Wednesday, July 4, 2012

SHABIKI WA SIMBA AJISHINDIA PIKIPIKI KATIKA BAHATI NASIBU YA 'FAN SIMBA'


Ofisa habari wa mabingwa wa soka wa Tanzania, Simba SC, Ezekiel Kamwaga (kulia) akimkabidhi  funguo ya Pikipiki Shabiki wa timu hiyo, Abubakari Hamis (katikati) kutoka Arusha baada ya kuibuka mshindi katika bahati nasibu ya Simba Fan Club katika hafla fupi  iliyofanyika jijini Dar es Salaam, jana. Kushoto ni Meneja wa kampeni hiyo, Talib Rashid, kutoka kampuni ya Push Media Moobile. Washiriki wa bahati nasibu hiyo wanatakiwa kutuma neno Simba kwenda kwenye namba “15678” na kuingia katika droo.
************************************
Na Mwandishi wetu

KLABU ya Simba imewataka wapenzi na mashabiki wake kuendelea kujiunga na huduma ya kutuma ujumbe mfupi kupitia huduma ya Fan Simba Club ili kupata taarifa mbalimbali za Simba ikiwemo matokeo ya michuano ya kombe la Kagame  inayotarajia kuanza Julai 14 mwaka huu na masuala ya Usajili.

Akizungumza Dar es Salaam jana wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi ya pikipiki kwa mshindi wa Bahati Nasibu ya Fan Simba, Ofisa Habari wa Klabu hiyo Ezekiel Kamwaga alisema kupitia huduma hiyo mashabiki wa Simba watapokea taarifa  za kila siku  ambazo wao watakuwa wa kwanza kuzipata kupitia huduma hiyo.

Alisema pia itaisaidia klabu ya Simba kujiongezea mapato yatakayoiwezesha klabu hiyo kuendesha mambo yake katika ufanisi mkubwa ikiwa ni pamoja na kusajili wachezaji wazuri.

Kwa upande wake Meneja  Kampeni wa Kampuni ya Push Mobile Talib Rashid ambao wameingia mkataba na klabu ya Simba kupitia huduma ya sms Fan Simba Club wamefunga droo ya bahati nasibu waliokuwa wakiichezesha kwa klabu ya Simba kupitia huduma hiyo kwa kutoa pikipiki na bajaji.

Bahati nasibu hiyo iliyokuwa ikichezwa kwa kipindi cha miezi mitatu sasa imefungwa kwa kuwapata washindi ambao ni wanafunzi wa shule za Sekondari huku mmoja akiwa ni Tito Zakaria kutoka shule ya Sekondari ya Mong'ola iliyopo Dodoma aliyejishindia pikipiki na Mohamed Ibrahim kutoka shule ya Sekondari ya Chandama iliyopo Kondoa na kujishindia bajaji.

WAREMBO WA MISS VYUO VIKUU TANZANIA WATEMBELEA BUNGENI MJINI DODOMA LEO KUJIFUNZA SHUGHULI ZA BUNGE

 Warembo wanaotarajia kupanda jukwaani kuwania Taji la Miss Vyuo Vikuu 2012, siku ya Ijumaa wiki hii ndani ya Ukumbi wa Maisha Club, Jijini Dar es Salaam, wakipozi kwa picha ya pamoja nje ya Ukumbi wa Bunge, wakati warembo hao walipofika kutembelea na kujifunza shughuli za Bunge mjini Dodoma Leo. 
 Warembo wanaotarajia kupanda jukwaani kuwania Taji la Miss Vyuo Vikuu 2012, siku ya Ijumaa wiki hii ndani ya Ukumbi wa Maisha Club, Jijini Dar es Salaam, wakipozi kwa picha ya pamoja nje ya Ukumbi wa Bunge, wakati warembo hao walipofika kutembelea na kujifunza shughuli za Bunge mjini Dodoma Leo. 
 Warembo kutoka (kushoto) Migesh Boniface, kutoka Chuo cha CBE Mwanza, Hadija Said Kutoka Chuo cha MSJ, Morogoro, Fina Revocatus na Jane Maluli, wote kutoka Chuo cha IFM, wakipozi na kuonyesha smile la nguvu nje ya Ukumbi wa Bunge.
 Kutoka (kushoto) ni Mrembo Fina Revocatus, Jane Maluli, na Teddy Isaya, wote kutoka  kutoka IFM, wakipozi.
 Mrembo, Migesh Boniface, kutoka CBE Mwanza, akipozi kwa picha.
 Mrembo, Jane Maluli, kutoka IFM, akipozi kwa picha.
Kutoka (kushoto) ni Hadija Said, (MSJ) Mororogo, Renatha Richard (ST Augustino) Morogoro na Hilda Edward, kutoka Chuo cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama Dar es Salaam, wakipozi kwa picha.

No comments:

Post a Comment