa iliyowaleta nyumbani wakiwa na wake zao walioa nchini Somalia baada ya kuishi huko kwa miaka 11,walikimbia vurugu za Januari 26/27 mwaka 2001
  Baadhi ya Watanzania waliokimbilia Mogadishu mwaka 2001 wakiwa katika Ofisi ya Uhamiaji Zanzibar jana. Wa kwanza ni Mohammed Adam(38)  akiwa amembeba mwanawe mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume,wanaotazama kamera ni baadhi ya wake wa Watanzania hao ambao ni raia wa Somalia waliowasili jana wakitokea Mogadishu Somalia na ndege ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia huduma za kibinadamu
 Baadhi ya Watoto wakiwa na wazazi wao Raia wa Tanzania waliokuwa wakimbizi nchini Somalia wakiwa katika Ofisia za Uhamiaji uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume mara baada ya kuwasili na ndege la UN zinazohusika na huduma za kibinadamu.
 Baadhi ya akinamama Raia wa Somalia ambao wameolewa na Watanzania waliokuwa ukimbizini Mogadishu wakifurahia jambo walipowasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume,hapa walikuwa wakisubiri taratibu za Uhamiaji
 Watoto ambao kwa sasa ni Raia wa Somalia wakiwa na wazazi wao Raia wa Tanzania waliokuwa wakimbizi nchini Somalia wakisubiri taratibu za Uhamiaji katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume jana baada ya kuwasili wakitokea Mogadishu na ndege ya Umoja wa Mataifa chini uangalizi wa UNHCR
Watanzania waliokuwa wakimbizi katika kambi ya Mogadishu wakielekea kupanda mabasi maalum yaliyoandaliwa na Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa baada ya kuwasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume jana(Picha na Juma Mohammed,MAELEZO Zanzibar)

WAZIRI MKUU AZINDUA MATREKTA SONGEA

 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwasha trekta wakati alipozindua kampeni ya  kimkoa ya matumizi ya matrekta makubwa katika kilimo mkoa wa Ruvuma iliyofanyika kwenye  uwanja wa zimamoto mjini Songea Julai 7, 2012.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama ngoma wakati  alipozindua kampeni  ya kimkoa  ya matumizi  ya matrkta makubwa katika kilimo mkoani Ruvuma iliyofanyika kwenye uwanja wa zimamoto mjini Songea Julai 7,2012.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikata utepe kuashiria uzinduzi wa  kampeni  ya  kimkoa ya matumizi  ya  Matrekta makubwa katika kilimo mkoani Ruvuma iliyofanyika kwenye  uwanja wa zimamoto mjini Songea Julai 7,2012.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua miche ya kahawa wakati alipotembelea shamba la katika kijiji cha Likopelo wilayani Songea vijijini Julai 7, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 

MH ZITTO KABWE ATEMBELEA BANDA LA PPF NDANI YA VIWANJA VYA SABASABA

 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,William Erio (kulia) akizungumza na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zito Kabwe (kushoto), Alipotembelea banda hilo kwenye Maonyesho ya 36 ya Biashara ya Kimataifa Uwanja wa Sabasaba Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,William Erio (kulia) akizungumza na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zito Kabwe (kushoto), Alipotembelea banda hilo kwenye Maonyesho ya 36 ya Biashara ya Kimataifa Uwanja wa Sabasaba Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,William Erio (kulia) akizungumza na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zito Kabwe (kushoto), Alipotembelea banda hilo kwenye Maonyesho ya 36 ya Biashara ya Kimataifa Uwanja wa Sabasaba Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,William Erio (kulia) akizungumza na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zito Kabwe (kushoto), Alipotembelea banda hilo kwenye Maonyesho ya 36 ya Biashara ya Kimataifa Uwanja wa Sabasaba Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,William Erio (katikati) akizungumza na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zito Kabwe (kushoto), Alipotembelea banda hilo kwenye Maonyesho ya 36 ya Biashara ya Kimataifa Uwanja wa Sabasaba Dar es Salaam na kulia ni Meneja Mahusiano ya Umma PPF,Lulu Mengele. 
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,William Erio (kulia) akizungumza na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zito Kabwe, Alipotembelea banda hilo kwenye Maonyesho ya 36 ya Biashara ya Kimataifa Uwanja wa Sabasaba Dar es Salaam.
 Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) na Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mkoa wa Morogoro,Anthony Mraka (kulia) akioneshwa picha ya Jengo la PPF Plaza Arusha katika TV na  Meneja Mahusiano ya Umma PPF,Lulu Mengele(katikati) na Afisa UhusianoJanet Ezekiel, Alipotembelea banda hilo kwenye Maonyesho ya 36 ya Biashara ya Kimataifa Uwanja wa Sabasaba Dar es Salaam.
Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) na Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mkoa wa Morogoro,Anthony Mraka (kulia) akiagwa na Meneja Masoko na Huduma kwa Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,Mbaruku Magawa (kushoto) na Meneja Mahusiano ya Umma PPF,Lulu Mengele,Alipotembelea banda hilo kwenye Maonyesho ya 36 ya Biashara ya Kimataifa Uwanja wa Sabasaba Dar es Salaam.
 
 

CHAMELEONE AFUNIKA TAMASHA LA USIKU WA MATUMAINI NDANI YA UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR

Chameleone akiingia uwanjani kuwarusha mashabiki waliofurika Uwanja wa Taifa usiku huu.
Jose akiimba na maelfu ya wapenzi wa burudani waliofurika ndani ya Uwanja wa Taifa usiku huu.
Sehemu ya maelfu ya wakazi wa jiji la Dar waliokuwa wanafuatilia shoo hiyo.

---
Mwanamuziki mahiri kutoka nchini Uganda, Joseph Mayanja 'Jose Chameleone' usiku wa leo amefunika vilivyo katika Tamasha la Usiku wa Matumaini lililofanyika ndani ya Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Chameleone aliwarusha mashabiki kwa baadhi ya nyimbo zake za zamani kama Mambo bado, Kipepeo na ile mpya iitwayo Valu Valu inayopendwa na watu wengi hapa Bongo.
 

TASWIRA ZAIDI ZA PAMBANO LA WEMA NA WOLPER,WEMA AMKIMBIA MPINZANI WAKE

Bondia Wema Sepetu akimkimbia mpinzani wake Jacklen Wolper wakati wa mpsambano wao 
Refa John Chagu akiwainua mikiono juu mabondia Jacklen Wolper kushoto na Wema Sepetu kuashiria mpambano wao ni droo
WEMA NA WOLPER wakipozi kwa picha
Mdau wa mchezo wa Masumbwi Nchini Ibrahimu Kamwe akimwelekeza bondia Wema Sepetu 
Baada ya mpambano wawili hawo hawo wanaondoka eneo la tukio
Mabondia ambani ni wacheza filamu maarufu nchini Wema Sepetu kushoto na Jacklen Wolper wakioneshana ufundi wa kutupiana masumbwi wajkati wo Tamasha la vMatumaini lililofanyika jumamosi katika uwanja wa Taifa.Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
 
 
 

No comments:

Post a Comment