Saturday, August 4, 2012

Rais wa Zanzibar Dk Ali Shein Akutana Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa Dk. Asha Rose Migiro na Waziri Mkuu Mizengo Pinda

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akifuatana  na Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa Dk. Asha Rose Migiro,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kumpa pole Rais kutokana na Ajali ya meli ya Mv Skigit,na kusababisha Wananchi kupoteza roho zao hivi karibuni.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa Dk. Asha Rose Migiro,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kumpa pole Rais kutokana na Ajali ya meli ya Mv Skigit,na kusababisha Wananchi kupoteza roho zao hivi karibuni.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda, alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kumpa pole Rais kutokana na Ajali ya meli ya Mv Skigit,na kusababisha Wananchi kupoteza roho zao hivi karibuni.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akizungumza na Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda, alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kumpa pole Rais kutokana na Ajali ya meli ya Mv Skigit,na kusababisha Wananchi kupoteza roho zao hivi karibuni.Picha na Ramadhan Othman Ikulu-Zanzibar

Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi:Mgomo Wa Walimu Nchini ni Batili

Wanasheria wa serikali wakiwasili mahakama kuu divisheni ya kazi jijini Dar es Salaam Alhamisi, Agosti 2, 2012 kusikiliza uamuzi wa mahakama hiyo.
Rais wa Chama cha Walimu nchini (CWT), Gratian Mukoba, akiingia mahakamani Agosti 2, 2012
 Katibu Mkuu wa chama cha Walimu nchini (CWT), Ezekiel Oluoch, akiwasili mahakamani hapo Alhamisi Agosti 2, 2012
Wanasheria wa serikali wakisubiri uamuzi wa mahakama Alhamisi Agosti 2012
Viongozi wa vyama vya wafanyakazi, pamoja na walimu, wakiwa mahakamani Alhamisi Agosti 2012, kusubiri uamuzi huo wa mahakama
 Viongozi wa vyama vya wafanyakazi pamoja na walimu, wakiwasili mahakama kuu divisheni ya kazi barabara ya Bibi Titi Mohammed jijini Dar es Salaam alhamisi Agosti 2, 2012 kusikiliza uamuzi wa mahakama kuhusu hatma ya mgomo wa walimu nchini Tanzania
Polisi wakilinda usalama nje ya mahakama.Picha na Mdau  Khalfan Said
--
MAHAKAMA Kuu Divisheni ya Kazi jijini Dar es Salaam, imesema mgomo wa walimu ni batili kwasababu haukuzingatia matakwa ya kifungu cha 84(1),(2) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazi ya mwaka 2004 na uliandaliwa kwa dhamila mbaya. 

Jaji Sophia Wambura wa mahakama hiyo alitoa uamuzi huo jana saa 9:14-37 alasiri huku ukumbi wa wazi wa mahakama hiyo ukiwa umefurika walimu ambapo katika uamuzi wake huo pia aliwataka walimu wote kurejea mara moja kazini. 

Jaji Wambura alisema asikiliza kwa makini hoja za mawakili waandamizi wa serikali Pius Mboya na Obadia Kameya ambao walikuwa wakiwawakilisha walalamikaji katika maombi hayo madogo namba 96/2012 yaliyoletwa chini ya hati ya dharula na Katibu Mkuu Kiongozi,Katibu Mkuu Ofisi ya rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Mwanasheria Mkuu wa Serikali na ya mdaiwa ambaye ni Chama cha Walimu Tanzania(CWT) ambao walikuwa wakiwakilishwa na wakili wa kujitegemea Gabriel Mnyele. 

 Jaji Wambura alisema mgogoro uliowasilishwa mbele yake na walalamikaji ni kwamba wanaiomba mahakama hiyo itamke kuwa mgomo wa walimu ni batili wakati wakili wa CWT ,Mnyere alidai mgomo huo ni halali kwa sababu umekidhi matakwa ya sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini. Jaji huyo alisema mahakama yake imefikia uamuzi wa kutofautiana na zoezi la upigaji kura za kuunga mkono mgomo ambalo liliendeshwa na CWT ambapo asilimia 97 ya walimu waliinga mkono kuanza kwa mgomo kwasababu zifuatazo: “Mosi, zoezi lile la upigaji kula lilikuwa likiwadanganya wanachama wa CWT kuwa zoezi hilo limeendeshwa rasmi na kwa mujibu wa sheria,zoezi lile halikukidhi matakwa ya sheria kwasababu wanachama wake walikuwa hawajaelewa na viongozi wa chama hicho madhara ya kufanya mgomo huo,zoezi lile halikufuata taratibu; 

