Thursday, January 19, 2012

Mauaji zaidi yatokea Sudan Kusini






Kundi la wapiganaji wa kikabila wenye silaha Sudan Kusini
Watu wenye silaha wamewaua takriban watu 51 wengi wakiwa wanawake na watoto katika mapigano ya hivi karibuni katika jimbo lenye mgogoro la Jonglei, gavana wa jimbo hilo Kuol Manyang amesema
Kiasi cha watu 22 wamejeruhiwa baada ya washambuliaji kuvamia na kuchoma kijiji cha Duk Padiet, aliongeza.
Waliojeruhiwa wamehamishiwa Juba makao makuu ya nchi.
Mfululizo wa mashambulizi ya kikabila kati ya makundi katika eneo hilo yamefanya maelfu ya watu kukosa makazi.
"Tunatarajia wengi wakiwa wamejeruhiwa kwa sababu walikimbia vijiji vyao usiku wa jana," Bw Manyang alisema.
Maafisa wameliambia shirika la habari la AFP kuwa mauaji hayo yalifanywa na kundi la Murle kwa kabila la Wadinka, kulipa kisasi kwa uvamizi mbaya wa mwezi uliopita katika mji wa Pibor.
Inafahamika kuwa baadhi ya Wadinka waliwasaidia wapiganaji wa Lou Nuer 6,000 ambao walishambulia Pibor.
Mzunguko wa ghasia hizi umedumu kwa miezi na mamia wameuawa. Zilianza kama wizi wa ng’ombe lakini zimesambaa na kushindwa kudhibitiwa.
Mwandishi wa BBC Afrika Mashariki Will Ross anasema mashambulio hayo yanaongezeka kuwa makali na si serikali wala askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa inavyoonekana wanaoweza kuwadhibiti.
Maafisa wanasema kuwa Jonglei ina ukubwa wa nchi ya Bangladesh na kwamba si rahisi kulinda kila kijiji.
Baadhi ya askari waliopelekwa katika eneo hilo wako Murle na eneo la kuzunguka Pibor lakini mashambulizi ya kisasi yanatokea katika jumuiya za Dinka na Lou Nuer.
Sudan Kusini, iliyopata uhuru wake mwaka jana imetangaza Jonglei kama ‘janga’ wakati UN imezindua harakati za dharura kusaidia walioathiriwa na mapigano hayo












NDUGU ZANGU......


JUMATANO hii ya leo kuna kusanyiko kubwa la watu kule Ifakara. Ni WaTanzania wanaoshiriki kumsindikiza kwenye safari yake ya mwisho, ndugu yetu mpendwa, Regia Estelatus Mtema.
Ni Jumatano hii ya leo, WaTanzania kwa mamilioni, nao, kwa kuelekeza fikra zao kwa Regia, wanashiriki kumsindikiza ndugu yetu Regia Mtema kwenye safari yake ya mwisho hapa duniani.
Katika maisha kuna visivyoshikika,visivyogusika, lakini vipo. Hisia, kwa mfano, zipo na zinaishi. R.I.P. REGIA ESTELATUS MTEMA.

