Friday, July 13, 2012

Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu Joseph Warioba Aongoza Mkutano Wa Kukusanya Maoni ya Wananchi Kuhusu Katiba Mpya Kijiji cha Veyula, Kata ya Makutupora, Dodoma

Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu Joseph Warioba akibadilishana mawazo na Wajumbe wengine katika Kijiji cha Veyula, Kata ya Makutupora, Dodoma Jumatano, Julai 11. 2012, kabla ya kuanza kwa mkutano wa kukusanya maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya. Picha na Omega Ngole
 
 

WENYE MITANDAO YA JAMII NCHINI SASA KUPEWA TUZO NA VODACOM TANZANIA

Waandishi wa mitandao ya kijamii na tovuti kupewa tuzo kutokana na jitihada na mafanikio yao.   
 
Tuzo hizo kuitwa “ Tuzo za umahiri wa digitali za Vodacom
Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania, itatoa tuzo kwa waandishi bora kumi mahiri katika mitandao ya kijamii kutokana na umahiri wao.

Tuzo hizo ambazo zimepewa jina la “Tuzo za Umahiri wa Digitali za Vodacom”, zitatolewa kwa washindi kumi kutokana na jitihada zao na mafanikio yao ikiwa ni kwa mala ya Kwanza kufanywa na kampuni ya simu za Mkononi ya Vodacom.
 
Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Rene Meza amesema kuwa Waandishi wa mitandao ya kijamii wanao mchango mkubwa katika kutoa taarifa mbalimbali ndani ya jamii, na mchango huu unatakiwa kuthaminiwa.
 
Wapo waandishi wengi katika mitandao ya kijamii na wanaandika masuala mbalimbali kuhusu biashara au hata yale yanayogusa jamii moja kwa moja, Ni kwa sababu hii ndio maana tunatambua na kuwapatia tuzo hizi kutokana na mabadiliko waliochangia katika utoaji wa taarifa” Alisema Meza.
 
Baadhi ya sifa ambazo zitapewa kipaumbele katika tuzo hizi, pamoja na mambo mengine, ni ubunifu na utoaji wa taarifa za kijamii,  Kuzingatia ueledi wa uandishi na uhuru wa vyombo vya habari, mahusiano na wasomaji katika utoaji wa taarifa, umahiri wa picha na ushirikishwaji wa vyombo vingingine.
 
Waandishi wa mitandao ya kijamii wata shindanishwa kadri inavyowezekana ili kuwawezesha kuongeza ueledi na umahiri katika kazi zao.
 
Kampuni ya Vodacom Tanzania pia itaanzisha  mfuko wa fedha wa maendeleo ya digitali, Kwa mujibu wa Meza fedha hizi zitatumika katika kuendeleza umahiri na kuboresha kazi katika mitandao ya kijamii na tovuti.“Huu ni mchango kutoka Mfuko wa M-pesa ambapo waombaji wataweza kuzitumia katika udhamini na kuendeleza shughuli zao”, Alisema Meza na kuongeza kuwa, “ Tunathamini mchango wa kila mtu, na tunahitaji waandishi wa mitandao ya kijamii wote waendelee kufanya kazi zao nasi tutaendelea kuthamini na kutambua mchango wao na kuwapa tuzo.”
 

MKURUGENZI MTENDAJI WA FULLSHANGWE APIGA TAFU MATIBABU YA SAJUKI

 
Mkurugenzi  mtendaji wa Fullshangwe Blog, Bw. John Bukuku akimkabidhi mke wa Sajuki, Wastara Juma kiasi cha Sh. laki moja 100,000, kama sehemu ya mchango wake kwa ajili ya matibabu ya Mumewe.
 
 
 
 