“Noti ya kugoma iliyotolewa na CWT Julai 27 mwaka huu saa tisa alasiri wakati zoezi la upigaji kura zile lilikuwa bado halijafanyika na kwasababu hiyo zoezi lile likikuwa batili: 

 “Kwa mdaiwa(CWT) kushindwa kufuata matakwa ya kifungu cha 42 na 43 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini,ni wazi taratibu zote walizozifanya za kupiga kura ya kuunga mkono mgomo na kugoma mdaiwa alizifanya akiwa na dhamila mbaya kwani wajumbe wa chama hicho hakuwa na makubaliano ya jinsi mgomo utakavyoendeshwa na kusimamiwa”alisema Jaji Wambura huku baadhi ya walimu wakiwa wamejiinamia. 

Alisisitiza kuwa CWT imeitisha mgomo huo ikiwa na dhamira mbaya kwasababu ni CWT ndiyo alikataa kuendelea na mazungumzo na mwajiri wake badala yake akaanzisha mgomo wakati Julai 27 mwaka huu, pande zote katika hizo zilifika mbele yake kuomba na upande wa mlalamikaji ukaomba mahakama itoe amri ya kutaka pande zote zisiendelee na jambo lolote hadi mahakama itakapowasilikiliza lakini cha kushangaza siku hiyo hiyo saa tisa alasiri CWT ilienda kutoa noti ya kuanza mgomo kwa walimu nchi nzima ndani ya saa 48 wakati kulikuwa na amri ya mahakama iliyozitaka pande zote kutoendelea kufanya jambo lolote linalohusiana na kesi hiyo ambapo mgomo huo batili ulianza rasmi nchi nzima kuanzia Jumatatu ya wiki hii na hadi sasa unaendelea.

 “Kwa maelezo hayo hapo juu nasisitiza mgomo huo ni batili kwani haujakidhi matakwa ya kifungu cha 84(1),(2) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya mwaka,na mgomo uliondeshwa kwa siku tatu sasa ni batili na ninaamuru mgomo huo usitishwe mara moja na walimu wote warejee kazini na kwa kuwa mdaiwa aliitisha mgomo huo kwa mkutumia taarifa kwa vyombo vya habari pia naamuru kiongozi aliyetoa taarifa hiyo ya mgomo aende tena kwenye vyombo vya habari akatangaze kuwa mgomo waliokuwa wakiufanya ni batili na kuwataka walimu warejee kazini mara moja na mahakama hii imemshangaa sana wakili Mnyere kwa kushindwa kuwashauri wateja wake mapema kwamba mgomo waliokuwa wakiundesha ulikuwa umekiuka sheria” alisema Jaji Wambura. Aidha pia naiamuru CWT kulipa gharama na fidia kwa kipindi chote ambacho wanafunzi wamekosa vipindi kwaajili ya mgomo huo batili na kama pande zote zinaona kuna hata ya kurudi meza ya majadiliano zilirudi kwenye meza ya majadiliano na zimualike mtaalamu wa sheria za kazi awasaidie kufikia mwafaka.

 Baada ya hukumu kutolewa,baadhi ya viongozi wa CWT waliwaomba waandishi wa habari waje nje ya mahakama kwani kutakuwa na mkutano lakini hata hivyo waandishi walipofika nje ya viwanja hivyo mahakama walimkuta Rais wa chama cha walimu,Gration Mkoba akiwa amenyongonyea na hata alipotakiwa atoe tamko ni lini atatekeleza amri ya mahakama iliyomtaka aende kwenye vyombo vya habari autangazie umma kuwa mgomo alioutisha ni batili na awatake walimu warudi kazini alishia kusema leo atafanya mkutano na waandishi wa habari na kwa upande wa wakili wao Mnyere alisema amekubaliana na uamuzi huo wa mahakama.



