Tuesday, October 2, 2012
AJALI MBAYA IMETOKEA ENEO LA MBALIZI MBEYA
AJALI MBAYA IMETOKEA ENEO LA MBALIZI MBEYA, MAGARI MAWILI YAGONGANA NA KUWAKA MOTO . WATU KUMI WALIPOTIWA KUFARIKI DUNIA, MBUNGE WA VITI MAALUM MH.MARY MWANJELWA ALIKUWEMO KATIKA AJALI HIYO, KATIBU WAKE ATEKETEA KWA MOTO.
WATU 10 wamakufa papo hapo ajalini, 20 wakijeruhiwa akiwemo Mbunge Mary Mwanjelwa,kibaka nae kwenye mishe eneo la tukio aambulia mauti dunia imekwisha !!
HIVI NDIVYO HILI GARI LILIVYO UNGUA MOTO BAADA YA AJALI
HILI NDILO GARI ALILOKUWEMO MBUNGE MARY MWANJELWA LIMETEKETEA LOTE KWA MOTO |
HIVI NDIVYO HILI GARI LILIVYO UNGUA MOTO BAADA YA AJALI
MAMIA YA WATU WALIOFIKA KUSHUHUDIA AJALI HIYO MBALIZI
HIVI NDIVYO GARI HILI LILIVYO PINDUKA NA KUWAKA MOTO BAADA YA AJALI
HII NI GARI NYENGINE AMBAYO PIA ILIWAKA MOTO BAADA YA KUGONGANA
FIRE WAKIWA WAMEWAHI ENEO LA TUKIO KWA AJILI YA KUZIMA MOTO HUO
Mkuu wa mkoa Mbeya Abas Kandoro akiangalia ajali liyotokea mbalizi mbeya mchana wa leo
MKUU WA MKOA WA MBEYA ALIYE VAA SUTI YA BLUE MH. ABASS KANDORO AKIWA ENEO LA AJALI
Watu zaidi ya kumi wamekufa baada ya lori la mafuta kufeli breki na kuyagonga magari mengine matatu katika mtelemko wa mlima wa Iwambi – Mbalizi nje kidogo ya Jiji la Mbeya.
WANANCHI MBALI MBALI WAKIWA WANASHUHUDIA AJALI HUKU WENGINE WAKIWA WANAENDELEA KUOKOA WALIO PATA AJALI
Katika ajali hiyoiliyotokea majira ya saa nane mchana, Mbunge wa viti Maalum CCM Mkoa wa Mbeya, Mary Mwanjelwa alinusurika kufa baada ya gari alilokuwa akisafiria, kugongwa na kuteketea kabisa kwa moto na kusababisha kifo cha Katibu wake, ambapo mbunge huyo amelazwa katika Hospitali Teule ya Ifisi
MBUNGE VITI MAALAM MBEYA DR.MARY MWANJELWA AKIWA HOSPITlLI YA FISI BAADA YA KUPATA AJALI |
Baadhi ya watu waliioshuhudia ajali hiyo, walisema kuwa lori hilo la mafuta lilifeli breki na kuanza kutelemka kwa kasi katika mlima huo, ambapo liliyagonga magari matatu ukiwamo Hiace yenye namba za usajili T 587 AHT.
Kwa upande wake, Muuguzi wa Hospitali ya Ifisi, Sikitu Mbilinyi alisema mbunge Mwanjelwa analalamika zaidi maumivu katika sehemu ya mgongoni na miguu sawa na dereva wake ambaye naye analalamikia miguu na amepasuka sehemu ya kichwani.
KIKOSI CHA FFU NAO WALIKUWEPO SAMBAMBA KATIKA KUHAKIKISHA ZOEZI LA UOKOAJI LINAENDA KIKAMILIFU.
PIA KATIKA ENEO HILI MBUNGE WA VITI MAALUM MH.MARY
MWANJELWAALIKUWEPO NDANI YA PICK UP ILIYO UNGUWA MOTO, KATIBU WAKE ATEKETEA KWA MOTO
wakati huo wananchi wakiwa katika uokoaji si ndo akatokea kibaka ama kweli UKISTAAJABU ya Musa utayaona ya firauni huo ndo msemo pekee ambao naweza kuutumia katika kukujuza yaliyotokea mapema mchana wa leo katika ajali mbaya eneo la mbalizi Mbeya vijijini
em shuhudia mwenyewe ujionanee yalomkuta kibaka uyooo
No comments:
Post a Comment