MATUKIO MBALIMBALI YA ZIARA YA RAIS KIKWETE NCHINI UINGEREZA

Rais Jakaya Mrisho kikwete, Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda na mkewe Mama Janet Museveni, Waziri Mdogo wa Uingereza wa Maendeleo ya Kimataifa Bw. Stephen O'Brien (kulia) na Mama Melinda Gates wakibadilishana mawazo kabla ya kuhutubia katika mkutano wa kimataifa wa viongozi kujadili Uzazi wa Mpango kwa nchi masikini zaidi duniani katika ukumbi wa Queen Elizabeth II jijini London July 11, 2012. Mkutano huo ni wa kwanza wa aina yake duniani na umeanzisha Mchakato wa Dunia ambao utalenga kuwawezesha wanawake wapatao milioni 120 katika nchi masikini zaidi duniani kupata habari, huduma na mahitaji ya kupanga uzazi bora zaidi na kuokoa maisha yao ifikapo mwaka 2020.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akuhutubia katika mkutano wa kimataifa wa viongozi kujadili Uzazi wa Mpango kwa nchi masikini zaidi duniani, katika ukumbi wa Queen Elizabeth II jijini London July 11, 2012. Mkutano huo ni wa kwanza wa aina yake duniani na umeanzisha Mchakato wa Dunia ambao utalenga kuwawezesha wanawake wapatao milioni 120 katika nchi masikini zaidi duniani kupata habari, huduma na mahitaji ya kupanga uzazi bora zaidi na kuokoa maisha yao ifikapo mwaka 2020.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake katika mazungumzo na Afisa Mtendaji Mkuu wa British Gas (BG Group), Sir Frank Chapman (wa pili kulia) na maafisa waandamizi wa kampuni hiyo. BG Group imewekeza kiasi cha Pauni 80 za Uingereza (Shilingi Trilioni 125) katika mradi wa kuchimba gesi asilia nchini Tanzania, na tayari visima vitano vya nishati hiyo vimeshatema gesi nyingi katika bahari kuu kusini mwa Tanzania maeneo ya Mtwara. Hii ilikuwa ni ziara fupi katika makao makuu ya BG Group mjini Reading, Uingereza ambako Rais Kikwete na ujumbe wake walitembelea Julai 11 kujionea namna kazi za uvumbuzi wa gesi asilia unavyofanywa na kampuni hiyo yenye kufanya shughuli zake katika nchi 21 katika mabara matano, ikiwa na jumla ya wafanyakazi 6,000.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri Mkuu wa Uingereza Bw. Donald Cameron, Rais Paul Kagame wa Rwanda na Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda wakijiandaa kupanda jukwaani kuhutubia katika mkutano wa kimataifa wa viongozi kujadili Uzazi wa Mpango kwa nchi masikini zaidi duniani. katika ukumbi wa Queen Elizabeth II jijini London July 11, 2012. Mkutano huo ni wa kwanza wa aina yake duniani na umeanzisha Mchakato wa Dunia ambao utalenga kuwawezesha wanawake wapatao milioni 120 katika nchi masikini zaidi duniani kupata habari, huduma na mahitaji ya kupanga uzazi bora zaidi na kuokoa maisha yao ifikapo mwaka 2020.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na  Afisa Mtendaji Mkuu wa British Gas (BG Group), Sir Frank Chapman alipotembelea makao makuu ya kampuni hiyo mjini Reading Uingereza Julai 11, 2012. BG Group imewekeza kiasi cha Pauni 80 za Uingereza (Shilingi Trilioni 125) katika mradi wa kuchimba gesi asilia nchini Tanzania, na tayari visima vitano vya nishati hiyo vimeshatema gesi nyingi katika bahari kuu kusini mwa Tanzania maeneo ya Mtwara. Hii ilikuwa ni ziara fupi katika makao makuu ya BG Group mjini Reading, Uingereza ambako Rais Kikwete na ujumbe wake walitembelea Julai 11 kujionea namna kazi za uvumbuzi wa gesi asilia unavyofanywa na kampuni hiyo yenye kufanya shughuli zake katika nchi 21 katika mabara matano, ikiwa na jumla ya wafanyakazi 6,000.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mdogo wa Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza Bw. Stephen O'Brien jijini London, ambapo Uingereza iliahidi kuendelea kuisaidia Tanzania katika mambo mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kusaidia kuendeleza sekta ya nishati hususan utafutaji wa gesi asilia.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Hussein Mwinyi akiongea na baadhi ya wajumbe wa mkutano wa kimataifa wa Uzazi wa Mpango katika ukumbi wa Queen Elizabeth II jijini London Julai 11, 2012. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Uzazi na Malezi Bora Tanzania (UMATI), Bi Josephine Mwankusye na kulia ni Naibu Mkurugenzi wa Afya ya Mzazi na Mtoto katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt Neema Rusibamayila.PICHA NA IKULU 
 
 