Waziri Mkuu Mizengo Pinda Akutana na Mchungaji Park Ock Soo Muasisi Wa Tasisi ya International Youth Felloship (IYF) ya Jamhuri ya Korea

   Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akizungumza na Mchungaji Park Ock  Soo ambaye ni Muasisi wa Tasisi ya  International Youth Felloship  (IYF) ya Jamhuri ya Korea (kushoto)   kwenye makazi yake Mjini Dar es salaam Agosti 3, 2012. Kulia ni Mkurugenzi wa Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Youth Development, Dkt. Elisante Ole Gabriel na wapili kushoto ni IYF nchini  Dkt. Kansolele  Ntevi.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiagana na Muasisi wa Taasisi ya International  Youth Fellowship (IYF) ya Jamhuri ya Korea, Mchungaji Park Ock Soo baada ya mazungumzo yao kwenye makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Agosti 3, 2012.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
 
 
 

Mchezaji Mrisho Ngassa Atua Simba Sc na Kuungana na Wachezaji Wenzake Wa Simba Mazoezini

 Karibu Ngassa tufanye kazi, maisha menyewe mafupi mshikaji"Kaseja",Ngassa hakuna shaka nimekaribia swaiba. 
 Aliyekuwa mchezaji  wa Azam,Mrisho Ngassa akiwa ameegemea gari yake aliyokabidhiwa jana mara baada ya kuwasili katika ufukwe wa Coco Beach kwa kuungana na wachezaji wenzake wa Simba baada ya maridhiano ya Azam,Simba na yeye kumalizika.Picha na Mdau Machellah
 
 
 
 
 

Taswira Mbalimbali Kutoka Maonyesho ya Wakulima Nanenane Mkoani Dodoma

 Mtunzaji Kumbukumbu na Mhasibu Abbas Mnyeto wa Wizara ya Fedha wakiwasaidia wazee wastafu upande wa Kilimo juu ya taratibu za kupata pesheni kwa watumishi wanapostaafu jana mjini Dodoma walipokuwa kwenye banda la Wizara hiyo kwenye maonyesho ya wakulima nanenane.
  Afisa Malipo ya Pesheni wa Mfuko wa Pesheni kwa watumishi wa umma (PSPF) Andrew Dayson (kushoto) akiwasidia Maafisa Polisi kujua kiwango michango yao mbalimbali ambayo wamekwishachangia tangu waingie katika utumishi wa umma wakati walipotembelea banda la Wizara ya Fedha kwenye maonyesho ya wakulima ya nanenane jana mjini Dodoma.
 Kaimu Afisa Uhusiano wa wa Mfuko wa Pesheni kwa watumishi wa umma (PSPF) Hawa Kikeke(kushoto) na Afisa Malipo ya Pesheni wa Mfuko wa Pesheni kwa watumishi wa umma (PSPF) Andrew Dayson (wa pili kutoka kushoto) wakiwasaidia Maafisa wa Polisi juu ya kupata taarifa za michango yao mbalimbali ambayo wamekwishachangia tangu waingie katika utumishi wa umma wakati walipotembelea banda la Wizara ya Fedha kwenye maonyesho ya wakulima ya nanenane jana mjini Dodoma.
 Afisa Uhusiano wa Chuo Mipango Dodoma Sarah Mmari (kushoto) akimwelimisha Yulis Otto (kulia) utaratibu wa kujiunga na masomo katika Chuo hicho wakati mzee huyo alioptembelea banda la Wizara ya Fedha jana katika maonyesho yanayoendelea mjini Dodoma.
 Afisa Uhusiano wa Chuo Mipango Dodoma Sarah Mmari (kushoto) akimwelimisha Yulis Otto (kulia) utaratibu wa kujiunga na masomo katika Chuo hicho wakati mzee huyo alioptembelea banda la Wizara ya Fedha jana katika maonyesho yanayoendelea mjini Dodoma.
 Afisa Masoko kutoka Dhamana ya Uwekezaji Tanzania (UTT) Said Mkomwa(kulia) akiwaelimisha wananchi faida za kuwekeza katika mifuko iliyoanzishwa na Dhamana ya Uwekezaji Tanzania jana mjini Dodoma walipotembelea banda la Wizara hiyo kwenye maonyesho ya wakulima nanenane.
 Mwanasheria kutoka Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana Emilia Mkubulo(kulia) akimwelimisha mmoja wa wananchi faida za kununua hisa jana mjini Dodoma alipotembelea banda la Wizara hiyo kwenye maonyesho ya wakulima nanenane.
 Afisa Uendeshaji wa Mfuko wa Pesheni kwa watumishi wa umma (PSPF) Kahenga Maulid( wa pili kutoka kulia) na Afisa Malipo ya Pesheni wa Mfuko wa Pesheni kwa watumishi wa umma (PSPF) Andrew Dayson (wa pili kutoka kushoto) wakiwasaidia watumishi wa Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) Monica Kung’aro (kushoto) na Mary Kulwijila(kulia) juu ya kupata taarifa za michango yao mbalimbali ambayo wamekwishachangia tangu waingie katika utumishi wa umma wakati walipotembelea banda la Wizara ya Fedha kwenye maonyesho ya wakulima ya nanenane jana mjini Dodoma.

Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) Chasitisha Mgomo Nchi Nzima

 Rais Chama cha Walimu nchini (CWT) Mwl. Gratian Mukoba akitoa taarifa ya chama hicho
--
UONGOZI wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT), umesitisha mgomo uliokuwa unaendelea nchini, hivyo kuwataka walimu kurejea kazini.
Rais wa chama hicho, Mukoba amesema wameamua kusitisha mgomo, baada ya kuingiwa na hofu ya viongozi wao wa juu kuhofiwa kukamatwa.
 
 

WADAU SASA WAKO MSAMVU KWA MAKUTI MJINI MOROGORO

Tayari Wadau wa Tukuyu Star Family wameshawasili hapa Msamvu kwa Bi Mkora wa Maggid Mjengwa mjini Morogoro wanapata chakula cha mchana kabla ya kuendelea na safari yao kuelekea Tukuyu Mkoani Mbeya kwa ajili ya kongamano la kufufua timu ya Tukuyu Star kesho mjini Tukuyu.
Kocha Keny Mwaisabula Mzazi ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya Tukuyu Star Family akipata menyu yake kushoto kwa ke ni mchezaji wa zamani Willy Martin na wadau wengine.
Wadau wakiendelea kupata Menyu katika hoteli ya Makuti Msamvu mjini Morogoro.
Kutoka kulia ni Mdau Edward Mwakajinga, Moses Mkandawile na Peter Mwambuja wakisubiri kupata menyu yao.
 
 
 
 
 
 

MTOTO AOKOTWA PPF TOWER ALAZWA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI


Mtoto ameokotwa eneo la PPF Tower, Jijini Dar Es Salaam saa sita mchana wa leo. Amekutwa amelala chini eneo hilo.

Ameletwa Hospitali ya Taifa Muhimbili na Askari wa Central Police. Mtoto huyu anakadiriwa kuwa na umri wa mwaka mmoja na nusu hivi, kwa hiyo hawezi kuongea.

Yeyote anayemfahamu mtoto huyu au wazazi wa mtoto huyu ajitokeze na kutoa taarifa sahihi kwetu kupitia namba yangu 0755 64 86 36 au 0715 64 86 36.

Mtoto tunaye Hospitalini, anaendelea kuhudumiwa. Tafadhali sambaza barua pepe hii.

Imetolewa na;
Aminiel Buberwa Aligaesha
Afisa Uhusiano Mwandamizi
 
Hospitali ya Taifa Muhimbili
 
 
 
 

MCHAKATO WA KUIRUDISHA TUKUYU STAR WAANZA RASMI

 Wadau wa timu ya Tukuyu Star Banyambala ya Mbeya wakiwa tayari kwa safari ya kuelekea Tukuyu kwa ajili ya Kongamano la Kuifufua upya timu hiyo iliyovuma miaka ya 1980 na 1990 katika soka la Tanzania na ilifanikiwa kuchuka ubingwa wa Bara mwaka 1986. katika picha kulia ni Kocha Kenny Mwaisabula Mzazi wa pili kutoka kulia waliosimama  ambaye ndiyo kiongozi na Makamu mwenyekiti wa Tukuyu Star Family, Fullshangweblog itakuwa ikikumuvuzishia moja kwa moja matukio ya kongamano hilo kutoka mjini Tukuyu Kesho. yakirushwa na Kamanda wa Fullshangweblog John Bukuku
Hapa wadau hao wakipozi kwa picha kabla ya uanza safari hiyo maeneo ya Ubungo jijini Dar es salaam.
 
 
 
 
 
 
 
 
 

No comments:

Post a Comment