penzi la facebook lasabisha kifo

UHUSIANO wa kimapenzi, ulioanzishwa kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook, umesababisha kifo cha mrembo nchini Nigeria.
Habari za mtandaoni zinadai kuwa mrembo huyo (jina halikutajwa) pamoja na boyfriend wake (jina pia halijatajwa), walikuwa kwenye uhusiano wa muda mrefu.
Imedaiwa kuwa wakati wawili hao wakiwa kwenye utekelezaji wa hatua za mwanzo za kufunga ndoa, mrembo huyo alimtaarifu boyfriend wake kuwa amepata mpenzi mwingine kwa njia ya Facebook.
Chanzo cha habari kiliiambia tovuti moja ya nchi hiyo kwamba mrembo huyo alianzisha urafiki wa Facebook na kijana mmoja raia wa Marekani (jina halijatajwa) kabla ya kibao kubadilika na kuwa wapenzi.
Chanzo kiliendelea kupasha habari kwamba mrembo huyo na mpenzi wake wa Facebook, walidumisha uhusiano wao kwa njia ya mawasiliano ya simu kwa muda mrefu kabla ya kukata shauri la kuonana ana kwa ana.
“Yule kijana raia wa Marekani alitembelea Nigeria, akafikia hoteli moja kubwa. Yule mrembo akaenda kukutana naye na kutumia muda mrefu chumbani.
“Ni kama baada ya kukutana ndiyo mapenzi yaliongezeka zaidi, kwani alipoondoka hotelini, yule mrembo alirudi kwa boyfriend wake aliyepanga kufunga naye ndoa na kumueleza kwamba mapenzi yamekwisha.
“Baada ya kuambiwa hivyo, kijana aliyekuwa na mategemeo ya kufunga ndoa na mrembo huyo, alimpeleleza mpenzi wake na kubaini mahali ambako kijana kutoka Marekani alifikia.
“Siku iliyofuata alivamia kwenye ile hoteli, akamkuta mpenzi wake na yule kijana wa Facebook, hapo ugomvi mkubwa ulizuka. Ugomvi haukuishia hapo kwa sababu kijana wa Nigeria aliahidi ni lazima aue mtu.
“Siku moja baada ya ugomvi hotelini, kijana wa Nigeria alimteka mpenzi wake na kumuua kwa kumkatakata na silaha inayodhaniwa kuwa ni panga,” alisema mtoa habari huyo.
Kwa mujibu wa mtandao huo mpaka pale habari hiyo inachapishwa, mtuhumiwa wa mauaji alikuwa hajakamatwa.

Kamati ya Bunge kuibana Ewura bei ya umeme

 
KAMATI ya Bunge ya Nishati na Madini imesema itakutana na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) na Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco), kujadili kupanda kwa gharama za umeme huku ikisema itakata rufaa kwenye Baraza la Ushindani Kibiashara kupinga ongezeko hilo.






kulala kwenye mwanga wa taa husababisha salatani

IKIWA na mshambuliaji wake hatari, Thierry Henry, Arsenal jana ilikutana na kipigo kikali cha mabao 3-2 kutoka kwa Swansea City,  katika mchezo mkali wa Ligi Kuu ya England uliopigwa kwenye Uwanja wa Liberty.
Katika mchezo huo uliokuwa mkali na wa kuvutia, Arsenal ilijikuta ikionyesha kiwango cha chini na kuwaacha Swansea wakitawala sehemu kubwa ya mchezo huo.
Mshambuliaji wa Arsenal, Robin Van Persie, aliifungia timu yake bao la kwanza katika dakika ya tano tu ya mchezo, lakini Scott Sinclair aliisawazishia Swansea dakika kumi baadaye na kuzifanya timu hizo kwenda mapumziko zikiwa sare ya bao 1-1.
Kipindi cha pili kilitawaliwa na Swansea ambao walionyesha kiwango kizuri na kupiga pasi za uhakika ambazo ziliwasaidia kujipatia bao la pili katika dakika ya 57 lililowekwa kimiani na Nathan Dyer.
Arsenal ambayo inashika nafasi ya tano(5), ilijipatia bao la pili katika dakika ya 69 kupitia kwa Theo Walcott, lakini dakika moja baadaye Danny Graham aliipatia Swansea bao la tatu.
Mashabiki wa Arsenal walikuwa na matumaini makubwa na timu yao kutokana na kiwango kilichoonyeshwa na Henry kwenye mchezo wa FA dhidi ya Leeds United lakini jana mshambuliaji huyo anayecheza hapo kwa mkopo akitokea New York Red Bulls ya Marekani, alibanwa na kushindwa kufurukuta.

No comments:

Post a Comment