MREMBO BORA WA MISS SINZA 2012 KUPATIKANA KESHO, TWANGA KUWASHA MOTO

 Mwalimu wa warembo wa shindano la kumsaka Miss Sinza 2012, Mwajabu Juma, akitoa maelekezo kwa warembo hao wakati wa mazoezi yao ya mwisho kujiandaa na shindano hilo litakalofanyika kesho katika Ukumbi wa Mawela Social, karibu na Vatcan Hoteli, Sinza. Shindano hilo litasindikizwa na burudani kabambe na shoo ya kufa mtu kutoka kwa Bendi ya African Stars, watakaokuwa wakitambulisha pia baadhi ya nyimbo zao mpya kwa mara ya kwanza, pamoja na msanii wa Vichekesho kutoka kundi la Ze Commedy linalorusha michezo yake kupitia Televisheni ya Chanel 5, Masawe Mtata, ambaye pia atakuwa akitambulisha video ya wimbo wake mpya uitwao Uongo Kweli.
 Warembo hao wakiwa katika mazoezi yao ya pamoja ya shoo ya ufunguzi, jana jioni ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mwisho kuelekea shindano lao litakalofanyika kesho kwenye Ukumbi wa Mawela Social, karibu na Vatcan Hotel.
 Warembo hao wakiwa katika mazoezi yao ya pamoja ya shoo ya ufunguzi, jana jioni ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mwisho kuelekea shindano lao litakalofanyika kesho kwenye Ukumbi wa Mawela Social, karibu na Vatcan Hotel.
 Warembo hao wakiwa katika mazoezi yao ya pamoja ya shoo ya ufunguzi, jana jioni ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mwisho kuelekea shindano lao litakalofanyika kesho kwenye Ukumbi wa Mawela Social, karibu na Vatcan Hotel.
 Warembo hao wakipozi kwa picha ya pamoja baada ya kumaliza mazoezi yao.

Warembo hao wakipozi kwa picha ya pamoja baada ya kumaliza mazoezi yao.
**********************************
*Mrembo wa Sinza kupatikana kesho (Ijumaa)

Mwandishi Wetu
MASHINDANO ya kumsaka mrembo bora waKitongoji cha Sinza, Redds Miss Sinza 2012 yatafanyika kesho (Ijumaa) kwenye ukumbi wa Mawela Social Hall (Ten Star Lounge) uliopo karibu na hoteli ya Vatican City.

Mashindano hayo yatashirikisha jumla ya warembo 14 wanaowania taji la kituo hicho pamoja na kuiwakilisha kitongoji cha Sinza kwenye mashindano ya Kanda ya Kinondoni na baadaye Miss Tanzania.

Mbali ya taji (crown) na nafasi ya kuiwakilisha Sinza katika Mashindano ya Kanda ya Kinondoni, pia mshindi wa kwanza katika shindano hilo atajinyakulia kitita cha sh. 500,000/=  katika mashindano hayo yatakayopambwa na bendi ya African Stars “Twanga Pepeta International’ ambao watakuwa wakitambulisha baadhi ya nyimbo zao mpya na Msanii wa vichekesho wa kundi la Ze Comedy la Chanel 5, Masawe Mtata, atakayekuwa akitambulisha video na wimbo wake mpya wa Uongo Kweli.

Akizungumza na mtandao huu, Mratibu wa mashindano hayo kutoka kampuni ya Calapy Entertainment, Majuto Omary, alizitaja zawadi nyingine kuwa ni shs 400,000 kwa mshindi wa pili, sh. 300,000 kwa mshindi wa tatu . Mshindi wa nne na wa tano watapata sh. 150,000 kila mmoja na waliobaki watapata sh. 100,000 kila mmoja kama kifuta jasho.

Aidha Majuto, aliongeza kuwa mbali ya kutembea jukwaani kwa ‘catwalk’ kwa warembo hao, pia kutakuwa na shindano la kusaka vipaji ambapo warembo watachuana  ili kumpata Mafoto Miss Talent Sinza 2012, ambapo mshindi atapata sh. 50,000 kutoka mtandao wa sufianimafoto.blogspot.com.

“Maandalizi yamekamilika na viingilio vitakuwa ni sh. 10,000 kwa viti vya kawaida na sh. 25,000 kwa vitu Maalum (VIP), tumeandaa shoo fupi na ya aina yake ili baadaye mashabiki wa fani ya urembo wa kitongoji cha Sinza wapate fursa ya kusugua kisigino na bendi ya Twanga Pepeta,” alisema Majuto.

Majuto aliwataja Warembo wanaowania taji hilo kuwa ni pamoja na Mariam Miraji, Naima Mohamed, Lulu Ambonela, Maria John, Judith Sangu, Eva Mushi, Vailet John na  Esther Mussa.

Warembo wengine ni Christina Samwel, Nahma Said, Aisha Ramadhan, Nancy Musharuzi, Brigitter Alfred na Merina Mushi.
 
Shindano hilo limedhaminiwa na Redds Premium Cold, Dodoma Wine, Gland Villa Hotel, Clouds FM, mtandao wa sufianimafoto.blogspot.com, Brake Point, Fredito Entertainment, Screen Masters,  Lady Pepeta na flexi.
 

No comments:

Post a Comment