WASHIRIKI WA MPANGO WA MAMA SHUJAA WA CHAKULA UNAODHAMINIWA NA NMB WAINGIA KATIKA KIJIJI CHA MAISHA PLUS
Mgeni rasmi katika uzinduzi wa kijiji cha Maisha Plus Naibu Waziri wa Jinsia, Wanawake na Watoto Mhe. Ummy Mwalim akitoa hotuba wakati wa uzinduzi wa shindano hilo kwenye kijiji cha Maisha Plus. Washiriki wa mpango wa mama shujaaa wa chakula unaodhaminiwa na benki ya NMB hatimaye wameingia katika kijiji cha Maisha Plus. NMB inaamini udhamini huo ni sahihi kutokana na kuwa utakuza kilimo na kuwasaidia wakulima wadogo katika maisha, mapambano dhidi ya njaa,umasikini na uhaba wa ajira miongoni mwa wanawake.
Naibu Waziri wa Jinsia, Wanawake na Watoto Mhe. Ummy Mwalim (kushoto) na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa Oxfam Bi. Monica Gorman wakifurahia kinywaji cha dafu wakati wa uzinduzi huo.
Mkurugenzi wa Shindano la Maisha Plus Bw. Masoud A. Kipanya (kushoto) akijadili jambo na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa NMB, Bw. Imani Kajula (kati) pamoja na wageni waalikwa katika uzinduzi huo.
No comments:
Post a Comment